CCM wanaweza kufanya yake ya ANC

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Kutano limeshika moto huko SA na ANC inagawanyika . Mbeki anabaki mtupu watu wanasema imetosha na Zuma tosha . Je wale wana CCM wa siku ile Dodoma walilkuwa na ubavu wa kusimama hadharani na kusema hapana kwa JK ? Jebu nisaidieni na mwisho nawapa salaam za Christmas .
 
Itachukua miaka mingi sana kwa moto unaowaka ANC kutokea CCM, Si mliyaona ya Dr Gharibu Bilal? ukim challenge mwenyekiti unaonekana mtovu wa nidhamu au muasi.
 
subutuuuuuuuuuuuu aka thubutuuuuuuuu labda sio Tanzania ile ile na Chama kile kile Cha Mafisadi na matapeli!
i wish watu kama kina Kada wangekwepo kutetea li chama lao kama kawa yao
 
Mimi nilitegemea JK awe na Mpinzani kura zimwagwe pale .Nilitegemea Msekwa awe na mpinzani kama tunavyo ona kule SA ANC wanavyo sema mzunguko means Mbeki basi na sasa Zuma tosha . Lakini je matumaini makubwa ya walala hoi wa SA yanaweza kuwa tone la machozi ndani ya bahari kama wadanganyija walivyo fanyiwa na CCM + JK ?Maana naona wana matumaini sana na Zuma namuona anafanana na JK kwa mbaali kwa maneno yake pale Dodoma siku ile .Ila sera zake na misimamo juu ya makampuni ya kigeni na Uchumi zinamfanya atofautiane na JK kwa kiasi kikubwa .
 
Tumejifunza mengi sana mkwenye mkutano mkuu wa ANC. Kwanza democracy at its best. Ingependeza CCM na vyama vingine viige kutoka kwao. Unaona kabisa ushindi huo unareflect matakwa ya watu. Mshindi kapita kwa asilimia 60 ila kwetu hapa utaambiwa ushindi ni 99.9% kweli hii? na aliyepiga kura ya No bongo atasakwa mchana na usiku.
Ni wakati wa kujifunza kuwa demokrasia is a must towards political stability.
 
uJUMBE WETU ccM ULIONGOZWA NA NANI KULE BONDENI KWA MZEE MADIBA?

HUYO ANAPASWA AJE ATUANDIKIA RIPOTI YA YOTE YALIYOJIRI KWA BABU,MWANAKIJIJI TUNAKUSHUKURU SANA KWA JITIHADA ZAKO.

CCM INALO LA KUJIFUNZA PALE TENA LA MAANA KABISA KTK MITIZAMO YA KISERA NA NA NAMNA YA KAMPENI NDANI YA CHAMA.

SHUKRANI
 
CCM hawana demokrasia kiasi hicho. CCM wakiamua kujenga demokrasia kama hiyo basi 2010 JK hatakuwa mgombea tena wa urais.

ANC wameipita CCM kwa mbali mno. Wewe angali tu jinsi Mbeki na Zuma walivyokuwa pamoja kwenye meza ya viongozi na kucheka na kutabasamu pamoja na tofauti zao kubwa.

CCM inabidi muone aibu, pamoja na miaka yote hiyo bado chama lenu liko kama chama cha Kikomunisti cha Korea kaskazini.

Kama viongozi wenu wanapendwa, kwanini wanaogopa mabambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenu?
 
uJUMBE WETU ccM ULIONGOZWA NA NANI KULE BONDENI KWA MZEE MADIBA?

HUYO ANAPASWA AJE ATUANDIKIA RIPOTI YA YOTE YALIYOJIRI KWA BABU,MWANAKIJIJI TUNAKUSHUKURU SANA KWA JITIHADA ZAKO.

CCM INALO LA KUJIFUNZA PALE TENA LA MAANA KABISA KTK MITIZAMO YA KISERA NA NA NAMNA YA KAMPENI NDANI YA CHAMA.

SHUKRANI

Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mzee wa maandiko Pius Msekwa. Pengine ni wakati wa kujifunza kutoka kwa wenzetu. Lakini kwa desturi zetu ndani ya CCM matukio ya ANC yatachukuliwa kama udhaifu na fujo zisizokubalika dhidi ya mwenyekiti; na ni 'fujo' ambazo hazitakubalika kamwe ndani ya CCM.
 
Mzee wa maandika akirudi atakuja na bla bla bla au hata hatakuwa na la kusema . Lakini ANC kufikia pale ni wanachama wake kuamua kitu ambapo ndani ya CCM mwanachama hatakiwi kusema lolote nje ya kumbi lao .
 
Ukijifanya unajua tunakukolimba mara moja, na mambo yanakuwa tambarare. Sasa Lunyungu mchallenge Mwenyekiti uone!
zidumu fikra za mwenyekiti
 
Imagine in November 2007 if Malecela, Mwandosya and Salim would have stood and say they want to be the party leader!

Would their name have gone through Kamati Kuu and Halmashauri Kuu for Mchujo? Or Wajumbe wa Mkutano Mkuu would have been presented with name and vote for whomever they wanted?

Hizi kura za kutewuliwa ni za kijinga! Yanapaswa yafanyike hivi, wagombea ngazi zote wapigiane kura katika ngazi zao halafu yale mafahali ndio wafike mkutano mkuu wapigiwe kura na si viini macho tunavyofanyiwa!
 
japo mfalime akiwa uchi wewe sema sawa maana ccm ni wa mfalme pweza anajikumbia yeye tu kila kitu hajui nini domekrasi au nini na tatrizo sio wao tu hata kwa raia wao watz wakidanganywa kidogo tu wanakubal hata wakiambiwa watajengewa barabara kuelekea mbinguni watasema sawa mzee ni sawa na mfalime pweza na kundi la wajinga watz
 
Ndiyo maana nina hoji Uenyekitim wa JK , Msekwa na Makamba kuwa Katibu Mkuu .Uongozo gani wa kugombania bila ya kuwa na mpinzani ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom