CCM washikwa wakigawa sare na hela Igunga

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
1. Nimepata simu kutoka kwa makamanda walioko uwanja wa mapambano, Igunga kuwa mnamo saa mbili na nusu usiku huu, Vigogo kadhaa wa CCM walikuwa wanagawa sare na fweza kwa wanawake waliokusanywa eneo la hospitali ya wilaya ya Igunga.

2. Kumeitishwa mdahalo kati ya wagombea wa Ubunge jimbo la Igunga ... mpaka sasa mdahalo unaendelea.

Mlioko Igunga, Tunaomba picha na taarifa zaidi.

Quality
 
Watanzania hawadanganywi tena.Watachukua fweza,tshirt,kanga na kofia sababu vinatokana na kodi yao then kura kwa m2 makini.
 
Sasa jamaa yangu mbona unaleta habari kavu kiasi hiki. Unataka kusema mpaka saa tano hii mdahalo unaendelea??? ..
 
Kazi ipo maana mafisadi wamejipanga. Lakini kwa uwezo wa Mungu Tutashinda hila zote.
 
mdahalo saa tano usiku?
safi sana Tanzania kama kenya vile,hakuna kulala
 
wana igunga tupeni raha watanzania tar 2, oct! piga chini hao nyoka watu, tupeni makamanda wa ukweli kwani wabunge wanaopiga makofi na kuropoka bungeni wametosha tunahitaji watakaoleta hoja nzito bungeni na kuongeza changamoto kwa serikali!
 
Watanzania hawadanganywi tena.Watachukua fweza,tshirt,kanga na kofia sababu vinatokana na kodi yao then kura kwa m2 makini.

Hawana muamana hawa, uwezo wa kujipambanua ungali mdogo na ndo mtaji wanaoutumia ccm, kurubuni watu kwa mtindo huo na mwishowe kupigiwa kura. Arrrrrrrrrrrrgh!
 
Kugawa pesa ni rushwa hiyo sijui kama TAKUKURU wapo huko Igunga, anyway hali jinsi ilivyo ni tata sana maana nahisi kwa wana Igunga sera za kila chama ni kama miluzi mingi humpoteza mbwa! At the end of day watashindwa wammpe nani kulingana na uelewa wa wapiga kura hao.
 
Tarehe 3 mwezi October 2011 watanzania kuvaa nguo nyeus kulaani utendaji wa serikali kama kama unaguswa na mabo yafuatayo basi na wewe vaaa na umwambie na mwenzako.
1.ukosefu wa ajira
2.kupanda kwa gharama za maisha
3.huduma mbaya za afya, elimu na maji.
4.ukosefu wa umeme
5. Ufisadi
6.mikataba mibovu
7. Ubaguzi kwenye mikopo ya elimu ya juu
8.malipo duni ya wafanyakazi wa serikali
9.ufujaji wa mali ya umma kwa watendaji wa serikali kwa safari zisizo na tija.
10. Kuwakumbatia wawekezaji katika kuiba ardhi na rasilimali ya wanyonge.
 
eeeeeee!!!! allah (s.w), wasaidie wana igunga, wasaidie chadema.
 
Tarehe 3 mwezi October 2011 watanzania kuvaa nguo nyeus kulaani utendaji wa serikali kama kama unaguswa na mabo yafuatayo basi na wewe vaaa na umwambie na mwenzako.
1.ukosefu wa ajira
2.kupanda kwa gharama za maisha
3.huduma mbaya za afya, elimu na maji.
4.ukosefu wa umeme
5. Ufisadi
6.mikataba mibovu
7. Ubaguzi kwenye mikopo ya elimu ya juu
8.malipo duni ya wafanyakazi wa serikali
9.ufujaji wa mali ya umma kwa watendaji wa serikali kwa safari zisizo na tija.
10. Kuwakumbatia wawekezaji katika kuiba ardhi na rasilimali ya wanyonge.

Hii nzuri lakini ianzishie thread yake.
Itakuwa operesheni maalum ya kuhamasisha watu kama Dr Kiza Besige wa Uganda na operesheni yake ya Walk to work.
 
hawa ndo wnavyoishi wanafikiri na wengine wanaishi hivo! kama simu yako ina camera ya mwenzio haina picha atazipataje??tumshukuru kwa taarifa nzuri!
 
Back
Top Bottom