CCM wanaswa wakinunua shahada • Wakutwa nazo 180 kibindoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wanaswa wakinunua shahada • Wakutwa nazo 180 kibindoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijui nini, Oct 23, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  WAKATI juhudi za kuliokoa Jimbo la Bukombe ambalo liko katika hatihati za kunyakuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zikipamba moto, viongozi wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa wakinunua shahada kutoka kwa wapiga kura.
  Habari kutoka Bukombe ambazo zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Selemani Nyakipande, zinasema viongozi hao ni Juma Mhoja na Shadrack Paul, ambao ni makatibu wa Tawi la Ushirombo na Msonga.
  Alisema viongozi hao walikamatwa katika Kijiji cha Msonga, Kata ya Runzewe, wakiwa tayari wamenunua shahada 185 za kupigia kura kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wanarubuniwa na baadhi ya makada wa CCM ambao wako katika mkakati wa kuliokoa jimbo hilo.
  Viongozi hao walikuwa wakinunua shahada hizo kwa bei kati ya sh 2,000 na 5,000 huku lengo kuu likionekana kuwalenga zaidi wafuasi wa CHADEMA ili kudhoofisha nguvu iliyopo.
  Kamanda Nyakipande alisema polisi inaendelea kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai kuwa tukio hilo linaingiliana na Sheria ya Gharama za uchaguzi.
  Hali ya kisiasa katika jimbo hilo ni tete kutokana na upinzani mkali uliopo kati ya CCM na CHADEMA, sababu kubwa ni kutokana na kuwapo makundi, baada ya kura za maoni zilizoibua malalamiko mengi.


  chanzo>>
   
 2. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Haya sasa kazi inaendelea Je Jeshi la Polisi watatenda Khaki???????????????????????????? :A S 39:
   
 3. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  utaona tu kesi itakavyoishia heewaniiii!!
   
 4. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu patachimbika,,,,bado hawajajua anayofanya Ridhiwani,ni aibu!!!
   
 5. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongo dar es salaam
   
 6. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa matawi ya Chadema hawako makini. Moja wapo ya kazi zao ni kuwaelimisha wafuasi wao juu ya kutouza shahada zao
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kwa nini vingozi wa Chadema wanaruhusu hii kitu jamani?
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Huyu ndie kabisaaa anamwalibia baba yake na atampunguzia kura na kumkoseshea wabunge wengi tuu kwani kila apitapo anaacha kasheshe kwa wana ccm. yeye anajiendea tuu wala haangalii kuna matatizo gani au kujua hali ya kisiasa ya chama inaupepo gani hapo na ajue jinsi ya kukabili matatizo
   
 9. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watahangaika sana ila mwaka huu watakoma. Na bado 2015.
   
 10. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Aangalie nin wakat anajua ni chama cha familia? Ningependa niwepo hapa anapofanyia campaign ili nione anaongea pumba gan
   
Loading...