Kwa muda sasa kumekuwa na mkinzano wa mawazo kuhusu mwenendo wa siasa zetu na awamu za uongozi wetu hasa awamu ya nne na tano ambazo kwa haraka zimebatizwa majina ya dhaifu na kidikteta. Dhana hizi zimeibuka kutokana na matendo na maamuzi yanayofanywa na viongozi wakuu.
Katika awamu ya nne ya uongozi wa nchi uliokuwepo chini ya CCM wanamageuzi walipaza sauti kuhusu udhaifu wa uongozi wa nchi kushindwa kuchukua hatua hata pale ukweli wa wahusika waliofanya makosa ya wazi unapokuwa wazi, mfano, wizi wa ESCROW kutakiwa kurejesha fedha na kuachwa bila hatua mahususi. Na sakata la orodha ya wauza dawa za kulevya.
Wakati huo wana ccm walionekana kutetea maamuzi hayo kwa nguvu zao zote wakitumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili kutuaminisha kwamba huo si udhaifu bali ni mbinu muafaka mpaka leo hatujaona tija yoyote. Kilicho wazi ni kuwa udhaifu ulitetewa, uliota mizizi na hatimae yakawa mazoweya ya kulindana na ukawa ndio mfumo wetu hadi leo.
Awamu ya tano nayo ilianza kwa makeke yake ya kutaka kujitofautisha na kile kilichoitwa udhaifu. Tumeona mambo yanavyokwenda katika nchi. Sasa mambo yamebadilika lakini kwa namna yake.
Badala ya kuwa imara imekuwa ikionesha ishara ya udikteta.
Tumetoka kwenye udhaifu hadi maamuzi ya mtu mmoja, kutopingwa, na kukosa busara na uvumilivu sisi hii hali tuiteje ?
Kama unazuwiya uhuru wa kujieleza na habari, unazuwiya vyama visifanye mikutano ya wazi maana yake nini? ina maana hutaki kukosolewa na hutaki watu wahabarishwe vile unavyotenda.
Sio siri watu hali mbaya, uchumi wetu unalega lega, watu wanaonewa na kukandamizwa, halafu unataka wasisikike kuwe kimya tu kama kwamba hakuna tatizo ? hapana.
Ukweli huu sasa kwa bahati mbaya unatetewa na vijana na makada wa CCM. Kwamba hali hii ni njema kwa taifa na wanataka tuiache serikali ifanye kazi. Hawa watu hawa ..? Wanataka tusihoji ukakasi huu wa kuvunjwa taratibu na wanataka tubariki dhulma hii. Hapana.
Imefika mahala hata viongozi wadogo wa serikali hawako huru kufanya maamuzi ya kimamlaka waliyonayo, wanalazimika kusubiri mshindo wa ikulu unasemaje na wao ndio waamue kwa mluzi tu wa huko. Kuna uoga, mawaziri ni kama hawapo, kuna hofu ya kutumbuliwa tu ndio imetawala badala ya uweledi na uwajibikaji hii ndio hali.
CCM na taasisi zenu za chama tambuweni kuwa hatutanyamaza kamwe na hatutakubali kubariki njama za viashiria vya na au udikteta kuwa ndio mfumo wetu wa maisha.
Ikiwa mmeshindwa kuwashauri viongozi wenu kutumia njia ya CHECK AND BALANCE katika kuongoza na leo mnatuaminisha kuwa mbadala wa Udhaifu ni Udikteta na sio njia ya wastani basi endeleeni na juweni kuwa mko peke yenu.
Msituhukumu kwa kupinga udhaifu ule kwa kutuletea udikteta na kutaka tuukubali kama ndio malipo ya watanzania.
Tutaendelea kupinga na kupiga kelele tena kwa nguvu sana. Mbadala wa udhaifu usiwe udikteta.
Inawahusu watu huru na GT pekee.
Kishada.