CCM wanajua wawekezaji wataikimbia nchi baada ya Vodacom kutangaza hasara iliyotokana na tozo?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Wote naamini tumeliona lile tangazo la kampuni ya Vodacom, lenye kichwa cha habari cha TAARIFA KWA UMMA, ambalo lilielezea kuwa kampuni hiyo imepata hasara ya Shs. Bilioni 103.8 Katika mwaka uliopita wa Fedha, kutokana na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kuanzisha hizi tozo zake kwa wananchi.

Hivi huyu Mwigulu Nchemba, anajua "impact" ya tangazo hilo kwa uchumi wa nchi hii??

Ni dhahiri kuwa hivi ninavyoandika "post" hii, wawekezaji kwa maelfu, aidha walioko nchini hivi sasa, au wale waliopanga kuja nchini kuwekeza, weshabadili mawazo na kuamua kutowekeza nchini kwetu.

Ninajaribu ku- imagine, hivi huyu Mwigulu Nchemba, ni kwanini ana roho ngumu kiasi hiki na hataki kujiuzuru, pamoja na kuwa yeye ndiye "source" ya janga hili la kuporomoka vibaya kwa uchumi wetu, kutokana na tozo zake za dhuluma, ambazo wananchi wamezipigia kelele Sana??

Huyu Mwigulu Nchemba, amefikia mahala anatudhihaki watanzania, eti asiyetaka kulipa tozo hizo ahamie nchi jirani ya Burundi!

Lakini hiki kiburi na jeuri anayoonyesha huyu Mwigulu Nchemba, inatokana na hii nchi kutokuwa na Katiba mpya ambayo itakuwa yenye kukidhi mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, kwa kuwa yeye Mwigulu anajua hata kama Umma wa watanzania watapinga tozo hiyo, lakini wakati wa uchaguzi mkuu utakapofika, Tume ya uchaguzi, itamtangaza yeye, kuwa mshindi, kwa kuwa tu ni mgombea wa CCM!

Lakini angejua thamani ya sanduku la kura, asingefanya uamuzi wa hovyo kiasi hiki.

KWA hiyo ni muhimu sana kuliko kitu chochote Katika nchi hii kwa hivi sasa, Rasimu ya Jaji Warioba, ambayo ndiyo Katiba iliyotokana na maoni yetu wananchi, irudi mezani na ndiyo itakayokuwa mkombozi wa Maisha yetu watanzania

Mungu ibariki Tanzania.
 
Waondoke tu kwakweli. Ningekuwa na media yangu ningeanza kupiga promo la kuhamasha wawekezaji kuondoka nchini. Nchi ya kihuni hii.
 
Wote naamini tumeliona lile tangazo la kampuni ya Vodacom, lenye kichwa cha habari cha TAARIFA KWA UMMA, ambalo lilielezea kuwa kampuni hiyo imepata hasara ya Shs. Bilioni 103.8 Katika mwaka uliopita wa Fedha, kutokana na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kuanzisha hizi tozo zake kwa wananchi.

Hivi huyu Mwigulu Nchemba, anajua "impact" ya tangazo hilo kwa uchumi wa nchi hii??

Ni dhahiri kuwa hivi ninavyoandika "post" hii, wawekezaji kwa maelfu, aidha walioko nchini hivi sasa, au wale waliopanga kuja nchini kuwekeza, weshabadili mawazo na kuamua kutowekeza nchini kwetu.

Ninajaribu ku- imagine, hivi huyu Mwigulu Nchemba, ni kwanini ana roho ngumu kiasi hiki na hataki kujiuzuru, pamoja na kuwa yeye ndiye "source" ya janga hili la kuporomoka vibaya kwa uchumi wetu, kutokana na tozo zake za dhuluma, ambazo wananchi wamezipigia kelele Sana??

Huyu Mwigulu Nchemba, amefikia mahala anatudhihaki watanzania, eti asiyetaka kulipa tozo hizo ahamie nchi jirani ya Burundi!

Lakini hiki kiburi na jeuri anayoonyesha huyu Mwigulu Nchemba, inatokana na hii nchi kutokuwa na Katiba mpya ambayo itakuwa yenye kukidhi mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, kwa kuwa yeye Mwigulu anajua hata kama Umma wa watanzania watapinga tozo hiyo, lakini wakati wa uchaguzi mkuu utakapofika, Tume ya uchaguzi, itamtangaza yeye, kuwa mshindi, kwa kuwa tu ni mgombea wa CCM!

Lakini angejua kuwa thamani ya sanduku la kura, asingefanya uamuzi wa hovyo kiasi hiki.

KWA hiyo ni muhimu sana kuliko kitu chochote Katika nchi hii kwa hivi sasa, Rasimu ya Jaji Warioba irudi mezani na ndiyo itakayokuwa mkombozi wa Maisha yetu watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Mtuache bana sisi tuna phd za uchumi
 
Mwigulu atajiuzulu vipi wakati mama yupo nyuma yake.? Tatizo linaweza kuwa Mwigulu lkn tatizo kubwa ni mama.
 
Nawashukuru sana vodacom wamenipa gawio la Mia nane ....

9I815T32Y47 Imethibitishwa.Umepokea Tsh897.00 kutoka 219777 - M-PESA FAIDA tarehe 8/9/22 saa 11:44 PM Salio lako ni M-Pesa ni Tsh........75.

Hii nayo TOZO inahusika!
Mimi wamenipa 56 asubuhi hii
 
Back
Top Bottom