CCM watangaza kumshtaki Zitto kwa kuwadhalilisha

Ccm wamejitokeza kutishia kuwa wataenda mahakamani ili kutupoteza maboya. Ni hivi malalamiko ya Zitto kuhusu huu uhuni ni ya kweli, ila waneshampooza Zito na chochote kitu kama kawaida yake, hatimaye Zito kabadili kauli, na ccm nao wakatoka na kauli ya kufunika ukweli.

Uchaguzi huu ni wa ajabu kidogo, hakuna matokeo rasmi mpaka sasa, wala picha za misururu ya wapiga kura ili tupime imani ya wapiga kura kwenye box la kura.
Ni Chadema pekee huwalazimisha CCM kutafuta kura feki kwenye mabegi meusi, ndio maana Zitto hupenda sana kushirikiana na Chadema wakati wa uchaguzi coz anajua anataka kutumia mgongo wa Chadema kufika anapotaka, kinyume na hapo CCM wanashinda kihalali kabisa, hakuna upinzani makini Tz nje ya Chadema, ACT bado wachanga sana field, ni mbwembwe za mitandaoni tu ndio zinawadanganya wanajiona wapo juu.

Zitto kusema kavamiwa na mapanga bila kuumizwa, bila kuyapiga picha, lakini hapo hapo wanatuonesha picha za magari na plate number, kwann wasingepiga picha na hayo mapanga? hawa jamaa siwezi kuwaamini, na huyu Zitto kwa kukurupuka kwake ataanza kuwarudishia CCM legitimacy waseme huwa wanashinda chaguzi kihalali hata kama huwa wanaiba kura.
 
Baada ya kiongozi ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kudai kuvamiwa na gari tatu za CCM, Katibu wa chama hicho tawala Mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema wanasubiria matokeo yatangazwe wafungue jalada mahakamani la kudhalilishwa na kiongozi huyo.

"Sisi kwenye kampeni tulikuwa na magari 48 katika Jimbo la Muhambwe pekee sawa na gari mbili kila kata sasa yeye kaona magari yanapita kwenye vituo huko akaanza kusambaza taarifa yanasambaza kura bandia tutamchukulia hatua baada ya matokeo kutangazwa," amesema Vyohoroka.

Mwenyekiti huyo wa ACT Wazalendo alituma ujumbe mfupi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter uliosomeka," tumetoka polisi. OCD wa Kibondo ametusaidia sana. Tupo salama. Tunaendelea kulinda ushindi wetu hapa Muhambwe mpaka mwisho. Polisi wamefanya kazi kwa weledi kabisa. Ni hatua kubwa.”

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama alisema tuhuma hizo sio za kweli huku akiwahakikishia wakazi wa jimbo hilo kwamba jeshi hilo halijapokea taarifa yoyote ya uwepo wa kura bandia.

Mwananchi
Ninyi wanasiasa nawachukia sana maana wote ni majambazi tu wa kujilimbikizia malii za Watanzania
 
Ccm ni chama cha majambazi! Hivyo huwezi kukitenganisha na wizi wa kura, wizi wa mali za umma, uporaji, uhujumu uchumi, ujangili, ufisadi, nk.
 
Ni Chadema pekee huwalazimisha CCM kutafuta kura feki kwenye mabegi meusi, ndio maana Zitto hupenda sana kushirikiana na Chadema wakati wa uchaguzi coz anajua anataka kutumia mgongo wa Chadema kufika anapotaka, kinyume na hapo CCM wanashinda kihalali kabisa, hakuna upinzani makini Tz nje ya Chadema, ACT bado wachanga sana field, ni mbwembwe za mitandaoni tu ndio zinawadanganya wanajiona wapo juu.

Zitto kusema kavamiwa na mapanga bila kuumizwa, bila kuyapiga picha, lakini hapo hapo wanatuonesha picha za magari na plate number, kwann wasingepiga picha na hayo mapanga? hawa jamaa siwezi kuwaamini, na huyu Zitto kwa kukurupuka kwake ataanza kuwarudishia CCM legitimacy waseme huwa wanashinda chaguzi kihalali hata kama huwa wanaiba kura.

Ni vizuri Zito kushiriki mwenyewe sasa ili kila aliyekuwa haamini yasemwayo kuhusu Zito awe na ushahidi usioacha shaka. Na ile jeuri ndogo aliyokuwa nayo Zito sasa amejua fika nguvu yake iko wapi.

Nimejaribu kumuuliza kila social media aliyoko aweke picha ya misururu ya wapiga kura, ili tuone imani waliyo nayo wapiga kura. Naona hilo sio yeye wala Nape wamethubutu kujibu. Ni kwamba kwa sasa wananchi wengi wamepoteza imani ya box la kura, hivyo ccm ndio wanapaswa wajitafakari sana kuliko hata ACT kwenye uchaguzi huu na zijazo.
 
Back
Top Bottom