CCM WANATAKA TUMSUSIE POMBE MLEVI KWA FAIDA YA NANI?(Makala Dira Jumatatu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM WANATAKA TUMSUSIE POMBE MLEVI KWA FAIDA YA NANI?(Makala Dira Jumatatu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, May 10, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nape-mjumbe.jpg
  Na Nova Kambota,

  Pengine hakuna ubishi kuwa katika historia ya CCM kuanzia kuasisiwa
  kwake haijapata kuyumba kama sasa tena waziwazi kiasi kwamba wadadisi
  washaanza kuhoji kuwa CCM inaenda orijojo au inakufa kabisa? na
  wengine washaanza kutabiri kuwa CCM ipo mbioni kugeuka chama cha
  upinzani.
  Nashawishika kuamini kuwa CCM inazidi kubomoka kwa kasi ya ajabu ,
  imani yangu hii inapewa nguvu na udhaifu mkubwa unaoendelea kuonyeshwa
  na viongozi wapya wa CCM ikiwa ni muda mfupi tu tangu wapewe uongozi
  huo.
  Mara baada ya kile kilichoitwa "operation vua gamba" kuzinduliwa
  rasmi kule Dodoma kama kawaida ya CCM walianza kujitapa kuwa huo ni
  uamuzi mgumu lakini wenye kuhoji wakauliza mgumu kivipi?, kwa mbwembwe
  kubwa tena bila kuombwa kina Mukama, Nappe na Chiligati wakaanza
  kueneza tambo zao kuwa mafisadi watashughulikiwa kikwelikweli, wenye
  kuhoji wakauliza tena CCM imeanza lini kuchukia ufisadi?
  Kwa sauti ya kikada kina Nappe wakazidi kutamba kuwa CCM imeamua
  kujivua gamba huku vyanzo mbalimbali vikidai kuwa miongoni mwa watu
  waliotajwa kuwa magamba ni pamoja na Rostam Aziz, Edward Lowassa na
  Andrew Chenge hivyo ni lazima wajiondoe wenyewe kwenye nafasi za
  uongozi ama sivyo ndani ya siku tisini watatemwa! ilitia hamasa sana.
  Lakini kabla hata ya siku thelathini kuisha tayari viongozi hao
  wapya wa CCM wameanza kukana maneno yao,hivi karibuni Nappe Nauye
  sambamba na Wilson Mukama walikana waziwazi kupeana siku tisini badala
  yake wakadai siku miaishirini kabla hili halijaisha wakaibuka na hoja
  kuwa mpaka kikao kifuatacho kisha wakabuni falsafa ya aina yake kuwa
  mtu akioga basi ni mwili mzima sio viungo vichache tu,hwaeleweki!
  Sasa katika sintofahamu hii inayonogeshwa utamu na hao watuhumiwa
  wa ufisadi ambao tayari kuna taarifa kuwa wanaweza kumwaga mtama
  kwenye kuku wengi kisha mambo yakazidi kuchacha. Hali hii ya
  watuhumiwa wa ufisadi kutishia uhai wa chama imefanya kasi ya kina
  Nappe kupungua tena ni wazi kuwa badala ya chama kuwayumbisha hao
  watuhumiwa wa ufisadi sasa ni dhahiri kuwa CCM ndiyo inayumba na
  kuyumbishwa sana na maamuzi legelege.
  Udhaifu huu wa kimaamuzi umefanya viongozi wapya wa CCM kukimbia
  baadhi ya maswali au kuwakimbia waandishi wa habari, kila mwenye macho
  aliona jinsi Nappe Nauye au Mukama walivyojitokeza wiki iliyopita
  kufafanua kuwa wanahabari wanapotosha kuandika kuwa watuhumiwa wa
  ufisadi wamepewa siku 90, naam! hakuna ubishi kuwa Nappe na Mukama
  wanazungumza kwa woga tena wanatetemeka hata ukiangalia nyuso zao sasa
  utaona zile tambo zao zimekwisha kabisa, walipima kina cha maji sasa
  wameona sio saizi yao!
  Moja ya maswali yanayowachachafya viongozi hawa wa ccm ni lini
  barua za kuwatimua mafisadi zitaandikwa? na nani atazisaini? kwa maana
  tayari kuna taarifa kuwa kila mtu anaogopa kuzisaini mara zipo kwa
  Nape, mara zipo mezani kwa Msekwa, baadaye zipo kwa Mukama na sasa
  zinadaiwa zipo kwa mwenyekiti wa chama lakini swali ni lilelile nani
  atathubutu kuzisaini?
  Wenye kuona mbali washaanza kuhoji kwanini CCM inahofu sana
  kutekeleza maazimio yake? inamwogopa nani? kwani kwanini wananchi
  wanaichukia CCM? jibu ni rahisi tu kwasababu inalea mafisadi na
  ufisadi, suluhisho la tatizo ni nini? jibu pia ni rahisi alihitaji
  tuwe na PHD ni kuwa CCM iwatimue mafisadi wote pasipo huruma wala
  ngojangoja, sasa hizi porojo za mara waandishi wanapotosha, ooh sio
  siku 90 bali 120, mara jamani mbona mnatuchimba sana? tuacheni tujenge
  chama chetu zinatoka wapi?
  Mbona wakati ule kina Nappe walijiapiza kuwashughulikia mafisadi
  bila huruma? sasa mbona huruma imekuwa kubwa sana tena ya siku 120?
  kwanini? na huu mchezo wa kukimbia maswali na hoja za msingi umeanza
  lini? nani kawaambia kuwa watanzania wana haja na propaganda zao?
  wanataka tuwaachie chama chao, inachekesha sana! kwani mtanzania gani
  mjinga ambaye atamsusia mlevi pombe akidhani amemkomoa? bilashaka
  hakuna!
  CCM hatuwezi kuiacha hata kidogo kwasababu ni chama tawala na
  udhaifu wake unayumbisha nchi yetu pia kamwe kwa ulevi wao wasitegemee
  tutawaachia pombe, wakinywa je? lazima tuendelee kuhoji udhaifu huu wa
  CCM au ndio wanataka tuanze kuamini kuwa CCM imefichwa kwenye kwapa
  za mafisadi? lakini kusuasua huku labda CCM wameanza kubaini kuwa
  dhana ya ufisadi ndani ya CCM sio jambo la watu watatu bali ni mfumo
  rasmi ambao labda umecheklewa tu kutangazwa, Tungoje tuone!
  Nova Kambota ni mwandishi kijana wa Makala , ni mchambuzi na mtafiti
  wa maswala ya kisiasa pia ni mwanaharakati wa vijana anapatikana kwa
  anwani ya barua pepe; novakambota@gmail.com au tembelea blog yake ;
  www.novatzdream.blogspot.com
  Au mpigie kwa namba 0717-709618 au 0766-730256.
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Poa sana kwa taarifa hii. Biblia imenena wazi Pepo awezi kumtoa pepo mwenzie.... Nami amin amin nawaambia Fisadi awezi kumfukuza fisadi mwenzie.
   
 3. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huo usanii wa ccm siye tuliushitukia mapema na kukataa single yao ya kusaula magamba.
   
 4. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Wacha chama cha MAGAMBA kiende tu. Hakuna marefu yasiyo na mwisho.
   
 5. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hongera mkuu naomba makala hii uipeleke kwenye magazeti yanayoeleweka siyo uhuru.
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hahahaha... propaganda hizo ni "NGUVU YA SODA" hakuna jipya hapo kila mtu anataka kuonekana yeye ni bora kuanzia Mukama na wenzake wote hakuna atakaye nyooshea mafisadi kidole.

  Waendelee na nguvu ya soda yao waone moto wa NGUVU YA UMA inavyofanya kazi!
  Mapambano ndio kwanza yameanza..... mziki mnene unakuja lazima Magamba yangooke tu!!!!!!!!!!!!!:peace:
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kusubiri siku 90 ziishe ni zaidi ya kungoja tamthilia ya isidingo the need iishe.Huu ni mchezo wa kuigiza tu hamna chochote.
   
 8. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  wenye akili zetu tulijua right from the day 1 kwamba ulikuwa ni mchezo wa kuigiza. Rebranding si strategy katika vyama vya kisiasa, sasa sijui nani kawaloga CCM wakai-apply!!! Kwa ufupi ni kwamba bila ufisadi (wa fedha za umma na kura) hakuna CCM so nani atakubali kujinyima ulaji CCM??? watawapata hao hao mabwege, wavivu wa ku-reason, rahisi kununulika (fulana, t-shirt, kofia, kilemba, kitenge na 5,000/-) sio mtu kama mimi!!!
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hapo umenena Mkuu. Hatuwezi kuiacha kuisema ccm kwa vile ndiyo ni chama tawala na kimeshikilia maisha ya Watanzania mikononi. Je! Utampa dereva aliyelewa chakari bus lenye abiria? La hasha. Kutokemea ulevi wake ni janga kwa abiria wote.
   
Loading...