CCM wanatumia watoto wadogo kwenye siasa

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078

makada wa CCM wakiwa wamembeba juu mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa wa Iringa
kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas kushoto akimkaribisha mwenyekiti wa chipukizi mkoa Enock Luhala mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa Chipukizi mkoa
Kamanda wa UV CCM ambae alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi wa Chipukizi mkoa wa Iringa Salim Asas akiwa na viongozi wa UVCCM mkoa Tumain Msowoya mwenyekiti wa umoja huo kushoto na mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa Enock Luhala kulia
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas kushoto na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya wakiwa wamewapakata wajumbe wa mkutano mkuu wa Chipukizi mkoa wa Iringa mara baada ya uchaguzi.Chanzo Mzee wa matukio

NB:
Kitendo kama hiki kingefanywa na CHADEMA, TLP, CUF na vyama vingine vya siasa tungesikia kelele kibao za magamba kuwa wameanza kutumia watoto kwenye siasa mnakumbuka yale ya vyuo vikuu juzi kati hapa magamba walivyo kuwa wakilia siasa zimeanza mashuleni leo hii wao wanawatumia watoto kama chipukizi.
 
Hivi mbona Kenya huwezi kuta hawa Wahindi wakifanya siasa? na hawataki kabisa kujihusisha na siasa, Ila huku Bongo tunawaona watu muhimu sana
 
Chadema.jpg
Hawa nao ni Chipukizi wa chadema?
 
Hivi mbona Kenya huwezi kuta hawa Wahindi wakifanya siasa? na hawataki kabisa kujihusisha na siasa, Ila huku Bongo tunawaona watu muhimu sana
bal.jpg kk.jpg jj.jpg nn.jpg
Huyu Mwanasiasa kutoka Kenya "Mhindi"umepata kumsikia,au kenya ipi unizungumzia?
Halafu nahisi wewe ni mbumbumbu wa siasa!
 
Hivi mbona Kenya huwezi kuta hawa Wahindi wakifanya siasa? na hawataki kabisa kujihusisha na siasa, Ila huku Bongo tunawaona watu muhimu sana

Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo unaweza kufanya chochote. Tanzania ni nchi pekee duniani ambapo wenye hela wapo juu ya sheria
 
Hivi mbona Kenya huwezi kuta hawa Wahindi wakifanya siasa? na hawataki kabisa kujihusisha na siasa, Ila huku Bongo tunawaona watu muhimu sana

Ubaguzi ni dhambi mbaya sana, nyie mkipewa hela na muhindi sawa ila wenzenu hamtaki wapewe.
 
Hii ni ishara mbaya kitendo cha wanasiasa kujitafutia umaarufu kupitia watoto wadogo. Kuna uwezekano mkubwa tukatengeneza taifa la kishabiki.
 
Back
Top Bottom