CCM wanatakiwa kutafakari kwa haya wanayowatendea watanzania!

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Wana JF,

Kwa heshima na taadhima nataka nizungumze machache kwenye uzi huu kuhusu chama Tawala CCM.
Kwamba kwa matukio yanayojitokeza hapa nchini mpaka sasa yanaelekea kutishia AMANI,UPENDO na MSHIKAMANO ambao Watanzania wamekuwa nao tangu nchi hii ijitawala zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Lakini nachelea kusema kwamba hii AMANI,UPENDO na MSHIKAMANO havipo tena na sioni haya kusema kwamba vitu hivi vimeondoka na mwenyewe aliyevianzisha, BABA WA TAIFA, MWL. J.K. NYERERE(RIP)! Kwa sasa Serikali ya CCM walipofikia hakuna tofauti na Serikali yoyote ya KIDIKTETA duniani. Kwa wale wenye kumbukumbu sahihi za tawala ovu zilizopita ambazo Serikali ya TANZANIA chini ya uongozi thabiti wa Baba wa Taifa ilizipiga vita. Kwa uchache tu nitaje Serikali DHALIMU ya Makaburu wa Afrika ya Kusini waliokuwa wakiwatendea Unyama Wazalendo wa nchi hii kwa kutumia mbinu hizihizi ambazo kwa sasa zinatumiwa na CCM! Kulikuwa na Serikali ya Uganda chini ya Dikteta Idd Amini Dada ambayo iling'olewa madarakani kwa msaada wa Serikali ya Tanzania chini ya Baba wa Taifa. Kulikuwa na Serikali za Wakoloni wa Kireno kule Msumbiji,Angola na Namibia zikiwakandamiza Wazalendo wa nchi hizo kwa staili hihii ambayo CCM wanaitumia sasa kuwaonea WAZALEND WA KITANZANIA.

Serikali ya CCM wanafanya hivo kwa vile tu Wazalendo hawa wako vyama vya UPINZANI kuipinga Serikali ya CCM kwa kutumia Katiba na Sheria za Nchi hii! CCM bado wanajidanganya kwamba Watanzania ni wajinga, wapole na wasahaulifu na hata wakipigwa mabomu wakauawa leo kesho watakuwa wamesahau na kunedelea kuipenda CCM ili iendelee kutawala milele. Huku ni kujidanganya!

CCM wanatakiwa kujua na hakika wanajua kuwa chama kikuu cha Upinzani kwa sasa ni CHADEMA na kinakubalika na Watanzania zaidi ya 2.2 miliioni waliokipigia kura chama cha CHADEMA dhidi ya Watanzania 5.3 milioni. Sasa chama kilichopata kura zaidi ya 2.2 milioni siyo ya kubeza na kutaka KUKISAMBARATISHA KWA KUKIUNDIA MIZENGWE NA KESI ZA KUBAMBIKIWA KWA VIONGOZI NA WAFUASI WAKE ATI KICHUKIWE NA WATANZANIA. Hakika huu ni uongo wa mchana kweupe!!

CCM wanatakiwa kujua pia kuwa nchi hii si ya CCM na Viongozi wake tu. TANZANIA ni ya Watanzania wote bila kujali itikadi zao za KIDINI au KISIASA,JINSIA au RANGI zao. Lakini kwa sasa CCM wanajitahidi kuwaaminisha Watanzania kwamba Tanzania ni ya Serikali ya CCM na mtu mwingine yeyote anayetaka kuitawala Tanzania basi yeye ni ADUI nambari wani wa CCM na hatakiwi hata kuishi!!

Tukio la Bomu pale Soweto kwenye Mkutano wa kampeni za kuhitimisha kampeni za Udiwani tarehe 15/06/2013 limeacha MAKOVU MAKUBWA sana kwenye mioyo ya Watanzania na hawatakaa wasahau kwa vizazi na vizazi vitakavokuja! Kwamba mkutano wa chama cha Upinzani uliweza kushambuliwa kwa BOMU LA KUTUPWA na mkono na kuuwa watu 4 mpaka sasa na Serikali ya CCM ikaanza kushangilia na kutoa matamko ya kebehi na dharau kana kwamba waliokufa pale hawakuwa Watanzania baali WAFUASI WA CHADEMA!!!

Niwakumbushe CCM kuwa hii ndiyo ile DHAMBI KUU aliyokuwa akiirudiarudia Baba wa Taifa na bado inarudiwarudiwa kwenye vipindi vya radio na TV za TAIFA na BINAFSI kwamba ukianza DHAMBI YA UBAGUZI KAMWE HUWEZI KUIACHA maana ni SAWA NA KULA NYAMA YA MTU kwamba ukishaonja huwezi kuacha hiyo dhambi na ITAKUTAFUNA TU! CCM tayari wamedhihirisha KUANZISHA na KUASISI DHAMBI YA UBAGUZI wa KISIASA na KIDINI ili kuweza kufanikisha MALENGO yao ili kufikia mafanikio ya Uchaguzi Mkuu 2015! Tumeona Arusha jinsi Serikali ilivowabagua CHADEMA tangu mwanzo wa tukio la Bomu mpaka na mpaka sasa jambo hilo liko wazi kabisa si kwa Watanzania tu baali hata kwa Mataifa mengine duniani.

Hii si picha nzuri hata kidogo na hakiKa CCM wanajua wanachokifanya. Lakini pia wajue kuwa hakuna SIRI hapa duniani na kwamba chochote CCM wanachokipanga dhidi ya CHADEMA taarifa lazima zitawafikia vongozi CDM tu. Kama sisi ni wamoja na kuna ndugu,jamaa.marafiki wanafanya kazi za POLISI, USALAMA WA TAIFA,MAHAKAMA na MSAJILI WA VYAMA na wana ndugu zao wako UPINZANI lazima taarifa zivuje tu kwa vile hakuna anaweza kuona ndugu yake anateswa au kuuawa kwa vile tu yuko upinzani. Hata kama ni mimi lazima nitatoa taarifa kwa ndugu zangu ili wasije wakauawa bure!

Mwisho CCM wajitafakari upya waone walipokosea na wakomeshe huu ujinga,uhuni, na uonevu wanaotufanyia Watanzania ati tu kwasababu wako upinzani! Upinzani si uadui wala Uharamia, wala Ugaidi. Ni wakti saa wa kuwaketisha chini makada wao wababaishaji amabo ndo wamekuwa vinara wa kuchochea na kuvuruga Amani huku wakijidai kufukia nyanyo zao kwa kivuli cha CHADEMA. Ni wakti mwafaka sasa kuwaondoa Mwigulu ,Nnepi na Wassira. Watatu hawa wamewahi kunukiliwa na media si mara 1 wala 2 kwamba CHADEMA KITAKUFA KATIKA MUDA WA MWAKA AU MIWILI CHADEMA KITAKUWA KMEKUFA. Juhudi na harakati zinazofabywa na CCM SASA NDIYO ZINATHIBITISHA MANENO YA UTATU WAO. Kila kitu kiko wazi kabisa na haihitaji mtu kwenda shule ili ujue nini CCM wamepanga!
 
Mkuu ccm wameziba masikio. Hata utu hakuna tena mioyoni mwao!

Tatizo kubwa ni Kikwete. Ogopa Rais anayetengenezewa risala. Hata salamu za kawaida lazima akaririshwe! Weka Jk na ccm mbali na demokrasia
 
Mkuu umejitahidi kuelezea vizuri sana,

Ila sina hakika kama masikio ya wenzetu hawa hayajaziba kwa ufisadi uliokithiri,

sina hakika kama mioyo yao haijaota kutu kwa matendo Yao ya kinyama,

sina hakika kama wanaelewa kwamba nchi hii ni ya watanzania wote kwa kiasi kikubwa walichofikia cha kulewa madaraka,

Na sina hakika Kama wanatambua kwamba wananchi wengine nao wana haki ya kuishi kwa jinsi ambavyo roho zao zimejaa ibada za kishetani

Ila tu watambue hawataweza kuua watanzania wote million 45 kabla hata wao Mungu kuwachukua kwa matendo Yao maovu
 
Your a great thinker and u deserve it

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom