CCM wapigana vibaya Kawe na mkutano kuvunjika

source:itv,habari za saa. Uchaguzi wa viongozi wa ccm wilaya ya kawe jijini dar es salaam umevunjika,huku wajumbe wakiishia kurushiana viti. Mmoja wa wagombea akihojiwa,amesema rushwa iliyo kithiri,ikiwemo ya ngono,imechangia kuvuruga uchaguzi huo! My take: Maumivu ya kichwa huanza taratibu,na kwa sasa ccm inahitaji dawa ambayo itaepusha kufa kwake!
amani na utulivu inapatikana ndani ya ccm pekee.
 
Kwa hali isiyo kuwa ya kawaida wanachama wa CCM katika uchaguzi mdogo wa chama wazicha kavukavu ktk uchaguzi mdogo wa chama. Source itv
 
Jimbo la kawe leo limegeuka kosovo. Uchaguzi kata ya kawe umegeuka uwanja wa vita baada ya wagombea kuanza kurushiana viti. Wengne wamelalamika kukuta majina yamepewa nafasi ambazo hawakuziomba. Viti vimerushwa na mabench yamevunjwa.uchaguzi hakuna. CCM DAYS ARE NUMBERED. Source itv taarifa saa 2
 
kuna kijana alinyanyua flower ves kubwa anataka kuwabonda nayo wenzie, hii ni zaid ya hatari
 
mkuu na mimi nimeiona itv,msela mmoja kamkosa mwenzake na meza,nimeshangaa kuona kuwa bado kuna vijana wapo ccm
 
Aibu..............Things fall apart
Full drama mbele ya kamera, kanifurahisha jamaa aliyerusha meza na alitaka kuvunja na vyungu kabisa kabla wenzake hawajamshika................ Nnauye Jr anahusika hapa nimesikia katajwa
 
Mkutano wa uchaguzi wa vijana CCM kata ya Kawe umevunjika baada ya vijana kupigana vibaya na kurushiana viti huku wakilaani uongozi wa juu kwa kutaka kuua chama.Ilikuwa ni aibu kuu kwa chama tawala ambapo vijana hao wametabiri chama chao kitazikwa muda si mrefu.
Sababu kubwa ya kupigana ni uongozi wa juu wa CCM kukata majina ya walioomba nafasi ya Mwenyekiti na kuleta jina la mtu ambaye hakuomba.Inadaiwa hiyo yote ni kutokana na makundi yanayotafuna chama hicho pamoja na Rushwa ya ngono iliyokithiri ndani ya chama hicho wilaya ya Kinondoni.

Source:Habari ITV

Hapo kwenye red: Tatizo la viti maalum-wanawake CCM naona linakuja kwa vijana wao. TACAIDS washikishwe ili wawape kinga na kuepusha maambukizi.
 
kumbe umalaya unaofanywa na mawaziri na kampeni maneja umeenea...hiki chama sijui tukipe jina gani mafisadi wao, wauwaji wao, rushwa ya ngono wao..
 
Aibu..............Things fall apart
Full drama mbele ya kamera, kanifurahisha jamaa aliyerusha meza na alitaka kuvunja na vyungu kabisa kabla wenzake hawajamshika................ Nnauye Jr anahusika hapa nimesikia katajwa

Hakika ilikuwa ni aibu kuu.Hivi vyama vyenye wanachama wa aina hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi
 
Back
Top Bottom