Elections 2010 CCM wanamkomoa nani: wapinzani au wananchi?

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Tumeandamana kupinga maamuzi ya nec kumtangaza Kikwete kuwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,, Chadema haina ugomvi na CCM, bali inaugomvi na Matokeo na uchakachuaji uliotokea Kipindi cha uchaguzi,, ambao uchakachuaji huo umefanywa na NEC,

Nawashangaa CCM wanatangaza kuandamana, eti Mwenyekiti amedhalilishwa,, kadhalilishwa wapi,, hivi CCM muko Serioue katika uongozi? hivi munafikiria Mukiandamana mutamkomoa nani Chadema? au Wananchi ambao mutawapa shida tuu ya kuungua jua na hakuna mutakacho wapa zaidi ya kunukishana jasho tu

hivi ni kweli CCM haina yafuatayo?
  1. Ndani ya CCM hakuna mafisadi ila kuna ufisadi!
  2. Fedha zilizochotwa kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT) zilikuwa kwa kazi maalum baadaye Waziri Zakia Meghji anajiumauma, "Aaah nanihii alinipotosha!"
  3. Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na wafuasi wake wanasema, "Elimu bure haiwezekani".
  4. Halafu meneja kampeni, Abdulrahman Kinana anashadidia, eti hata Mwalimu Nyerere hakusomesha watoto bure ila alikopa fedha nje kwa ajili ya kusomesha bure; fedha alizokopa zilianza kulipwa awamu ya tatu.
Mimi nasema Kazi hii huu ni mwanzo tuu,, na mwisho utapatikana soon wananchi ungeni mkono Chadema jamani....
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
hivi naomba kujua CCM wanamkomoa nani,, kwasababu wananchi ndo wanaathilika mojakwa moja jamani
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,228
2,000
hivi naomba kujua CCM wanamkomoa nani,, kwasababu wananchi ndo wanaathilika mojakwa moja jamani
Ndugu yangu...hili swali lako jibu lake ni kizungumkuti tu.
CCM haijali kukomoa wananchi na wananchi hawajali wakikomolewa na CCM!
Wewe toa solution ya kuondoa hii deadlock....basi!
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Solution M-mbabe ni Katibababa,, na Katiba haipatikani mpaka tuandamani,, so Maandamano ya amani yanahitajika jamani
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Ndugu yangu...hili swali lako jibu lake ni kizungumkuti tu.
CCM haijali kukomoa wananchi na wananchi hawajali wakikomolewa na CCM!
Wewe toa solution ya kuondoa hii deadlock....basi!
CCM inawakomoa wadanganyika kwa kuwa na wao wako tayari kukomolewa.
Usingefikili kwamba mtu mwenye akili timamu anaishi nyumba kama hii anaweza toa kura kwa kwa CCM. Lakini wengi walio katika hali kama hii wametoa kura zao amini usiamini.

View attachment 17181
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
CCM inawakomoa wadanganyika kwa kuwa na wao wako tayari kukomolewa.
Usingefikili kwamba mtu mwenye akili timamu anaishi nyumba kama hii anaweza toa kura kwa kwa CCM. Lakini wengi walio katika hali kama hii wametoa kura zao amini usiamini.

View attachment 17181
Hao ndio Wanachama wa CCM wenye Maisha bora,, CCM oyeeeeee
 

Ki tochi

Member
Oct 19, 2010
49
0
"CCM inawakomoa wadanganyika kwa kuwa na wao wako tayari kukomolewa.
Usingefikili kwamba mtu mwenye akili timamu anaishi nyumba kama hii anaweza toa kura kwa kwa CCM. Lakini wengi walio katika hali kama hii wametoa kura zao amini usiamini."

Kilimo kwanza watakuelewa ila maisha yatazidi kuwa magumu.
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Uwiano maalum Swali lako halina mantiki hata kidogo,, ni pumba na halihusiani na topic
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
kwa CCM hakuna jipya mi naona mambo yetu ni yale yale tuu,, sasa akili kichwani,, Mukitaka Uchaguz urudiwe
 

Lionheart

New Member
Nov 21, 2010
2
0
Katika maisha watu hawawezi kuwa level moja watu wote hawawezi kufanana katika matumizi na mahitaji Yao ya kila siku... Waswahili wanasema kila Mbuzi atakula kulingana na urefu wa Kamba yake
 

Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
794
250
Mi natoa Wito kwa Wananchi wote tuachane na hizi Itikadi za Vyama vyetu natuiangilie Tanzania.Tatizo kubwa la Watanzania pa1 na viongozi wetu ni kupuuzia Maswala ya Msingi bila kutafakari kwa kina madhara yake ya baadae,Juzi hapa tumetoka kwenye Uchaguzi na tumeshuhudia wote Utumbo uliofanywa na NEC nakukaribia kuhatarisha Amani,ivi mnafikiria tukiendelea kuwa na Tume ya aina hii ktk Uchaguzi wa 2015 Amani itakuwepo!!Tuitumie Chadema kama njia tu na kuiunga mkono katika kuhakikisha inapatikana Tume huru itakayotenda haki nakuaminiwa na Watanzania wote.Tusipotoshwe na Wanasiasa kwa Maslahi yao Binafsi Swala La Katiba ni muhimu kwa Ustawi wa Demokrasia na Amani katika Nchi yetu.
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Ibra Mo kaka umeongea kitu cha maana sana na kama hawata kifuata basi wao ni mambumbumbu au wanafanya makusudi kwakuwa ni wezi tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom