ccm wanajibu hoja za chadema kwenye mkutano wao hapa tegeta kwa ndevu

zamlock

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
3,840
657
chama cha mapinduzi kinafanya mkutano wake hapa tegeta kwa ndevu na ajenda kubwa ni kujibu hoja za chadema kuhusu dowans, mfumko wa bei, kupanda kwa ghalama za umeme, hizo ni taarifa nilizopata kutoka ndani ya uongozi wa chama lakini imekuwa ni siri kubwa mpaka saizi wana chama wamejikusanya na miziki ya taarabu inapigwa na wananchi wamesogea kwa ajili ya kutaka kujua nini kitazungumziwa hapa saizi lakini kwa taarifa za ndani zinasema mpaka saizi hata viongozi wa matawi awajajua ajenda ni nini na wao wamebaki wameshanga nitawapa taarifa mkutano utakapo anza na viongozi wao watakapofika,
 
jamani ccm kweli wamechoka wanajibu hoka zao kwa njia ya ajabu sana wanatoa maneno ya kejeli yuko hapa mbunge wa ilamba magharibu ndye anayejibu hoja ambazo ajui kiini chake ni aibu sana huu mkutano umepwaya sana
 
Tafadhali tupo kila kitu coz tuna hamu ya kujua watajibu vp hizo hoja. Makamba(mzee mtoto) atakuepo?
 
huyu mbunge lameck anashangaza sana kusema anataka kutoa ajira kwa kukopesha pikipiki 30 kwa kila kijana hapa tegeta sasa swali linakuja kwa nini asiende kusaidia kwenye jimbo lake ilamba magharibi mpaka aje kusaidia kwenye jimbo la kawe hapa au ndio uchokozi kwa sababu jimbo linaongozwa na halima mdee
 
Huko ni kupagawa. Kwa sasa CCM wanayo kazi nzito ya kupangua hoja mpaka waeleweke kwa wananchi. Leo nilikuwa kwenye msiba wa ndugu yangu hapa Makambako Mbunge wake Jah People kama kawaida na kibendera chake cha CCm kwenye gari eti anajipendekeza kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye naye alikuwepo
Ushauri: CCM watumie watu makini kujibu hoja tena wawe systematic sio kukurupuka mara Tambwe, chiligati,Makamba sijui shigela yaani vurugu tupu
 
wasije kujibu wakajifunga zaidi...baadae wakapingana wao wenyewe ...mpaka mabalozi nyumba kumi watajibu vioja,yalaaaaa...toooba!
 
mkutano ndo umekwisha na wananchi wamekaa na kujihoji iweje huyu mbunge wa iramba magharibi aje kuzungumzia maswala ya jimbo la kawe na kusema atoe msaada wa kukopesha pikipiki kwa vijana 30 kwa tegeta, bunju, makonde, na boko hapo ndipo wananchi waliwafuata waandishi wa habari wakitaka kuhojiwa ili waweze kuuliza iweje huyu mbunge ashindwe kupeleka msaada huo wa boda boda kwenye jimbo lake mpaka ailete hapa kawe kwakwel wananchi wamekuwa na muamko wa hali ya juu sana na wamekuwa wazi mbele yake kumweleza janja za siasa hizo atuzitaki kwa kweli kwa mtizamo wangu na hisi hata huyu mbunge lameck atajihoji sana kwa nini amebeep pasipo takiwa, na pia wamemaliza kwa maneno ya kejeli kuwa padri na mpiga disco kamwe awawezi kuongoza nchi hii na ndipo wananchi walipoamka na kuanza kuwashambulia kwa maneno makali kwa sababu waligusa ambapo apakutakiwa kugusa
 
naona wamewapeleka na masheikh pia huko arusha leo walikua na mhadhara msikiti wa bondeni
 
Back
Top Bottom