CCM Wanajidanganya kuhodhi mchakato wa Katiba ni wa wananchi wote

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Ukifuatilia hoja za wana CCM kama vile Jenista Mhagama Bungeni utashangaa. Wanajisahau kiasi kwamba wanadhani katiba ya nchi ni mali ya CCM. Muda huu siyo wa CCM kudanganya wananchi. Huwezi kutenganisha mchakato wa kuunda katiba na katiba yenyewe. Lazima kila mwananchi ashiriki na akubali mchakato wa kutafuta katiba kabla hata katiba yenyewe haijapendekezwa. Hivyo, mjadala kuhusu namna ya kuunda tume ni muhimu sana sawasawa na kupendekeza nini kiwe ndani ya katiba. Kwa vyovyote vile mchakato wa kutafuta tume lazima ujali usawa na masilihi wa wote ili mchakato usitoe mwanya kwa chama na hasa CCM kuhodhi nani aingie kweye tume na nani asiwepo kwenye tume ya kuunda katiba. Tume lazima iwe na uwakilishi wa usawa na hili linawezekana ikiwa kwanza makubaliano yafikiwe juu ya tume hii. CCM wanachokosea wanadhani katiba hiyo ni yao na siyo ya watanzania wote. Hili ni kosa kubwa sana. Hakuna mwananchi atakayekubali CCM kuhodhi mchakato wa katiba, ni ya wote. Na hivi kwa nini Zanzibar wawe na sauti kubwa kiasi hicho wakati wao siyo nchi? Kwa nini Zanzibar waamue mambo ya bara hata yasiyohusu muungano wakati wao waliandaa katiba peke yao bila kuhusisha wabara. Nani atakayekubali upuuzi huu? Hakuna.
 
Hili ndo tatizo la wabunge wa CCM. They cant see the obvious. Utawasikia nampongeza Rais, tunatekeleza Ilani ya CCM. Wanatakiwa kujua watu kwa sasa wana uelewa mkubwa na haogopi tena. Wao wenyewe kwenye chama ni kama walokole wanaonena kwa lugha tofauti zisizoeleweka na kudai wameshukiwa na roho mtakatifu
 
Back
Top Bottom