CCM Wanatumia Madawa ya Kuongeza Ufisadi - Steroids

kinetiq01

Member
Aug 25, 2006
49
0
Ukifuatilia kwa makini hii mikasa ya ufisadi na rushwa, hakika unaweza kudhani CCM ndiyo Mungu wa Tanzania.Kumbe katika hali halisi, kila mtu ana Mungu wake au imani yake.

Nasema hivyo kwasababu vitendo vya rushwa na matumizi ya ovyo ya mali ya umma vimekithiri kiasi ambacho hakielezeki.It's like the guys are on steroids.Madawa ya kuongeza nguvu za ufisadi.

Hivi mtu kama Prime Minister, ambaye hata akistaafu maslahi yake yanagharamiwa kwa fedha ya wananchi, ana haja gani ya kujilimbikizia mali?Greed ya hali ya juu, lakini utakuta hodari sana wa kwenda kanisani, kwa imani kuwa anapunguza makali ya dhambi zake.

Tatizo la msingi ni moja.CCM itakapoacha kulea uchafu kama chama, ndipo Tanzania itapata matumaini ya kusonga mbele.Na serikali imekuwa siyo ya wananchi tena, ni serikali ya genge la walafi wa CCM.Rais Kikwete kwa upande wake ana udhaifu wa aina tatu:-
  • Mnafiki - Anawachekea watanzania lakini anawaachia rafiki zake wananyonya wananchi masikini.Historia itakuja kuonyesha kwamba, dhambi nyingi zilifanywa wakati wa Mkapa, lakini nyingi zaidi zimefichuka wakati wa Kikwete kwasababu ni kiongozi dhaifu.
  • Mwoga - Anaogopa kuchukua hatua zinazostahili kwa kuhofia atawaudhi wafadhili wake ambao sasa wanajinafasi kufidia gharama zao.Haiwezekani rais ukawa na urafiki na kila mtu anayeharibu kisha usichukue hatua kali na kuziba mianya ya wizi, labda kama na wewe unanufaika.
  • Hajui la kufanya - Pamoja na yote anayojaribu kufanya ukweli ni kuwa ameishiwa ideas za kuiongoza Tanzania, amezidiwa na ukubwa wa kazi, hakutegemea kazi ya urais ni ngumu kiasi anachoshudia.
 
Mawazo yako ni mazuri ila yanahitaji uchambuzi wa kina. Sikatai kuwa PM hayumo kwenye haya mascandal yanayokuja kila siku, ni wazi RICHMONDULI na mikataba mingi tu yumo,si ajabu ukaskia kampuni yake inagombania tenda ya kuchapisha vitambulisho vya uraia, si ajabu hii. ni mengi ukiyasikia unaweza kubebea bunduki ukawafutilia mbali hawa mafisadi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom