CCM wanawaza kubaki madarakani, hawawazi Uchaguzi Huru na hawataki Katiba Mpya

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,471
2,644
Wasalaam,

Leo ilikuwa maadhimisho ya cku ya demokrasia duniani ambapo kwa hapa tanganyika mgeni rasmi alikua mh Rais wa JMT. Sasa nimesikitika na vijembe alivyokua akirusha wakati akihutubia ikiwemo kauli za kibaguzi dhidi ya wanaume.

Mh Samia hajaongelea hali ya demokrasia hapa tanganyika, hajasema serikali ya wanyonge inaheshimu vp haki za wananchi wake. Yeye mwenyewe mh rais amekua akilalamika juu ya police wake kubambikia wananchi wake kesi mbalimbali ambazo hazina dhamana.

La pili la ajabu akasema 2025 wanawake wamweke Rais mwanamke na sio kumchagua, hapa km una akili timamu utagundua 2025 hakuta kua na uchaguzi bali uchafuzi tena mbaya kuliko ule wa 2015.

Haieleweki ni nini kipaumbele cha Rais wetu na Serikali ya CCM. Hawa watu wamejaa uchu wa madaraka wanawaza kujineema wao na familia zao, hawana uchungu na watanganyika na wanapeana madaraka kana kwamba hii ni ya kifalme.

Ukiangalia maisha yamekuwa magumu wananchi tunaumia viongozi hawajali wajilipa kodi zetu, ccm ni vigeugeu hawatabiri na ndio sabubu hawaki tanganyika iandike katiba yake kwani wanatambua uhali waliofanya utawafunga jela ndo sababu ya kujipa kinga ya kutoshtakiwa mahakamani

Hitimisho ni kama taifa tuungane kuitaka serikali yetu ya wanyonge ya CCM kuwasikiliza na kuheshima maoni ya wanyonge, tanganyika ni ya watanganyika wote na sio kikundi cha watu wachache ndani ya CCM. CCM waheshimu demokrasi kwa vitendo.
 
Hiyo ndio Kanuni ya Maisha. Aliyepo Madarakani anapigania Kubaki hapo...! Na anayegombea Kuwa Madarakani naye Atakuwa anapambana na Hali yake Kuingia Madarakani..!
 
Inabidi na sisi wapinzani tuanze kampeni zetu sasa manake mtemi ameshaanza tena kwa kasi.
 
Back
Top Bottom