CCM wataka Maalim Seif akamatwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Maalim Seif.jpg
Sheni.jpg
CCM.jpg

Wakati zikiwa zimebaki siku 21 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na hoja ya kutaka mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akamatawe na kuwekwa ndani kwa madai ya kujitangazia ushindi kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar jana, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu, alisema Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, anapaswa kukamatwa na Jeshi la Polisi na kufunguliwa mashitaka ya kujitangaza mshindi wa urais wa visiwa hivyo baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 kabla ya kufutwa siku tatu baadaye na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Kabla ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi Oktoba 28, 2015, Maalim Seif aliwaambia waandishi wa habari kuwa matokeo rasmi waliyo nayo, na ambayo walikuwa wameyapata kutoka kwa mawakal wao katika vituo vyote vya uchaguzi visiwani humo, yalionyesha kuwa yeye anaongoza kwa kupata asilimia 52.87 ya kura zote na kumuacha mpinzani wake, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na hivyo akaitaka ZEC itende uadilifu kwa kutangaza mshindi halali wa uchaguzi huo.

Hata hivyo, akizungumza jana, Jabu alisema Maalim Seif alikiuka sheria za uchaguzi na hivyo anastahili kukamatwa na kufunguliwa mashitka yake.

“Kitendo cha Maalim Seif kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa ameshinda urais Oktoba 25 mwaka uliopita kabla ya kura kuhakikiwa na kutangazwa na ZEC ambayo ndiyo yenye dhamana ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar na kingeweza kuleta mtafaruku wa kisiasa,” alisema Waride, aliyekuwa ameongozana na kiongozi mwingine wa juu katikaa idara yake, Moderine Castico.

Aidha, alisema CCM ingependa kuona watu wote walioshiriki kuvuruga uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.

Alieleza kuwa uchaguzi uliovurugika umeipa hasara kubwa serikali lakini inashangaza kwamba hakuna hata mtendaji mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kuhusika na kosa hilo.

Kuhusu wasiwasi wa kukwama kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kama vyama vinavyoshiriki vitashindwa kukamilisha masharti ya katiba baada ya CUF kususia uchaguzi wa marudio, Waride alisema vyama vinavyoshiriki visidharauliwe na wala hakuna haki ya kuvipuuza.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema Maalim Seif hana kosa alilofanya kwa madai ya kutangaza mwelekeo wa matokeo kabla ya tume ya uchaguzi.

Alisema taarifa alizotangaza ni matokeo yaliyokusanywa na mawakala wake katika majimbo na ndiyo kazi yao kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

“Vyombo vya sheria vinatambua hakuwa na makosa kutangaza mwelekeo wa uchaguzi na kwamba, matokeo rasmi hutangazwa na tume ya uchaguzi,” alisema Shehe.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Zanzibar (DDCI), Salum Msangi, alisema jana kuwa uchunguzi wa jalada la Maalim Seif la kudaiwa kujitangaza mshindi umekamilika na kukabidhiwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim, tangu mwaka jana.

Mbali na jalada la Maalim Seif, pia alisema majalada mengine ambayo hadi sasa yapo kwa DPP ni pamoja na watendaji wa ZEC waliohusika kuvuruga uchaguzi wa Oktoba 25.

Juhudi za kumpata DPP Ibrahim Mzee Ibrahim kujua mwenendo wa majalada aliyodai DDCI kuwa yamekamilika hazikufanikiwa baada ya simu yake kuwa imezimwa.

chanzo.Ccm wataka maalim akamatwe - Mzalendo.net

Na CCM unguja wakimakamata Maalim seif watakuwa wanamzidishia Umaarufu zaidi Duniani itatambuwa kuwa Chama Cha Mapinduzi Unguja hakina haki za kibinadamu. Vikwazo vya Uchumi vitakuja nchini Tanzania dhidi ya kukamatwa Maalim seif Mawazo yangu binafsi.
 
Nami ningekuwa ndio naongiza vyombo vya dola hasa police huyo jamaa mpaka sasahv hukumu yake ishatoka ata huko mahakan… maana kujitangazia matokeo ni.kosa kwa mujibu wa sheria na adhabu yake kifungo cha miaka 5 au faini Tsh 500,000/= ay vyote kwa pamoja , sasa watu kama hawa unawalimisha vyua tano ili ujinga ufie mbali.
 
Mbona hawakuyasema haya siku hiyo alipojitangaza? Walikua wapi siku zote? Yaani makamu wa Rais anakamatwa kama kibaka tu hivyo? Binadam wengine bhana.
 
Nami ningekuwa ndio naongiza vyombo vya dola hasa police huyo jamaa mpaka sasahv hukumu yake ishatoka ata huko mahakan… maana kujitangazia matokeo ni.kosa kwa mujibu wa sheria na adhabu yake kifungo cha miaka 5 au faini Tsh 500,000/= ay vyote kwa pamoja , sasa watu kama hawa unawalimisha vyua tano ili ujinga ufie mbali.
poor thinking
 
Hili povu lote ni kwa sababu tu amekataa kushiriki uchaguzi!
 
Nami ningekuwa ndio naongiza vyombo vya dola hasa police huyo jamaa mpaka sasahv hukumu yake ishatoka ata huko mahakan… maana kujitangazia matokeo ni.kosa kwa mujibu wa sheria na adhabu yake kifungo cha miaka 5 au faini Tsh 500,000/= ay vyote kwa pamoja , sasa watu kama hawa unawalimisha vyua tano ili ujinga ufie mbali.
Kwa mawazo yako haya utakua product ya SAUT au kile kichofungwa juzi..
 
Nyie CCM, msiwafanye Watanzania mburura kama nyie. Tuelezeni adhabu ya mtu kujitangazia ushindi kabla ya tume ya uchaguzi. Adhabu hii ipo. Mbona hamkufanya?

Alichofanya Maalim Seif Shariff Hamad ni kujumlisha matokeo yaliyokwishwa tangazwa na tume ya uchaguzi vituo husika na washindi kupewa vyeti. Hiyo hoja yenu inatoka wapi?

Ukanamizaji mnaofanya mtaulipa mbele ya umma. Nchi hii si mali yenu na haitakuwa mali yenu. Uovu wowote ule hauna umilele. Mwenye umilele ni Alah au Mungu. Hatuwezi kuchukua nafasi yake. Hakuna dola yoyote duniani iliyodumu milele. Soma historia ya ulimwengu vizuri!!!!

Mnarudia uchaguzi kwa lengo lipi hasa kama kosa ni mtu kujitangazia ushindi? Mbona sheria inasema wazi kwa mtu kujitangazia ushindi? Haki hiyo Jecha kaitoa wapi? Mbona mwawafanya Watanzania mburura?

Hakika nawaambieni, hata mkishinda kwa kulazimisha kurudia uchaguzi hamtakuwa salama. Na huu ndio mwisho wenu!!!! Mwisho wa ubaya ni AIBU. Mjiandae kwa aibu hiyo!
 
Nami ningekuwa ndio naongiza vyombo vya dola hasa police huyo jamaa mpaka sasahv hukumu yake ishatoka ata huko mahakan… maana kujitangazia matokeo ni.kosa kwa mujibu wa sheria na adhabu yake kifungo cha miaka 5 au faini Tsh 500,000/= ay vyote kwa pamoja , sasa watu kama hawa unawalimisha vyua tano ili ujinga ufie mbali.
Wewe huna akili wala busara ya kumshinda mwenyekiti wako jk,
 
View attachment 326310 View attachment 326311 View attachment 326312

Wakati zikiwa zimebaki siku 21 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na hoja ya kutaka mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akamatawe na kuwekwa ndani kwa madai ya kujitangazia ushindi kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar jana, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu, alisema Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, anapaswa kukamatwa na Jeshi la Polisi na kufunguliwa mashitaka ya kujitangaza mshindi wa urais wa visiwa hivyo baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 kabla ya kufutwa siku tatu baadaye na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Kabla ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi Oktoba 28, 2015, Maalim Seif aliwaambia waandishi wa habari kuwa matokeo rasmi waliyo nayo, na ambayo walikuwa wameyapata kutoka kwa mawakal wao katika vituo vyote vya uchaguzi visiwani humo, yalionyesha kuwa yeye anaongoza kwa kupata asilimia 52.87 ya kura zote na kumuacha mpinzani wake, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na hivyo akaitaka ZEC itende uadilifu kwa kutangaza mshindi halali wa uchaguzi huo.

Hata hivyo, akizungumza jana, Jabu alisema Maalim Seif alikiuka sheria za uchaguzi na hivyo anastahili kukamatwa na kufunguliwa mashitka yake.

“Kitendo cha Maalim Seif kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa ameshinda urais Oktoba 25 mwaka uliopita kabla ya kura kuhakikiwa na kutangazwa na ZEC ambayo ndiyo yenye dhamana ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar na kingeweza kuleta mtafaruku wa kisiasa,” alisema Waride, aliyekuwa ameongozana na kiongozi mwingine wa juu katikaa idara yake, Moderine Castico.

Aidha, alisema CCM ingependa kuona watu wote walioshiriki kuvuruga uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.

Alieleza kuwa uchaguzi uliovurugika umeipa hasara kubwa serikali lakini inashangaza kwamba hakuna hata mtendaji mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kuhusika na kosa hilo.

Kuhusu wasiwasi wa kukwama kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kama vyama vinavyoshiriki vitashindwa kukamilisha masharti ya katiba baada ya CUF kususia uchaguzi wa marudio, Waride alisema vyama vinavyoshiriki visidharauliwe na wala hakuna haki ya kuvipuuza.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema Maalim Seif hana kosa alilofanya kwa madai ya kutangaza mwelekeo wa matokeo kabla ya tume ya uchaguzi.

Alisema taarifa alizotangaza ni matokeo yaliyokusanywa na mawakala wake katika majimbo na ndiyo kazi yao kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

“Vyombo vya sheria vinatambua hakuwa na makosa kutangaza mwelekeo wa uchaguzi na kwamba, matokeo rasmi hutangazwa na tume ya uchaguzi,” alisema Shehe.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Zanzibar (DDCI), Salum Msangi, alisema jana kuwa uchunguzi wa jalada la Maalim Seif la kudaiwa kujitangaza mshindi umekamilika na kukabidhiwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim, tangu mwaka jana.

Mbali na jalada la Maalim Seif, pia alisema majalada mengine ambayo hadi sasa yapo kwa DPP ni pamoja na watendaji wa ZEC waliohusika kuvuruga uchaguzi wa Oktoba 25.

Juhudi za kumpata DPP Ibrahim Mzee Ibrahim kujua mwenendo wa majalada aliyodai DDCI kuwa yamekamilika hazikufanikiwa baada ya simu yake kuwa imezimwa.

chanzo.Ccm wataka maalim akamatwe - Mzalendo.net

Na CCM unguja wakimakamata Maalim seif watakuwa wanamzidishia Umaarufu zaidi Duniani itatambuwa kuwa Chama Cha Mapinduzi Unguja hakina haki za kibinadamu. Vikwazo vya Uchumi vitakuja nchini Tanzania dhidi ya kukamatwa Maalim seif Mawazo yangu binafsi.
CCM inasema mkamateni DCI anasema jalada limeshakamilika Daaah
 
Kama uchaguzi ulifutwa kwa kuwa Maalim Seif kajitangaza mshindi wa urais, je ni nani alijitangaza mshindi wa uwakilishi hadi uchaguzi huo ukafutwa? Ni nani alijitangaza mshindi wa udiwani hadi nao ukafutwa. Kama makosa yalikuwa kwa Maalim Seif na kujitangaza mshindi urais, je kwa nini matokeo ya uwakilishi na udiwani yalifutwa?
 
View attachment 326310 View attachment 326311 View attachment 326312

Wakati zikiwa zimebaki siku 21 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na hoja ya kutaka mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akamatawe na kuwekwa ndani kwa madai ya kujitangazia ushindi kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar jana, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu, alisema Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, anapaswa kukamatwa na Jeshi la Polisi na kufunguliwa mashitaka ya kujitangaza mshindi wa urais wa visiwa hivyo baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 kabla ya kufutwa siku tatu baadaye na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Kabla ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi Oktoba 28, 2015, Maalim Seif aliwaambia waandishi wa habari kuwa matokeo rasmi waliyo nayo, na ambayo walikuwa wameyapata kutoka kwa mawakal wao katika vituo vyote vya uchaguzi visiwani humo, yalionyesha kuwa yeye anaongoza kwa kupata asilimia 52.87 ya kura zote na kumuacha mpinzani wake, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na hivyo akaitaka ZEC itende uadilifu kwa kutangaza mshindi halali wa uchaguzi huo.

Hata hivyo, akizungumza jana, Jabu alisema Maalim Seif alikiuka sheria za uchaguzi na hivyo anastahili kukamatwa na kufunguliwa mashitka yake.

“Kitendo cha Maalim Seif kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa ameshinda urais Oktoba 25 mwaka uliopita kabla ya kura kuhakikiwa na kutangazwa na ZEC ambayo ndiyo yenye dhamana ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar na kingeweza kuleta mtafaruku wa kisiasa,” alisema Waride, aliyekuwa ameongozana na kiongozi mwingine wa juu katikaa idara yake, Moderine Castico.

Aidha, alisema CCM ingependa kuona watu wote walioshiriki kuvuruga uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.

Alieleza kuwa uchaguzi uliovurugika umeipa hasara kubwa serikali lakini inashangaza kwamba hakuna hata mtendaji mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kuhusika na kosa hilo.

Kuhusu wasiwasi wa kukwama kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kama vyama vinavyoshiriki vitashindwa kukamilisha masharti ya katiba baada ya CUF kususia uchaguzi wa marudio, Waride alisema vyama vinavyoshiriki visidharauliwe na wala hakuna haki ya kuvipuuza.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema Maalim Seif hana kosa alilofanya kwa madai ya kutangaza mwelekeo wa matokeo kabla ya tume ya uchaguzi.

Alisema taarifa alizotangaza ni matokeo yaliyokusanywa na mawakala wake katika majimbo na ndiyo kazi yao kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

“Vyombo vya sheria vinatambua hakuwa na makosa kutangaza mwelekeo wa uchaguzi na kwamba, matokeo rasmi hutangazwa na tume ya uchaguzi,” alisema Shehe.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Zanzibar (DDCI), Salum Msangi, alisema jana kuwa uchunguzi wa jalada la Maalim Seif la kudaiwa kujitangaza mshindi umekamilika na kukabidhiwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim, tangu mwaka jana.

Mbali na jalada la Maalim Seif, pia alisema majalada mengine ambayo hadi sasa yapo kwa DPP ni pamoja na watendaji wa ZEC waliohusika kuvuruga uchaguzi wa Oktoba 25.

Juhudi za kumpata DPP Ibrahim Mzee Ibrahim kujua mwenendo wa majalada aliyodai DDCI kuwa yamekamilika hazikufanikiwa baada ya simu yake kuwa imezimwa.

chanzo.Ccm wataka maalim akamatwe - Mzalendo.net

Na CCM unguja wakimakamata Maalim seif watakuwa wanamzidishia Umaarufu zaidi Duniani itatambuwa kuwa Chama Cha Mapinduzi Unguja hakina haki za kibinadamu. Vikwazo vya Uchumi vitakuja nchini Tanzania dhidi ya kukamatwa Maalim seif Mawazo yangu binafsi.
Kijana unajisumbua na Maalim....huyu ni CCM wala usijisumbue!
 
Hahaaa. Ccm walichelewa kujitangazia Zanzibar ushindi kama huku bara walivyofanya sasa wana haha.
 
Nami ningekuwa ndio naongiza vyombo vya dola hasa police huyo jamaa mpaka sasahv hukumu yake ishatoka ata huko mahakan… maana kujitangazia matokeo ni.kosa kwa mujibu wa sheria na adhabu yake kifungo cha miaka 5 au faini Tsh 500,000/= ay vyote kwa pamoja , sasa watu kama hawa unawalimisha vyua tano ili ujinga ufie mbali.
Si ajabu na wewe ulimaliza hata darasa la saba!!
 
Back
Top Bottom