CCM washambulia msafara wa CHADEMA, wampiga Mwandishi wa Habari, wakimnyang'anya kamera

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
Wakuu sasa labda haya ni maagizo au ni kitu gani, subjected to debate. Leo kulikuwa na mikutano miwili ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Msalato, Manispaa ya Dodoma, nje kidogo ya mjii.

CHADEMA walikuwa wanazindulia katika eneo la Msalato Bibo, karibu na Shule ya Sekondari Msalato, vipaji maalum. CCM wao walikuwa wanafanyia uzinduzi wao katika eneo la Msalato Gulioni, ni eneo ambalo liko karibu na barabara.

Msafara wa CHADEMA umefika eneo hilo majira ya saa 9. Kama ilivyo ada ya wageni wakifika mahali, viongozi wa kitaifa walikuwa wanakwenda kuweka saini katika kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Kata ya Msalato. Ili ufike mjini iliko ofisi hiyo ni lazima upite eneo la gulio, walipokuwa CCM.

Kufumba na kufumbua, wakati msafara ukipita maeneo hayo, ukiongozwa na watu wa pikipiki takribani 40+, hee mara mawe yakaanzwa kurushwa upande wa msafara wa CHADEMA kutoka kwa wafuasi wa CCM ambao wengi wao walikuwa wamesombwa kwa magari kutoka mjini.

Kama hiyo ya kuponda mawe msafara wa CHADEMA haitoshi, sasa wakaamua kwenda hatua nyingi zaidi mbele, wakamkamata mwandishi wa habari Danson Kaijage. Wakaanza kumshuhushia kipondo kikali. Wakitaka kumyang'anya kamera, wachukue picha alizopiga wakati wanawashambulia CHADEMA.

Kariibu wote waliokuwa wakimshambulia Kaijage anawafahamu. Salama yake ilikuwa ni kuwasili kwa polisi eneo hilo, ambao hata hivyo walichlewa sana kufika eneo la mkutano kufanya kazi yao ya ulinzi. Polisi walishindwa ku-guarantee usalama na kuzuia yaliyotokea leo.

Nitakuja kumalziia kuelezea namna ambavyo CCM walisomba watu kutoka mjini, mgeni rasmi akaonekana akija eneo la mkutano lakini akakutwa watu hawajasombwa vya kutosha hivyo akalazimika kurudi tena mjini mpaka watu wajae, kisha akarudi tena baadae kufanya uzinduzi.

Unajua mgeni rasmi alikuwa nani?
 
Kupia, kuuwa, kuchochea, kudanganya, kunyanya, vitisho na ukandamizaji ni dalili za kushindwa katika hoja.

Ccm ya Kikwete si ile ya Mwalimu, mwinyi au mkapa, walikuwa na aibu kiasi na vijinidhamu hii ya sasa kama vile alivonena

ni ushahidi wa kufilisika kwa mwanasiasa na sasa wantafuta uhalali (legitimacy) kwa lazima, ili chochote

kikitendeka waseme CHADEMA.


 
Na Bwana Mkubwa ndio amesema CCM haifi tutakufa sisi tunaokitabiria kifo, najaribu kufunga domo langu lakini haiwezekani lazima niseme CCM imezeeka, imechoka na yenyewe inajipeleka kaburini, sasa kusomba watu ili mkutano ujae ndio wanamdanganya nani?
 
Sasa itabidi chadema itafute njia ya mkato kujilinda,ikiwemo kuunda jeshi lake,mambo mengine hayavumiliki kabisa,halafu siku hizi wamewa target waandishi zaidi,kutokana na waandishi wengi kujielewa na kutoa habari za kweli kitu ambacho kwa ccm ni uhaini,anyway poleni sana makamanda wetu,vipi wewe hujadhurika?Pamoja tutashinda.
 
Badala ya kuleta habari unaleta mipasho wewe uwa uaminiki toka ulivyotuletea umbeya kuwa mbunge wa CCM kafumaniwa kisha kakatwa mapanga, ulifuata picha mpaka leo ujarudi...Chadema mbona nyie mliushambulia msafara wa Pinda, kwa mawe Mwanza na kuwapiga mawe wafuasi wa CUF Arusha.
 
Kwanza poleni. CCM wakiambiwa wao ndio watatuletea vita wanakanusha. Kila siku wanaumbuka. Mungu hamfichi mnafiki. Kila siku wanahubiri CDM chama cha vurugu na zamani walihubiri CUF.

Haya nayasema kwakuwa najua CCM kwa kufanya fujo na kupiga watu ni kitu cha kawaida. Wakishafanya fujo wanakaunusha kwa nguvu zote huku wakielekeza lawama kwa vyama vya upinzani.

Lakini pamoja na hayo bado habari hii haijathibitishwa hivo Makene tunataka ukweli wa habari hii. Usije ukatuletea vituko kama vya Julius Mtatiro na hadithi za Nape.

Tunakuamini kamanda tupe ukweli.
 
wasiwasi ni hali ya huyo mwandishi (GOD FORbid) ili tuandae kamati mapemaaaaa..anyway tunakoelekea sio kuzuri
 
Back
Top Bottom