CCM wataka posho, CUF wauana , NCCR wavunja chama, CHADEMA je mko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wataka posho, CUF wauana , NCCR wavunja chama, CHADEMA je mko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Dec 15, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Posho zaipasua CCM
  • Wangelipwa 43,560,000/- kwa mwaka
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] UAMUZI uliotolewa juzi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupinga ongezeko la posho za wabunge, kumezua tafrani ya aina yake kutoka kwa wabunge wa chama hicho.


  Juzi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipinga nyongeza za posho kama zilivyotangazwa na Spika wa Bunge na kikawataka wabunge wake kutafakari na kuacha kuzipokea.
  Wabunge kadhaa wa CCM wamepinga tamko hilo wakishikilia msimamo wao wa kutaka wapewe nyongeza za posho za vikao kutoka sh 70,000 hadi sh 200,000 kwa madai kuwa sababu zilizotolewa na Spika Anne Makinda ni za msingi.
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] CUF watwangana

  • Mmoja adaiwa kuvunjwa mkono  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] VUGURU kubwa zilizosababisha kuharibiwa kwa magari na watu kadhaa kujeruhiwa vibaya zilizuka jana kati ya makundi mawili ya wafuasi wa viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohamed.

  Mapigano hayo makali yalizuka baada ya kundi kubwa la vijana walinzi maarufu kama ‘Green Gurds’ waliokuwa wamebeba mapanga, visu na nondo kutoka makao makuu ya CUF kuvamia ziara ya mbunge huyo eneo la Mabibo, jijini Dar es Salaam wakiwa na nia ya kuzuia mikutano yake.
  Tanzania Daima lililokuwa katika eneo hilo, lilishuhudia kundi hilo la vijana lililowasili katika eneo la Mabibo kwenye Tawi la Chechnya ambako Hamad Rashid alikuwa akitangaza nia ya kuwania ukatibu mkuu, na kuanza kumshusha kwa nguvu kutoka katika jukwaa alikokuwa akihutubia.

  Mara baada ya kutulia kwa mapigano hayo, Hamad Rashid alilaani kitendo cha kuvamiwa na kundi la wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad, akisema kuwa ataendelea na dhamira yake ya kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa CUF, ikiwa ni pamoja na kukifufua chama hicho ambacho alidai kuwa kimedodora.  KAFULILA AVULIWA UONGOZI NCCR- MAGEUZI


  Wakati hali ikiwa tete katika Chama cha CUF, mzozo mwingine mkubwa ambao umeibuka ndani ya Chama cha NCCR- Mageuzi umefikia hatua mbaya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Samuel Ruhuza, kumvua madaraka ya Ukatibu Mwenezi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
  Akizungumza na gazeti hili jana jioni kwa njia ya simu, Kafulila alikiri kupokea barua ya kuvuliwa wadhifa huo kutoka kwa Ruhuza, akisema ameambiwa kuwa hayo ni mamlaka ambayo anaweze kupewa na kuondolewa.
  “Ni kweli nimepokea barua lakini mimi sijaona tatizo lolote kwani sikuomba nafasi hiyo bali niliomba ubunge. Ujue hadhi ya ubunge ni kubwa kuliko katibu mwenezi, hivyo nimejulikana na kuheshimika kwa wadhifa wa ubunge,” alisema.
  Alifafanua kuwa ana uhakika shinikizo la kuondolewa kwake limetoka kwa Mbatia, kwani ameonesha wazi kuwa hamtaki yeye pamoja na Mbunge wa Mhambwe, Felix Mkosamali, kutokana na kutofautia naye.
  “Mbatia hata yeye ubunge anajua una hadhi kuliko hata uenyekiti wake, ndiyo maana aliomba kura Jimbo la Kawe lakini akashindwa. Ila anajua hali ni ngumu na anaweza kuangushwa kwenye NEC ijayo, hivyo anadhani mchawi wake ni mimi na Mkosamali,” alisema Kafulila.


  ZITO(CHADEMA) AMKINGIA KIFUA NAPE


  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), ameutaka umma usimbeze Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye juu
  ya tamko lake la kupinga posho mpya za wabunge kwa kusema alichofanya ni hekima za harakati.


  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]Zito alisema, “Hii ndio
  huitwa hekima za harakati.

  Nimesikitishwa sana na wanaobeza kauli ya Nape kuhusu posho za wabunge.”

  Akiendelea kusisitiza Nape aungwe mkono, Zitto alisema, “Lengo letu haswa nini? Kwamba
  Zitto aonekane mshindi? Hapana.


  Kwamba Chadema ionekane mshindi? Hapana.
  Lengo letu ni kuondoa posho za vikao kwa
  wabunge na viongozi wa umma.

  Lengo letu ni mwananchi wa Tanzania ashinde kwa kupunguza matumizi mabovu. Ye yote anayeunga mkono lengo hilo tunapaswa kumwunga mkono”.

  HII NDO SIASA YA TANZANIA HIVI SASA.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Chadema inatowa elimu ya uraia juu ya kuundwa katiba mpya, hizo sarakasi za vyama vingine ni janja ya CCM kutuondoa attention yetu kwenye hoja muhimu ya katiba. waache wafu wazikane wao wenyewe.
   
 3. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Tayari nimeishasahau kama kuna mchakato wa katiba, hivi huu mchakato umefikia wapi???
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  heee wewe magamba mbona mwepesi sana wa kusahau,
  Itakuwa umesahau kuwa babu wa loliondo alikuwa anatoa kikombe!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Siasa za Tanzania sasa ni segemnege!
   
 6. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Kwani siku hizi njia zinapitika,, maana ccm's kada walikunywa sana ,, je walipona akina magufuli, Mkono, jk, na wenzake?? au ilikuwa danganya toto???

  siasa ya tanzania ni bora ya vyuo vikuu imetulia kidogo na mambo yao yanaendeshwa kitaaluma zaidi,
   
 7. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Achana na NCCR kwa sababu ni CCM B toka enzi za mrema we si unaona hata baada ya Mrema kwenda TLP nayo iko taaban inaishi kwa huruma ya CCM,Hao CUF ndo usiseme waliyataka wenyewe waliponyang'anywa Ushindi wa visiwani kwa kuahidiwa U-makamu, kwa hiyo chama cha upinzani kilichobaki ambacho ni matumaini makubwa kwa watz ni CHADEMA Only.
   
 8. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa Posho, pale Migogoro ndani ya vyama, kule katiba mpya na huku Jairo scandal tuanze na lipi? Hao wanataka kutuletea delay technique ili kutusahaulisha, tukomae nao mpaka kieleweke.
   
 9. d

  dada jane JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Matola umenena.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  We acha tu. Yaani shida rupu, sijui 2015 tutafanya nini! NI dalili kuwa tunaelekea kuchagua makapi tena
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo mleta mada unataka na cdm iingie kwenye mgogoro?
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Cdm kuna mgogoro mkubwa tu mmesahau ya shibuda,zitto na harakati zake za kugombea urais 2015 na bila kusahau Selasini ambae kiulisia sio cdm ila wana cdm wenyewe hawajui hilo
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Asiyejua maana Aambiwi maana
   
 14. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Hapana mie naona hapa CHADEMA kiwe mshauli wa hivi vyama kwa hiki kipindi kigumu.
   
 15. e

  evoddy JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  CHADEMA kazi yetu ni kujenga hoja za msingi kwa wananchi ili waondokane na siasa uchwala na za jino kwa jino.Hatuna muda wa kurushiana makonde na ndiyo maana hatuna vikundi vya ulinzi kama wenzetu
   
 16. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  akili za bata wa nchi kavu hizi, Zitto atakuwa na umri gani 2015??
  Hiyo ya selasini, wewe ni mkewe? Alikuambia kwamba yeye sio cdm kwenye bed talk?
  Uhuru wa kuropoka huu.
   
 17. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inteligensia ya Mwema ambayo huwa inatabiri vurugu kwenye mikutano chadema ilikuwa wapi kwa CUF?Nawapa big up CDM manake wameonyesha ukomavu tofauti na wanavyokichafua kuwa ni chama cha vurugu.Wametuita wazururaji mara wavuta bangi lakini sasa ndio wamejua kumbe bangi ya siku hizi inafaa na haina madhara.
   
 18. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  CDM ni chama dume, hiyo stage ambayo hivyo vyama vinapitia CDM waliishaipitia zamani, miaka ya 1992 to 1995 wakati chama ni kichanga
   
 19. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siasa zetu bwana!!!!!! Najisikia kichefuchefu ngoja nikatapike kwanza nitarudi baadae!!!!!
   
 20. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Tanzania hakuna upinzani, vyama vyote ni makundi ya CCM.
   
Loading...