KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Usinifanye kuwa kilaza kama wewe usiyeelewa kitu.Huwezi kunielewa.
Ila ujumbe ulitolewa leo ni kuwa humu nchini hakuna mwanasiasa atakayetoa kafara maslahi yake ya kiutawala ili ampatie maslahi mwanasiasa mwingine, katiba mpya ni fursa ya maslahi kwa baadhi ya wanasiasa na hatari ya kupoteza kwa baadhi ya wanasiasa hivyo kama kweli katiba unaihitaji sana, simama na wenzio ipiganie bila kutumia mwanasiasa.
Lakini ngoja nikusifu kwa kutambua hili uliloandika hapa mwenyewe, kama kweli unaelewa ulichoandika:
"Ila ujumbe ulitolewa leo ni kuwa humu nchini hakuna mwanasiasa atakayetoa kafara maslahi yake, ya kiutawala ili ampatie maslahi mwanasiasa mwingine"
Kama unaelewa maana ya maneno hayo uliyoandika hapa, sina sababu kabisa ya kuhangaika na wewe, ila kwa jambo moja tu usilolielewa vizuri kama inavyoonyesha kukomalia kwako kwa jambo hili.
Maslahi ya Tanzania (waTanzania), kamwe usiyachanganye na maslahi ya wanasiasa, iwe CCM, CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa.
Wananchi wataungana na chama chochote/ kundi lolote litakalosimamia matakwa yao kuondoa dhulma za wazi amabazo sasa CCM wanaonyesha kwa wananchi wa nchi hii.
Wewe utaendelea kuimba hapa ukidharau juhudi hizo zinazofanywa kwa njia mbalimbali, ikiwemo na kujifanya kwamba wananchi hawana mahitaji ya Katiba Mpya, kwa vile tu kundi lako la utawala linafaidika na hali hiyo. Kuwa kipofu kwa maksudi hiyo ni hiari yenu, lakini haitazuia mabadiliko yanayokuja kuwafyekea mbali kama hamtazinduka toka kwenye ndoto hizi mbaya zinazowasumbua wakati huu.
Unadai hapo juu, kwamba hakuna wananchi wanaoweza kukabili bunduki milioni tano. Nikuhakikishie kwamba haihitajiki wananchi milioni tano; laki tano hadi milioni moja inatosha kabisa kuwatupilia mbali wavunja haki za waTanzania nyinyi mliolewa madaraka.
Safari hii hamponi.