CCM wanarukia kila wanachokiona kitawaokoa - Wamesahau kuwa mabadiliko ni lazima

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Baada ya kuona upepo haupo tena upande wao na Jahazi la UKAWA linakwenda kwa kasi ya ajabu ,sasa CCM inarukia kila kinachowapitia mbele yao wakiamini kitawasaidia ,yaguju CCM inakwenda na kuburuzwa na maji na imeshapwelewa juhudi za kuikwamua zinaonekana kutofua dafu.

Machungu na ghadhabu walizonazo zinawapelekea kuganda na Lowasa kila wanapopita ni wao na Lowasa wamesahau kuwa Lowasa katoka kwenye choo kilichojaa na kutapakaa kuhamia kwenye nyumba safi.

Siasa za kistaarabu zimeanza kuwashinda na wameanza kuonyesha rangi yao halisi ya ubabe ,kupachua mabango kupachua bendera na kuzidi kutandaza uongo angalau waone kama hayo yatawasaidia lakini wapi MABADILIKO ni lazima na mabadiliko wanayohitajiwaTanzania wa leo ni kuona CCM inaondoka madarakani.

Mccm wasijidanganye mwaka huu wapange wapangavyo wanaenda zao ,mapingamizi Mungu kawalaani yamepigwa na chini,uchovu wa Slaa nao umeanza kuwadhuru.Sera za mgombea wao ni yale kwa yale tutajenga hospitali,tutajenga barabara ,sijui tutajenga hiki na kile ni yale kwa yale ya Kikwete na Mkapa ni yale yale yao ya CCM kupita wakidanganya wakiwadanganya wananchi safari hii hadanganyiki mtu CCM mtafute kazi za kupara miwa na kunywa maji yake ila kuipata serikali ya taifa la Tanzania ni kindende,halafu sahauni.
 
Joto hasira

Member
Nov 21, 2013
41
95
well said..hakuna ubishi hawa jamaa wako i.c.u wanapumulia mashine..wamejawa roho zakishetani tu kuhakikisha wanatugawa watanzania kwa rangi,makabila,na dini ili waendelee kufaidi mema ya nchi hii..hawajali tena chochote wao ni madaraka tu..kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho..lazima tuwachinje october hata mwenyekiti wao anaejiandaa kukabidhi dola kwa upinzani analijua hilo.
 
Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,194
2,000
system Imefail kwa mara nyingine tena, lipumba , slaa, maandamano, next kumuapisha President Lowasa
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
system Imefail kwa mara nyingine tena, lipumba , slaa, maandamano, next kumuapisha President Lowasa
Ni kweli kabisa CCM wanashindana na upepo wa mabadiliko na bado kwani kipimajoto kinapanda kikionyesha CCM huenda ikafa japo hatuliombi hilo.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,875
1,500
Hivi ile single wa CHADEMA ni Chama Wakiristu na

CUF ni chama cha waislamu imeishia wapi?

Chama kinachoingia madarakani kwa FITINA hakiwezi kuongoza kwa HAKI na kuleta maendeleo, kitaendeleza FITINA hata kikiwa madarakani.
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,892
2,000
walisema hawataki maandamano kipindi cha kampeni ghafla wao ndiyo wanasapoti maandamano ,... kiukweli mchezo wanao ucheza wakubali tu wameokota galasha .. wakae kimya na kijichanga upya
 
kiluvya

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,326
2,000
Wamechemka sanaa...watu wapo tayari kwa mabadiriko..tatizo ccm ni mfumo ndo umewafikisha hapo....nibora nipigie kura jiwe na sio chama dola...nimechoka nimechoka....
 
Sometimes

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
4,546
1,500
Laiti members wa JF wangekuwa ndiyo wapiga kura pekee, EL angekuwa anasubiri kuapishwa tarehe 26/10/2015! Lakini wapi, wenye vichinjio wengi wapo vijijini ambako smartphones ni nadra na TV mpaka vibanda vya kulipia!
 
Zagazaga

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
564
500
Laiti members wa JF wangekuwa ndiyo wapiga kura pekee, EL angekuwa anasubiri kuapishwa tarehe 26/10/2015! Lakini wapi, wenye vichinjio wengi wapo vijijini ambako smartphones ni nadra na TV mpaka vibanda vya kulipia!
jipe moyo mzeee
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Ningekuwa mimi niko kwenye msafara wa EL ningekuwa nahutubia kwa dkk tano! hoja kubwa ikiwa ni nini maana ya UKAWA basi!! KATIBA KATIBA! Unaua CCM asubuhi na mapema! hakuna haja ya kusema meeengi!
Yaani bahati ya mwaka huu kwa upande wa Upinzani ni nzuri sana,kwani wanachotaka kuona wananchiwa Taifa hili la Tanzzania ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani ,hawataki kusikia mambo ya sera wala ilani na CCM wanalijua hilo ,wananchi wamewabadilikia kiasi ya kufika kusema wako tayari hata kupigia au tuseme kulipa jiwe kura yao nakumbuka kura za CUF za maruhani.

Kwa ufupi UKAWA hawana haja ya kutangaza sera au kuzinadi ,kwani CCM wamefikisha hizo sera na ilani kuwa mambo ya kufikirika hayana ukweli,muda wa miaka hamsini si kidogo ikichukulia nchi haina machafuko ya ndani wala ya nje,nchi imejaa amani ,wananchi wake walikuwa si walalamikaji ni hewala kila kitu kinachonywa na CCM ,yaani shwari kabisa.

maneno matatu tu yanatosha kwa mtu aliepo UKAWA kuyasema na kushuka jukwaani Ondoa CCM Madarakani (OCM)
 
Chungurumbira

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,170
1,195

Huyo Magufuri wao sasa naye anasema ya UKAWA yaani elimu bure, mabati na saruji kushusha bei! huku ni kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwa!
 
MOSSAD II

JF-Expert Member
Apr 14, 2013
3,973
1,195
Laiti members wa JF wangekuwa ndiyo wapiga kura pekee, EL angekuwa anasubiri kuapishwa tarehe 26/10/2015! Lakini wapi, wenye vichinjio wengi wapo vijijini ambako smartphones ni nadra na TV mpaka vibanda vya kulipia!
labda kijijini kwenu lakini siku hizi watu wengi wa vijijini wanajitambua!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom