CCM watangaza kumshtaki Zitto kwa kuwadhalilisha

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Baada ya kiongozi ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kudai kuvamiwa na gari tatu za CCM, Katibu wa chama hicho tawala Mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema wanasubiria matokeo yatangazwe wafungue jalada mahakamani la kudhalilishwa na kiongozi huyo.

"Sisi kwenye kampeni tulikuwa na magari 48 katika Jimbo la Muhambwe pekee sawa na gari mbili kila kata sasa yeye kaona magari yanapita kwenye vituo huko akaanza kusambaza taarifa yanasambaza kura bandia tutamchukulia hatua baada ya matokeo kutangazwa," amesema Vyohoroka.

Mwenyekiti huyo wa ACT Wazalendo alituma ujumbe mfupi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter uliosomeka," tumetoka polisi. OCD wa Kibondo ametusaidia sana. Tupo salama. Tunaendelea kulinda ushindi wetu hapa Muhambwe mpaka mwisho. Polisi wamefanya kazi kwa weledi kabisa. Ni hatua kubwa.”

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama alisema tuhuma hizo sio za kweli huku akiwahakikishia wakazi wa jimbo hilo kwamba jeshi hilo halijapokea taarifa yoyote ya uwepo wa kura bandia.

Mwananchi
 
Zitto ameshapata majibu yake ya kumjaribu mama, siasa ni ushindani na kukubalika kwa mgombea wako, usitegemee kushinda bila maandalizi yoyote, hakuna majaribio kwenye mambo ya msingi hata siku moja.

Chama lazima kiwe na misingi inayoekeweka kwanza kabla ya kukimbilia kushiriki uchaguzi, au angesubiri kushirikiana na Chadema kama alivyozoea, na hayo madai yake yote yanapoteza maana kwasababu alishaambiwa toka mwanzo CCM ni wale wale akakaza shingo.
 
Zitto ni mjasiriamali wa siasa
 
Ccm wamejitokeza kutishia kuwa wataenda mahakamani ili kutupoteza maboya. Ni hivi malalamiko ya Zitto kuhusu huu uhuni ni ya kweli, ila waneshampooza Zito na chochote kitu kama kawaida yake, hatimaye Zito kabadili kauli, na ccm nao wakatoka na kauli ya kufunika ukweli.

Uchaguzi huu ni wa ajabu kidogo, hakuna matokeo rasmi mpaka sasa, wala picha za misururu ya wapiga kura ili tupime imani ya wapiga kura kwenye box la kura.
 
Drama za watoto wa familia moja hizi
Maneno ya mtu aliyekata tamaa kabisa haya, siasa ni Sanaa, hamna cha sayansi wala Nini, wenzenu CCM wanajua sana kucheza na hii fani, ghafla bin vuuu Wana mwenezi mpya, katibu mkuu mpya, Mwenyekiti mpya.... nyie bado sura zenu ni zile zile, stori zenu ni zile zile za kipindi kile....kazi mnayo...

Upinzani mpaka leo mnashindwa kwenda na step za hii fani, mnatunyima sana raha wapenzi watazamaji, we ona jinsi Harmonize anavyoserebuka na style za wasafi na jinsi zilivyomuwezesha kukaa kileleni. Ukiona chongo ita/ jifanye makengeza.

Kulikuwa na zama za pop, baadae bomblast, saizi tuna wabana pua na trap, mambo yanachange nyie mmeng'ang'ania miungu watu, hamna alternatives?
 
Nina hakika hujui ulichoandika
 
Back
Top Bottom