CCM wanawacheza mchezo gani haswa? Maana hata iweje hawana nia na Katiba Mpya kabisa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
6,633
14,036
Wakuu jana CCM wametoa press na kusema kuna haja ya kufufua mchakato wa Katiba mpya

Katiba mpya ambayo imekuwa kilio cha muda mrefu cha wapinzani na wataka mabadiliko nchini, inatarajiwa kukuza demokrasia, kuleta uwajibikaji, ugatuaji wa madaraka na ufanisi wa kuendesha serikali

Sasa CCM ambao walikataa katiba 2014 na kusisitiza mara kwa mara katiba haina umuhimu sababu wananchi wanachohitaji ni kula tu, ghafla wamebadilika

Nina uhakika hawana nia wala mpango wowote na katiba mpya, lakini nsiojaelewa ni karata gani wanacheza haswa

CCM ni chama kinachopenda ubwanyenye (Conservatism) na ukiritimba (monopoly) kwenye siasa mambo ambayo Katiba mpya inataka kuleta mapinduzi dhidi yake, nitatoa miofano michache kuthibitisha hayo

1. Katiba ya CCM imempa madaraka makubwa sana mwenyekiti wao ambaye ndio Rais na mtu yoyote akimkosoa ndani ya chama basi ndio mwisho wake kisiasa, mfano Ndugai alipokosoa kuhusu mikopo, kuna Baraka Shamte alimkosoa Mwinyi akafukuzwa chama

2. pia hata Bunge linavyoendeshwa kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wanakosoa mawaziri lakini wabunge hawa wamekuwa wakitishwa kuwa wanampinga Rais,

3. CCM miaka ya hivi karibuni kupitia vyombo vya habari, wasanii, viongozi wa dini wamekuwa wakitengeneza image ya Umungu kwa Rais, mtu ambaye hana makosa, jasiri, anajua yote, mwenye nia njema kuliko wote, mwenye akili kuliko wote na kwa image hii wanaom kosoa wote wanaonekana watukutu ama waliokosa nidhamu, sasa hawa watu ndio watake katiba itakayoleta demokrasia na kupunguza nguvu ya Rais? UNLIKELY

jE MKAKATI WAO NI UPI HASWA?
 

mboyapatrick

Member
May 26, 2022
40
58
Hapa swala unyumbu kama kweli wamedhamiria CCM watoe time frame vinginevyo ni usanii wao tu maana Kuna baadhi ya wananchi wanasema hawatakuwa tayari kutoa ushirikiano wakati wa sensa
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
13,959
52,504
Hawana lolote, kama wanashindwa kufuata sheria zilizopo kwenye hii Katiba chakavu, wanaenda kutengeneza "Katiba Mpya" ya kazi gani ikiwa bado hawajabadilisha hizi tabia zao za kutofuata sheria?

Ndio maana siamini kama kweli CCM wana nia ya dhati na Katiba Mpya, wanatuchezea akili tu lakini najua mbele ya safari wameshajua watakachofanya ili kuharibu huo mchakato, muhimu wajue tu, issue ya Ngorongoro haiwezi kusahaulika.
 

AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
3,440
3,432
Mkakati wa siku zote ni kuutia mifukoni upinzani at any cost. Hizi tricks mara Maridhiano, Mara katiba mpya ni porojo tupu. CCM hii ya majizi haiwezi wapa Watanzania katiba ya warioba yenye msingi wa serikali tatu kabisa hilo haiwezi tokea. Ila wanaweza wapa katiba ya zamani ila modified.
 

Bepari2020

JF-Expert Member
Nov 7, 2020
2,073
2,420
Katiba mpya inayogusa muungano na suala la uraia pacha msahau. Kamwe CCM hawatakubali.
 

Bloodstone

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
599
608
Kura za maoni kupigia kura katiba pendekezwa... ndipo mchakato ulipoishia ndio jamaa watavopiga chenga ya mwili
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom