CCM wanamkimbiza mtu mwenye pumzi kuwazidi, katoka hatua 100 hadi 1000!!

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
Katika siasa kuna mambo mengi hufanyika ili kujijengea heshima na sifa kwa wananchi. Hivyo wanasiasa hutafuta kila njia kuhakikisha wanawavuta wananchi upande wao. Katika sakata la makinikia CCM wamekua wajanja sana kutaka sifa ziwaendee wao huku wakiwachafua wapinzani waonekane sio wazalendo na ni wateteaji wa wezi. Sasa wapinzani wamebadili mbinu ili kwenda sambamba na CCM.

Lissu amewaambia mara kadhaa kwamba njia inayotumika na mheshimiwa rais sio sahihi ya kuzuia mchanga bila kufuata utaratibu . Hawa wawekezaji siku wakiamua kutushitak tutakua hatuna pa kuponea. Ccm wakasema hakuna kanuni ya kumkamata mwizi . Hakuna taratibu kumshughulikia mwizi . Unaweza kufanya vyovyote vile ili mradi unatimiza lengo lako la kulinda raslimali za nchi.
Wakaenda mbali zaid na kumwita Tundu Lissu anatetea wezi.

Sasa upinzani wamefikiria na kugundua njia sahihi ya kukimbizana na ccm katika hii ajenda ya kujizolea sifa kwa wananchi. Tukumbuke hili swala kwa liliopofikia limekua la kisiasa zaid kuliko kitaalam.

Wapinzani wamekuja na ajenda hii hapa. Kwa vile mnasema hawa ACACIA NI WEZI, na mnasema hakuna kanuni ya kupambana na wezi , hivyo basi tunawaomba wananchi wamsaidie mheshimiwa rais Kwa kuzuia usafirishwaji wa dhahabu nje ya nchi kutokea migodini. Wananchi wahakikishe ndege hazitui wala haziruki katika viwanja vilivyo migodini ili kuzuia kutorosha dhahabu. Yaan upinzani wameenda mbali zaid kwa kusema. Haiwezekani uzuie mchanga huku unaruhusu dhahabu kutoroshwa. Dhahabu na mchanga kipi kina thamani kubwa? Kama unalia kwa kuibiwa kupitia mchanga iweje ufurahie kuibiwa dhahabu pure??

Yaan ccm waliwakimbiza wapinzani hatua 100 wao wameenda nao hatua 1000 mbele. Sasa pumzi ya CCM imekata wanaanza kulia kwa kuwaona wapinzani wanahamasisha kujichukulia sheria mkononi. Mie nauliza hivi . Ni sheria gani mheshimiwa rais katumia kuzuia mchanga!?wapinzani wanataka migodi yote ichukuliwe hatua CCM mnataka kupambana na ACACIA TU! Kwa hapa nani anatetea wezi??

Niwakumbushe wana jamii forum. Kwa wale wanaotumia akili kufikiri na sio kiungo kingine . Mheshimiwa HECHE zile kauli zake za kuhamasisha wananchi wake wajiandae kuvamia migodi haikuwalenga wananchi, kimsingi ilikua inamlenga mheshiwa rais. Alikua anamwambia hivi , aprochi yako kuwaita hawa wezi si sawa. Hata kama wanatwibia ni kwa ujinga wetu kupitia mikataba. Hivyo tunapaswa kubadir mikataba. Njia sahihi sio kuwaita wezi kwa kuzuia mchanga huku dhahabu wanaendelea kuchimba. Wananchi wanakuelewaje? Kama ni wezi mbona hujawazuia kuendelea kuzalisha?? Na kingine kwani kuna mgodi ambao tunanufaika nao ? Mbona migodi mingine huigusi??kwan wanaotwimbia ni ACACIA pekee??
Wananchi nendeni mkazuie wezi kuendelea kuzalisha madini.

Sasa nawauliza wa jamii forum , kati ya ccm na upinzani nani wanatetea wezi. Upinzani wanaosema uzalishaji wote usimame au ccm wanaosema mchanga usiende??

Usimkimbize mtu bila kujua pumzi yake!!
 

successor

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
3,061
2,000
Ukitaka kudumu ndani ya CCM lazima uwe mnafiki, hiyo ndio sifa kubwa ya mwanaCCM yeyote yule, kuanzia mwanachama wa kawaida, kiongozi wa shina hadi taifa.
 

nygax

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,070
2,000
Duh! kumbe mada imeshahama kutoka `tutashtakiwa' mpaka `pure gold' twende kazi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom