CCM watelekeza mamia ya watu Mwanza waliowachukua vijijini kuwaleta kwenye maadhimisho yao

Okay, here is a suggestion: CDM wachangamkie kuwasaidia hawa watu kurudi makwao. Ili wakifika vijijini wakasimulie jinsi CCM ilivyowapeleka mjini na kuwatekeleza, hadi chama kinachojali watu cha CDM kilipojitolea kuwasaidia kurudi nyumbani.
Hakika CDM itavuna mara dufu!
Dada Leticia changamkia hii tenda ya wanaoenda Kwimba, mtaji wa imani for 2015.
Ukiwasaidia hao watasahau haraka sana na 2015 watapewa tena vi t-shirt na kofia. Bora kuwaacha hapo wasote mpaka kila mtu afike kwake kwa nguvu zake mwenyewe. Kweli Tanzania bado sana.
 
Mkuyuni wapi wewe! njoo maeneo ya Kirumba,Mwaloni na Ghana uone kumetapakaa mashati na kanga za kijani na watu wamechoka kwa njaa na kiu wanadhurura bila kujua uelekeo. Kwa kweli ukiangalia sura zao zimekata tamaa kwa kutokujua nini wafanye maana waliowaleta wame ingia mitini.
Mbaya zaidi wameanza kujisaidia hovyo maana vyoo ni vya kulipia na walio wapa ubwabwa jana hawakuwapa pesa za kulipia vyoo. Sasa hivi ni saa tisa kasoro, kuna dalili za wengi wao kushindwa kuondoka tena leo hii na hali ni mbaya sana.

mkuu hao ni wanacdm mbona hunielewi?
 
Wakuu;

Nipo mwanza na habari ni kuwa ccm wamewatelekeza watu wengi sana bila ya kuwapatia usafiri wa kurudi makwao.

Hii ni baada ya kuwasomba jana kuwaleta kwenye maadhimisho ya miaka 35 ya chama chao.

Utawahurumia akina mama wengi na baadhi ya wanaume jinsi walivyokosa matumaini kwa sababu mabasi yaliyowaleta hawayaoni na wala viongoz wa ccm hawaonekani, yaani wanahangaika kwelikweli

Ni aibu sana kwao pamoja na kujikomba bungeni kwa naibu spika kuwa uwanja ulitapika.

Wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini hawataki kusikia,wana pua lakini hwataki kunusu,sasa wasaidiweje....hiyo ndio ccm bwana,hakuna cha kuwaonea huruma,wanatakiwa wakome kujikomba komba kwa wakubwa,ccm ni ya wachache bwana,jana hiyo hiyo wenyewe wamekula flight wamerudi makwao,wengine kwenye vx zao,wao wamebaki kuchafua mji wa Mwanza tu kwa kujazana hovyo
 
CHADEMA acheni uongo, mimi niko Mwanza hapa na sioni mtu yeyote aliyekosa usafiri. Kwa kuwa majimbo yote hapa Jijini Mwanza mliyachukua sasa mlitarajia kwamba CCM wasingepata watu?
 
Kama wameweza kuwatelekeza Wagonjwa mahospitalini, wakati madaktari wamegoma, ndo watashindwa kuwatelekeza "Viherehere"! Chezea ccm wewe!!
 
hahaaaaah nasikia Nape katokomea na fuko na mshiko kwakua yeye ndio aliekua anafanya mipangilio yote ya kujua wapi na wapi wakasombwe wale watu, njaa ya pilau inawaponza
 
hahahaaa kiukweli siwahurumii hata kidogo mana hawa ndo wanatuangushaga kwenye uchaguzi kwa kupenda kwao mapilau na kofia za bwerere, wakome tena wakome kbs

Hivi nyie huwa hamna uwezo wa kugawa hayo mapilau na kofia au? Hela huwa mnapeleka wapi wakati hata kodi huwa mnakwepa kulipa?
 
hahaaaaah nasikia Nape katokomea na fuko na mshiko kwakua yeye ndio aliekua anafanya mipangilio yote ya kujua wapi na wapi wakasombwe wale watu, njaa ya pilau inawaponza

Huna cha kuchangia zaidi ya kuona kuwa uongo wako nao ni point?
 
Sio ya ccm kumbaff weee hao ni wanamchi fukara waliodanganyika sio kwa mapenzi yao kwa ccm bali kwa njaa umasikini na ujinga waliopandikiziwa na ccm. Hivyo unafikiri wakipata matatizo sisi kama wananchi tusihoji?kwa kuwa eti ni ya ccm?hao ni baba na mama zetu pia kaka na dada zetu. Ucheni ukatili huo!!
Mkuu hachana nae huyo anaejiita raia mwema,anaonyesha ni kiasi gani ni mvivu wa kufikiri,ila simlaumu,unaua ukishakua "msahadadiaji" wa magamba lazima uwe mvivu kifikra
 
Hivi nyie huwa hamna uwezo wa kugawa hayo mapilau na kofia au? Hela huwa mnapeleka wapi wakati hata kodi huwa mnakwepa kulipa?

Sasa uwezo wa kugawa pilau na kofia ndio msingi wa kuwajengea wananchi uwezo wa kimaendeleo?ebu fikiria kwanza kabla ya kusema mkuu,au na wewe ni walewale ambao magamba ndio mtaji wao?na suala la kukwepa kodi ebu lianike wazi hapa with evidence
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari


Propadanda nyingine bwana! Kwanini useme ni sh. 200 wakati ni sh. 100? Wakati huu unataka watu waamini kwamba CHADEMA walisomba watu na kuwaleta kwenye maadhimisho ya CCM wakawapa tisheti na kofia alafu baadae wakawatelekeza? Bytheway Msosi ulitosha, ni shilingi ngapi zilitumika?
 
Kama wameweza kuwatelekeza Wagonjwa mahospitalini, wakati madaktari wamegoma, ndo watashindwa kuwatelekeza "Viherehere"! Chezea ccm wewe!!

Kwani jana hawakumuelewa JK ....ALIWAAMBIA " Tatizo lenu kubwa ni Njaa Zenu".....chezea mkweree anatukana wewe huku unajiona....unacheka kumbe unatukanwa weye...
Wazee wangu jana walisombwa toka vijijini .....wakapewa visenti,wakalazwa gesti..na kuchinjiwa magombe 50...............uwanjani kikwete akawaambia.." kweli wazee wanaume wazima na wanawake wazima...mnachukuliwa mnapewa visenti mnawekwa gesti?? ......tatizo lenu kubwa ni njaa zenu"................hicho kijembe alikitoa kwa mwavuli wa nukuu ya rafiki yake mpenzi Ditopile wa Mzuzuri........
So sad ...wana mwanza wazee wenu na mama zenu kutukanwa .....na wasielewe asilani ,waakabaki wanamkenulia meno JK...Tatizo lau kubwa wana mwanza nikukubali kupokea pesa za nape na kula pilau yake ..sasa malipo yake ..kawalipa Kikwete....Kawapashaaa!!!

Kweli akutukanae hakuchagulii tusi!
 
I like CCM watu wa Mwanza wameweka serikali ya CDM madarakani wanapelekewa wali ngombe na CCM wanaenda acha waadhibiwe, wamewapata acha wawachape kwa kutoichagua ccm kwa nn hawakupeleka sherehe Tabora au Bgmyo? Mwanza madiwani wengi ni wa cdm wabunge cdm halmashauri ya cdm utawezaje kufanya sherehe nyumbani kwa mtu ukaacha kwako? Any way hao ni ndugu zetu makamanda wawakusanye wawape darasa la elimu ya uraia kisha muwapenauli ya kurudi kwao wapewe kadi na kofia za chadema au bendera ndogo ndogo nina hakika hawatakaa waisahau cdm maishani mwao.
 
leteni picha jamani mbona maneno mengi... Ningependa sana kuona picha
 
Inaonekana Chadema umati wa jana wa CCM hamkutarajia bado mna weweweseka! Acheni propaganda za Kitoto Chadema na Uzushi wenu! Hao watu wapo uwanjani? Upuuuuuuuzi tu mnaendekeza hapa JF
 
Back
Top Bottom