CCM wanafiki, wamtekeleza Sioi Sumari baada ya matokeo kutangazwa

:heh:Ndio ajifunze kupitia makosa,we unadhani Mkapa angesubiri na zile kashfa alizotoa jukwaani wakati wa uzinduzi.

Walikuwa wanajua wameshindwa kuiba kwa hiyo lazima matokeo yawe ovyo ndio maana wengine wamekimbia.

:A S 576:
Adelina.
 
mwenyewe nilishangaa kumuona asubuhi asubuhi akitetetmeka peke yake bila hata wale walinzi wake. hata nywele akuwa hajachana wala kuvaa zile nguo za ccm. halafu alionekana kuwa na aibu halafu mdomoni alionekana mwenye hamu ya kuvuta sigara.
 
mwenyewe nilishangaa kumuona asubuhi asubuhi akitetetmeka peke yake bila hata wale walinzi wake. hata nywele akuwa hajachana wala kuvaa zile nguo za ccm. halafu alionekana kuwa na aibu halafu mdomoni alionekana mwenye hamu ya kuvuta sigara. muangalie u tube kwenye kutangaza matokeo.
 
wanafiki wakubwa hao wewe utamnadi vipi mgombea wakati yeye mwenyewe hajipigii kura.Namshauri mh E.Lowasa ajifunze kutokana na wakati next round ni jimboni kwake Monduli ajiandae kupisha nji,peoplesssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssss pooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooower
 
Katika hali isio ya kwawaida, Mgombea wa CCM bw.Sioi Sumari, alijikuta akiwa peke yake kwenye chumba cha kuhesabu kura, huku wapambe Livingstone Lusinde,Mwigulu nchemba,Christopher ole Sendeka, na wapambe wengine wakitokomea kusiko kujulikana, wakimwacha Ndg.Sumari peke yake, ikionekana kana kwamba ametekelezwa huku hajui kilichokuwa kikiendelea na ikisemekana baadhi ya magamba wako njiani kuelekea Dar, nakushauri ndg.Sioi uhamie tu CDM, uendeleze mapambano na Mh.Joshua Nassari katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru

Asije CDM huyu,sisi hatutaki linkage na Mafisadi. NAMSHAURI siyoi AENDE MONDULI AKAOMBE KIBARUA CHA KUCHUNGA NG'OMBE.
 
Jamani acheni kuwalaumu akina mwigulu, lusinde na mkapa. Hata kama ni wewe ungesubiri kuaibika vile? Mii nashukuru walivyokimbia mapemaaaaaaaaaaa, kupotezea
 
pole Sioi. ndo siasa zetu hizo. jipange na tazama mbele. tafuta kitu kizuri zaidi cha kufanya na si siasa. in fact kama unataka siasa, kuingia kwa gea ya CCM kwa Tanzania tuliyomo sasa ni tatizo kubwa zaidi. CCM ni liability kwa Watanzania kisiasa kwa sasa kuliko chama kingine chochote. tujiandae na mgombea binafsi na hapo ndo utaona watu wengi waliokuwa CCM watakapoishia huko!!! Pole ndugu yangu, ila rudi kwenye profession yako na jipange kwa yaliyo mbeleni. Narudia tena, achana na CCM. She is a dead body!!!
 
Katika hali isio ya kwawaida, Mgombea wa CCM bw.Sioi Sumari, alijikuta akiwa peke yake kwenye chumba cha kuhesabu kura, huku wapambe Livingstone Lusinde,Mwigulu nchemba,Christopher ole Sendeka, na wapambe wengine wakitokomea kusiko kujulikana, wakimwacha Ndg.Sumari peke yake, ikionekana kana kwamba ametekelezwa huku hajui kilichokuwa kikiendelea na ikisemekana baadhi ya magamba wako njiani kuelekea Dar, nakushauri ndg.Sioi uhamie tu CDM, uendeleze mapambano na Mh.Joshua Nassari katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru

Hapo kwenye red sijapaafiki.
 
Sidhani kama kuna haja ya kulaumu watu. Kama kura zilikuwa hazitoshi na uwezekano wa kuziongeza kwa mazabe ulikuwa umefungwa pingu na vijana wa CDM waliokuwa wanalinda kura basi ni dhahiri kuwa kwa usalama na aibu ilibidi wapambe wakimbie, hata hivyo Sioi bado alikuwa na wawakilishi wengi tu kutoka chama chake na mmoja wapo ni msimamizi wa uchaguzi.

Nafikiri Sioi asijione mnyonge sana ila achukulie uchaguzi huu kuwa ni 'Training ground ya siasa kuelekea 2015'. Ila next time asitumie sana pesa kuomba uteuzi wa chama maana uteuzi wa chama si guarantee ya kuwa mbunge.
 
Back
Top Bottom