CCM wanauwana .... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wanauwana ....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hasara, Nov 3, 2007.

 1. H

  Hasara Senior Member

  #1
  Nov 3, 2007
  Joined: Dec 29, 2006
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CCM wanauwana ....
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ahamua kumaliza ruswa katika nafasi ya umakamu wa mwenyekiti wa CCM kwa kumteuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, baada ya kugundua waliyo mzunguka walikuwa na ajenda ya siri, walifanya kampeni kubwa yeye akiwa safarini,walitumia resource nyingi za taifa kujinadi,

  Baada ya muungwana kujua hilo haya ndiyo mawazo na uwamuzi wake
  na wengine walituma wabunge sehemu mbali mbali kuwafanyia kampeni wengine hadi kupatwa na mauti,

  waliyo jinadi sana na kumuogopesha muungwana ni waziri wake mkuu,

  Baada ya uchaguzi huu ndiyo kila kiongozi atajua nini cha kufanya na JK ni nani wake basi hapo ndipo tutaona vilio vya wakubwa...subirini

  wengi wametumia mamilioni ya pesa alafu unakuja kuweka mgombea pekee?

  maana ya mmgombea pekee ni nini?
  naomba kutoa hoja
   
 2. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135

  Wana CCM njooni mumjibu Hasara hapa.
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Dua,

  Usimsikilize Hasara. Ni kweli aliyosema, ila sio kweli kuwa EL alitaka u makamu. Hell NO, ni uongo , kuna waliotaka hiyo nafasi, nitaelezea mengi nikirudi kutoka Dodoma na nikiwa nimefanikiwa hazima yangu ya kilichonileta Dodoma!

  Wale wa Dar tunaofahamiana mnaweza kuandaa party tu..., haina haja ya kungoja mpaka kesho. mambo juu ya msitari!
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Dua,

  Kwa ufupi Mtandao umepigwa chini vibaya sana, Yaani Muungwana ameprove kuwa Kiongozi wa kweli. Waliitaka nafasi ya umakamu WAMEIKOSA! Check NEC watakavyoanguka.

  Mungu mbariki Muungwana Mungu ibariki Tanzania.

  Jamani narudi ndani. I love JF
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Nov 3, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FD,
  Hao mtandao ni akina nani ikiwa JK yupo nje. Mimi nilidhani Mtandao ni wafuasi wa JK mwenyewe kumbe inavyoonyesha kuna mgawanyiko kati ya JK na EL...
  Na kama ndivyo basi kwa nini asianze na kumsimamisha EL moja kwa moja kwani waziuri mkuu sio nafasi inayochaguliwa na wananchi. Ni yeye mwenyewe, kuondoa mzizi wa fitna ni kumwondoa EL ktk nafasi ya Waziri mkuu lakini kuacha mzizi huo, mvua itanyesha na mti utastawi kwa uwezo wake Mungu.
   
 6. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #6
  Nov 3, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ushupavu wake utaonekana kwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi na nchi na wala sio hayo maigizo ya hapo Kizota. Mwambie akae chini afikiri namna ya kutokomeza lindi la umaskini, atumie urais wake kutomeza ufisadi, achape kazi, atulie, aache kuzurura na kuwagawaiwa wazungu vipanda vya ardhi yetu. Tunamtakia kila la heri akifanya hivi.
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  FD

  Hicho ni kipi hasa kilicho kupeleka Dodoma, maana umekuwa ukirudia kila mara "kilichonileta" hapo Dodoma au ndio U- NEC mkuu.

  Haya basi mimi nakuombea kila la kheri ufanikishe azma yako hiyo..
   
 8. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  FD pamoja na kuwa ww ni mwanachama wa sisiemu, je na ww ni mgombea katika uchaguzi huu? Naona unawaambia jamaa zako waanda aherehe. Tudokeze kidogo basi.
   
 9. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  haya maneno yametoka wapi ?
   
 10. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Masatu, kama umemsoma vizuri apo juu, FD anawataka wale wa dar wanaomfahamu waandae party manakeinaelekea atapata kile 'alichofuata' apo dodoma

  Sisi tusiokufahamu tutashirikije FD au ndo unatutosa mkuu?
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mimi nili joke, inawezekana kuna ukweli. haya Fd ninakutakia kila la heri, huenda ukawa chachu ya mabadiliko kwenye chama chenu.
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nakulilia TZ hata mimi nina wasiwasi FD akipata kilichompeleka Dodoma huenda hata kwenye "cocktail" hatuto pata mwaliko!

  Taarifa zilizojiri ni kuwa Mswahili nae ameonekana akivinjari maeneo ya Kizota huenda nae akaramba dume....

  Chelea chelea utakuta mwana si wako..
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2007
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nilisema Watanzania tumepata Raisi ambae hajawahi kupatikana,na pia nilisema kuhusiana na mitandao au vigogo waliokuwa wanachumia matumbo yao tu,hawa walikuwa ni wengi na wameshaota mizizi na kuota kwa sura nyingi kila kona ya Tanzania ,kupambana nao ni kazi ngumu na ni hatari ila JK ameliona na anakwenda nalo taratibu sana bila ya kumwaga unga.Tulieni anawajua ni nani wapenda maendeleo kwa nchi na wananchi na ni nani ni walaji au makupe.
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sisi tulio wahi kuendesha malori mabovu aina ya BEDFORD, kama yale ya kusombea mkaa,tunajua namna ya kuya treat pale gear namba 1 ikishindwa kuingia na wakati huohuo lori liko katikati ya kilima.

  Gear # 1 ikigoma kuingia hapo maisha yako na ya abiria wengine ndani ya Lori yamo mikononi mwa utingo.
  Utingo anakaa standby muda wote akisikiliza change down ya Gia.

  Unapangua gia namba 4 na kurushia namba 3 unaweka moto chini lori linajibu mapigo.
  Unapangua gia namba 3 na kubandika gia namba 2 unaweka moto chini mpaka kwenye bati lori linalalamika kishenzi lakini haliendi kokote.
  Unapiga moyo konde unapangua gia namba 2 unaitafuta 1 na moja inakutafuta wewe Toba!.

  Unaita kwa sauti kuu ya mayowe ya shetani kubanwa mkia na mlango.

  Haya! haya! mwanangu kula Rec!

  Kama paka, mwizi utingo huyoo! anaruka na kigogo chake begani, na wakati huo huo gia Box inalalamika Giiiiiiiiieeeei!

  Utingo kwa Timing ya hali ya juu kabisa anasubiri lori lisimame kabla halijaanza kurudi kinyume nyume utingo anabandika kigogo, lori hata kama limebeba dunia yote linasimama pale pale, na lori linasimama wote mnaangau kicheko.

  Tumewahi kujaribu Semi trailer kubwa za zaidi ya tani 100, kwa perfect timing zinasisima bila wasi. Siyo kwa vigogo viwili, kimoja tu.

  MH Kikwete ametumia principle ya lori bovu mlimani kumlamba kete Edward Lowassa.

  Good Move.
   
 15. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  tena hata usinikumbushe malori babu, maana hata mie nimepush sana mzee, maeneo ya mpwapwa, mafinga, shinyanga, dodom, singida kote huko miaka ya 80 nikitafuta afueni ya maisha !
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280

  Mungu ambariki Muungwana kwa kipi hasa alichokifanya kwa Watanzania!? kusaini mikataba mibovu, kukumbatia mafisadi, wala rushwa na viongozi wanaopenda kujilimbikizia mali, haya kweli yanastahili kuombewa mungu ambariki!!!? :confused:
   
Loading...