Ccm wapotoshaji wakubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wapotoshaji wakubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Papa D, Jan 15, 2011.

 1. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kumekuwa na majivuno hasa kwa Watanzania waliopo ndani ya nchi na CCM kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani. Wamekuwa wakijitangaza kila kona ya dunia kuwa TZ kuna amani ilhali wakificha ama kupotosha hali halisi iliyopo hapa TZ. Binafsi nasema Tanzania hakuna Amani kwa mujibu wa tafsiri ya neno "AMANI" Kama kuna mwana JF anatofautiana na mimi aseme kwa mifano halisi. OTHERWISE; Tukubaliane hatuna amani na nini kifanyike kuleta Amani!
   
 2. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Tanzania Hakuna Amani ila kuna yafuatayo:-

  -Ukondoo wa Watanzania wengi hasa walio vijijini.

  Na ukondoo huo unatokana na kutojua haki zao, kuwa na uelewa mdogo kutokana na CCM kuwanyima elimu.

  Watanzania wengi waishio vijijini kukosa elimu ndo mtaji wa CCM.

  Watanzania wengi hawapati haki zao.

  Bila Haki hakuna Amani.

  Mifano ipo mingi- Wawekezaji kupewa mashamba wakati watanzania wanalia njaa - Mbarali Mbeya

  haki, taratibu kukiukwa ili kutetea masilahi ya Vigogo na ccm kwa ujumla

  uroho wa madaraka, ubinafsi na 10% katika mikataba feki inayoangamiza uchumi wa Tanzania.

  mfumuko wa bei unaotokana na Wahujumu uchumi (mafisadi) hatimae maisha ya watanzania kuzidi kuwa duni....
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kama amani=upotevu wa haki za binadamu, nakubali tz tuna amani tena ya kutosha.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ogopa kusemea amani kwenye umasikini uliokithiri, huo ni uoga tu wa muda!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama unataka kujuwa kuwa Tanzania kuna amani au hakuna, tazama Somalia, Merekani, na kwingineko kwing tu. Hizo nchi mbili nimezitaja kwa sampling tu.
   
 6. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna amani TZ. kila mtu analalamika hali ngumu wakati wafisadi wanakula bata. Rasilimali zinaliwa kwa viongozi, wageni na mafisadi.

  Haki haipo. Polisi wananyanyasa watu
   
 7. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Zomba kama unataka kuona AMANI nenda Botswana; Singapore; Japan; Samoa; Ghana; Denmark na kwingineko kwingi tu! Hizo nimezitaja kwa sampling tu!
   
 8. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tanzania hakuna amani bali kuna unyanyasaji mkubwa sana kwa wananchi wake,na hii yote inatokana nakuwa na serikali dharimu.
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Tanzania hakuna amani bali kuna ukimya
   
 10. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kuupntosha umma Zomba. Usitumie mifano ya nchi zilizo kwenye vurugu kuhalalisha kuwa TZ tuna amani. TZ hakuna amani bali kuna utulivu wa kisiasa unatokana na uoga wa waTZ kudai haki zao, na ujinga wa kutokujua namna ya kudai.
  Inapofikia hatua kama hii kwamba utulivu wa nchi unatokana na woga wa wananchi wake kuhoji mamlaka, ujue ni hatari. Ipo siku watavaa ujasiri after being conscious na hapo ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno kwa tabaka tawala.
   
Loading...