CCM wanaswa wakinunua shahada, mwizi ni mwizi tu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wanaswa wakinunua shahada, mwizi ni mwizi tu !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Oct 22, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  CCM wanaswa wakinunua shahada - Tanzania Daima
  Wakutwa nazo 180

  WAKATI juhudi za kuliokoa Jimbo la Bukombe ambalo liko katika hatihati za kunyakuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zikipamba moto, viongozi wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa wakinunua shahada kutoka kwa wapiga kura.

  Habari kutoka Bukombe ambazo zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Selemani Nyakipande, zinasema viongozi hao ni Juma Mhoja na Shadrack Paul, ambao ni makatibu wa Tawi la Ushirombo na Msonga.

  Alisema viongozi hao walikamatwa katika Kijiji cha Msonga, Kata ya Runzewe, wakiwa tayari wamenunua shahada 185 za kupigia kura kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wanarubuniwa na baadhi ya makada wa CCM ambao wako katika mkakati wa kuliokoa jimbo hilo.
  Viongozi hao walikuwa wakinunua shahada hizo kwa bei kati ya sh 2,000 na 5,000 huku lengo kuu likionekana kuwalenga zaidi wafuasi wa CHADEMA ili kudhoofisha nguvu iliyopo.

  Kamanda Nyakipande alisema polisi inaendelea kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai kuwa tukio hilo linaingiliana na Sheria ya Gharama za uchaguzi.

  Hali ya kisiasa katika jimbo hilo ni tete kutokana na upinzani mkali uliopo kati ya CCM na CHADEMA, sababu kubwa ni kutokana na kuwapo makundi, baada ya kura za maoni zilizoibua malalamiko mengi.
  Huko Zanzibar, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba, amewakoromea wanachama wa CCM wanaoendeleza makundi kutokana na chuki za kuanguka kwenye uchaguzi kuwa ni ‘washamba wa siasa’.

  Hayo ameyaeleza alipokuwa akizungumza na wanachama wa umoja huo, Tawi la CCM Kizimbani katika Jimbo la Dole, Wilaya ya Magharibi Unguja, akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ushindi kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.
  Aliwataka wanachama wa CCM kuvunja kambi zao na kujenga umoja ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi mkubwa Tanzania Bara na Zanzibar katika ngazi zote, kuanzia urais hadi udiwani.
  Alisema UWT taifa tayari imeshajipanga katika mikoa, wilaya, majimbo hadi katika wadi zote na wanachama wa CCM wahakikishe ushindi katika ngazi zote.
  Alisema baada ya kumalizika kura ya maoni na wagombea kupatikana, pande zilizokuwa zikipingana zilitakiwa zivunje kambi, lakini kuna baadhi ya wanachama hadi sasa wanaendeleza tofauti zao kwa kukosa ukomavu wa kisiasa.
  Alisema wapo wagombea walioshindwa kwa kura nyingi katika mchakato wa kura za maoni, ambao hadi sasa wanakataa kuwaunga mkono wale walioibuka washindi.
  Alisema ni kitendo cha kusikiktisha kuona wanachama hao wanatumia hata udini na ukabila, vitendo ambavyo ni sumu katika kudumisha umoja wa kitaifa ulioasisiwa na marehemu Mwalimu Julius Nyerere na mzee Abeid Aman Karume.
  Aliwataka wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali wajenge ushirikiano wa karibu na wenzao ambao walianguka na kuhakikisha chama hicho kinafikia malengo yake.


  CCM inatupeleka wapi ? Piga, ua na galagaza, ushindi ni lazima yasema CCM !


  Tanzania kweli twahitaji ukombozi
   
 2. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM hawafai hata kwa kazi ya uongozi wa chekechea. NI wezi wa kupindukia
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tusikubali kuongozwa na wezi
   
 4. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Hii inasikitisha sana jamani;Dr Slaa zungumzia suala hili kwenye mkutano wako wa leo na ukitolea mfano ujinga huu wa CCM wa kununua shahada za kura kama tayari kimepoteza uchaguzi!

  Chama kinachojitapa kama kitashinda kwa asilimia zaidi ya 89 ya kura zote kinajihusisha kwa nini kununua shahada za wafuasi wa chama kitachopata si zaidi ya asilimia 11 ya kura zote halali?

  Sidhani kama mchakato huu wa kununua stashahada za wafuasi wa CHADEMA ni amri ya CCM-Mkoa,nahisi huu ni uamuzi wa CCM-Taifa wakipata baraza zote toka makao makuu Lumumba!
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Ni vema Dr.Slaa akagusia wimbi la umwagaji damu linalosababishwa na wafuasi wa CCM akitolea mfano, Maswa Magharibi, Hai na pia azungumzie ununuzi wa shahada 185 uliofanywa na viongozi wa CCM.Hii iatasaidia kuelimisha jamii ielewe uozo wa chama cha JK NA SERIKALI YAKE wanavyojaribu KUBAKA DEMOCRASIA
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Wamekipata cha moto
   
 7. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti anasign sheria za uchaguzi, watendaji wanaveruga! Alisign kwa utashi wake kweli au alilazimishwa? Hii ni aibu kubwa sana!!!!
   
Loading...