MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Katika mambo ambayo CCM wanapaswa kulaumiwa na kukemewa kabisa ni wao kua chanzo cha mgogoro wa upatikanaji wa Mameya wa Manispaa za Ilala na Kinondoni pamoja na jiji kwa ujumla.
Hi kweli pamoja na Waziri wa Tamisemi kukemea michezo hiyo michafu juzi lakini hili alikua analifahamu tokea mwanzo! Kwani hata Simbachawene hafahamu tokea mwanzo kuwa pamoja na yeye kama waziri alikua anahujumiwa?
Ni zaidi ya mwezi sasa karibia halmashauri zote na Manispaa pamoja na majiji nchini wameshamaliza chaguzi zao, Viongozi wameshapatikana na sasa vikao vya mabaraza ya madiwani vinaendelea kujadili mambo ya msingi lakini kwa Ilala,Kinondoni na jiji zima kwa ujumla kwakua upinzani wana madiwani wengi ndio iwe nongwa?
Kuna tatizo gani mameya wa Manispaa zote na jiji wakitoka upinzani? Kwani mameya hao watakua na biashara gani zaidi ya waliotangulia? Kule Temeke kwenye madiwani wengi wa CCM uchaguzi ulishapita muda mrefu na hapakua na mbunge hata moja wa kutoka Zanzibar aliyepelekwa kule na viongozi walichaguliwa na sasa vikao vinaendelea.
Kasi anayoitaka kwenda nayo rais Magufuli itaanzia wapi upande wa Kinondoni na Ilala kama vikao vya kujadili hoja zake havifanyiki? Hivi hapa si ndio kumhujumu Rais? Ndani ya Manispaa hizo kuna mapato ya ndani ya kila mwezi kwa ajili ya kuendeshea miradi yao na sasa kama hakuna vikao vya kujadili mipango na matumizi ya mapato hayo itakuaje?wakurugenzi watakaa na kina nani kupitisha bajeti za Manispaa hizo?
Kwanini sisi tusiite kua hii ni mipango madhubuti kumhujumu Rais baadae aonekane ameshindwa kazi?
Kama upande mmoja una madiwani wengi na wamekubaliana watoe Mgombea mmoja wa umeya kwa kauli moja inamaana Meya na naibu watatoka upande huo! Figisu figisu za nini? Kona kona za nini?
Wewe sio diwani wala sio Mgombea unapeleka Pingamizi mahakamani la nini? Kwa faida ya nani? Kutokuwepo kwa vikao vya mabaraza ya madiwani kujadili maendeleo huku wewe unakimbilia mahakamani kuweka Pingamizi ili iweje? Wewe unafurahia Wananchi wakose maendeleo sio?
Bila kula maneno ni kwamba CCM Ilala na Kinondoni wanamhujumu Rais Magufuli maana hamna vikao vya mabaraza ya madiwani, hakuna kasi ya aina yeyote ya maendeleo.