CCM wana jipya lolote kutoka Dodoma?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Ilikuwa ni weekend ya vikao vya CCM, kuanzia kikao cha Kamati ya Maadili, then CC na hatimaye NEC. Je, kuna habari yoyote ya maana kutoka huko kwenye hivyo vikao ambavyo vimetawaliwa na usiri mkubwa??
 
Ilikuwa ni weekend ya vikao vya CCM, kuanzia kikao cha Kamati ya Maadili, then CC na hatimaye NEC. Je, kuna habari yoyote ya maana kutoka huko kwenye hivyo vikao ambavyo vimetawaliwa na usiri mkubwa??

Duh! Kwa hili nadhani tumsubiri mtaalamu wake mzee wa sauti za umeme FMES, labda atakuwa na mawili matatu kutoka huko. Personally sina clue yoyote kwenye hili
 
Ina ashiria nini? Maamuzi yamekuwa magumu ama agenda zimekuwa nyingi?
Hapana, ratiba ndiyo ilipangwa hivyo. Ajenda za leo hazikuwa ngumu sana-masuala ya usalama wa chakula na hali ya siasa. Ngoma nadhani ipo kesho watakapojadili masuala ya uchaguzi
 
Ina ashiria nini? Maamuzi yamekuwa magumu ama agenda zimekuwa nyingi?

Hapana, ratiba ndiyo ilipangwa hivyo. Ajenda za leo hazikuwa ngumu sana-masuala ya usalama wa chakula na hali ya siasa. Ngoma nadhani ipo kesho watakapojadili masuala ya uchaguzi
Nasikia kuliibuka ubishi kidogo baada ya juhudi za kutaka kurudisha umoja na mshikamano kwa wana CCM kuelekea 2010 baada kwani wengine walihoji 'utampatanishaje wezi (mafisadi) na wenye mali (wapinga ufisadi)...

MN kama upo maeneo hayo basi tuwasiliane mkuu, I will give you a call tomorrow
 
Kuna mtu ameona maandiko yaliyobandikwa jukwaani mbele kwenye kitambaa cha kijani, yanaonekana yanalenga ujumbe fulani, knimeona kwa michuzi sentensi inapoishia lakini sijui inaanzaje. Nahisi ni sentensi nzuri kama wadau tutaioona.
 
MKuu FMES alijiuzuri kuleta habari za kikachero za vikao vya CCM, sasa shida tupu, Mzee ES come back plaese, no body to fill the gap.
 
Kuna usiri mkuu wa ajabu safari hii ndani ya vikao vya CCM,lakini nyepesi nyepesi ni kuwa kuna wajumbe waliotaka kumtosa Makamba kutoka kwenye nafasi ya ukatibu Mkuu.

Inasemekana kundi la wazee ndani ya CC ndio waliomtetea kwamba akiondolewa kutakuwa na ufa mkubwa ndani ya chama.Je makamba anawayaunganisha makundi yapi.Mimi nafikiri ndiye kiungo wa mafisadi ndani ya CC na ndiyo sababu inakuwa vigumu kumtema.Vinginevyo angeshapoteza nafasi hiyo muda mrefu.
 
- Duh! Wakuu naona inatia huruma kweli hapa, ngoja tutafute dataz za kweli sasa,

- So far wakulu wote wako kikaoni, lakini tutakuwa nazo wakimaliza tu na kama kawa tutaziweka hapa soon!

Respect.

Kamanda Field Marshall Es!
 
wote wanafiki hawana jipya zaidi ya kupanga kuiba kura 2010. Tuwe ngangari ili kuiokoa nchi.
 
Ilikuwa ni weekend ya vikao vya CCM, kuanzia kikao cha Kamati ya Maadili, then CC na hatimaye NEC. Je, kuna habari yoyote ya maana kutoka huko kwenye hivyo vikao ambavyo vimetawaliwa na usiri mkubwa??

CCM mambo mazito !
http://www.majira.co.tz/index.php?v...zito-&format=pdf&option=com_content&Itemid=57
http://www.majira.co.tz/index.php?v...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57
http://www.majira.co.tz/index.php?o...0by0mb3B0aW9uPWNvbV9jb250ZW50Jkl0ZW1pZD01Nw==

Monday, 17 August 2009 07:23
*Vigogo wavutana siku mbili, NEC yakutana saa 12 jioni
*Watuhumiwa ufisadi taabani wainamisha vichwa
*Kamati Kuu sasa yasukuma hatma yao kuamuliwa NEC
*Makundi yajipanga kila moja kulinda maslahi yake

Na John Daniel, Dodoma

Majira

KATIKA hali inayothibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakabiliwa na mtihani mgumu katika historia yake, kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kimelazimika kufanyika kwa siku mbili kutokana na kile kilichoelezwa, mvutano wa ajenda nzito zinazotishia hatma ya chama.

Kwa mujibu wa ratiba, kikao kicho kilipangwa kufanyika kwa siku moja (Jumamosi) na kupisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichopangwa kuanza jana asubuhi.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya CC kilidokeza kuwa wajumbe walipata wakati mgumu kufikia maamuzi ya ajenda mbalimbali ambazo nyingi, zililenga kile kinachoelezwa kutaka kurejesha maadili yanayopukutika kwa kasi ndani ya chama hicho kikongwe nchini.

Kundi linalodaiwa kuchukua mrengo wa kukumbatia mafisadi, lilisimama kidete kupinga ajenda hiyo kwa maelezo kwamba inahatarisha uhai wa chama na inaweza kukisambaratisha jambo lililozua mjadala mkali na kikao hicho kulazimika kufanyika kwa siku mbili.


"Kama mlivyoandika Jumamosi, agenda ni hizo hizo na kweli zimeleta mjadala mkali lakini lile la Richmond ndio linaendelea, kwa mwendo huo, NEC itawaka moto na inaweza kufika Jumanne (kesho)," kilisema chanzo chetu.

Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya kikao hicho ulibaini kuwa mgawanyiko mkubwa katika CC ulichangiwa na kundi lililotaka chama hicho kijisafishe suala la ufisadi kwa gharama yoyote ikiwemo kuwaondoa wote wanaotuhumiwa mara moja.

Hata hivyo hali inaonekana si shwari wa watuhumiwa ufisadi ndani ya chama kutokana na mapendekezo mazito ya CC kwenda NEC ambayo inatakiwa kutoa maamuzi ya mwisho dhidi ya watu hao.

wachunguzi wa mambo mjini hapa, wametafsiri hali hiyo kuwa CCM tayari imeanza kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa hao jambo lililothibitishwa na baadhi ya wanachama wanaotuhumiwa kuonekana wamenyong'onyea, kuashiria kupata mshtuko mkubwa.

Wakati CC ikielezwa kuweka wazi kutaka hatua za haraka na baraka za NEC dhidi ya mafisadi, kulikuwa na kila dalili ya kikao cha NEC kilichoanza jana saa 12 jionikutawaliwa na mjadala mkali na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kupata wakati mgumu kuongoza kikao hicho.

Hata hivyo inadaiwa kuwa kundi linalodaiwa la mafisadi nalo limejipanga kuhakikisha watu wao wanakuwa salama bila kuathiriwa na NEC jambo linaloongeza ugumu wa kikao hicho.

Kuhusu uhalali wa vikao vya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili kero za Muungano, CC imetaka wapinzani kutambua kwamba Makamu wa Rais ndiye Mwenyekiti wa vikao hivyo na kwamba ataendelea kuhudhuria.

Ajenda zingine zilizotarajiwa kujadiliwa na NEC jana jioni ni pamoja na malipo ya walimu, Mkataba wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mkataba wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) kundi la wabunge machachari wanapinga ufisadi bungeni, pamoja na hali ya uandikishiwaji Daftari la Kudumu la Wapigakura Tanzania Visiwani.

Ajenda zingine ni Hali ya siasa na chakula nchini pamoja na matokeo ya chaguzi mbili za Biharamulo na Busanda.



 
Wanasema safari hii mambo yamezidi kuwa magumu Zanzibar kwani wamevuruga mapema katika mikakati ya kukwiba kura na hivyo inawezekana kabisa Watanzania walio wengi wakaamka kutoka usingizini na kusababisha kizaa zaa cha kuibuka kwa kishindo anguko la wabunge wa CCM hapo 2010.
 
Back
Top Bottom