CCM wanashikamana juu wakati mashina chini yanapukutika kwa kasi!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Magamba ni chama cha kushangaza kweli kweli! Wanashikamana juu, ambapo huko chini mashina yanapukutika kwa kasi ya ajabu, na hakuna hata mmoja anayeshtushwa na hilo!

Nawapa hongera CDM kwa kuanza kuirarua CCM kwa kutokea chini, ambako ndiko hujigamba kuwa ina nguvu kubwa.
 
tunaendeleza operesheni kimya kimya, wakija kustuka msingi umevunjika na paa ndo linadondoka.
Ehh Mungu, wape CCM moyo mgumu kama wa Pharao ili tuwatandike mapigo kumi ya hatari na mwishowe watasadiki, amen.
 
tunaendeleza operesheni kimya kimya, wakija kustuka msingi umevunjika na paa ndo linadondoka.
Ehh Mungu, wape CCM moyo mgumu kama wa Pharao ili tuwatandike mapigo kumi ya hatari na mwishowe watasadiki, amen.

Hongera sana mkuu i like it. huu ndo muda JK anatutakia mema CDM aendeleee kusubiri upepo upite halafu baadaye ataona kimbunga kinaingia hadi kwake na Ridh an Miraji wake
 
Ndio maana mb Visenti Nyerere aliwaambia CHAMA CHA MAGAMBA kuwa wanacheza sarakasi huku wamevaa mataulo........ lazima wabakie uchi. M4C inachukuwa kasi.
 
Mkuu wangu "mshikamano" wa kifisadi sio mshikamano bali ni ufalme uliofitinika ambao huanguka wenyewe. Wenye busara wachache wameanza kusoma maandishi ukutani lakini "mfalme" hataki kukubali kwamba yuko uchi. Sasa utupu wake nje nje hata watoto wadogo wanashuhudia sehemu nyeti za mfalme huyu mpumbavu CCM zikining'inia mchana kweupe.

Heshima ya mfalme imekwisha vimebaki vicheko vya dharau kila kona ya taifa lile baadhi "wakimhurumia" na wengine wakimdhihaki kwa upumbavu wake.
 
Back
Top Bottom