CCM wamtumia salamu Sugu 'kaa mkao wa kula'

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
2,000

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amemtumia salamu Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwa akae mkao wa kula katika Jimbo analoliongoza.

Dkt. Bashiru kuelekea uchaguzi Mkuu amesema hakuna uchawi, wizi, kupendelea huku akiwataka waache visingizio wachape kazi.

"Bwana Sugu kaa mkao wa kula nakuja kwako hakuna uchawi kuna kazi, hakuna sijui wizi sijui kupendelewa acheni visingizio," alisema Dkt, Bashiri akiwa Dodoma.

"Chapa kazi ya siasa mpate dawa yenyewe iingie mpone hiyo ndio CCM mpya lakini ni vizuri tukahamasisha Watanzania wengi kushiriki katika uchaguzi ikiwezekana wote wenye umri wa kupiga kura."
 
Livejr

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,645
2,000
Unafikiri Sugu atajibu huu uharo?

Uwanja wa siasa za majukwaan upo kwa Ccm tu.

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amemtumia salamu Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwa akae mkao wa kula katika Jimbo analoliongoza.

Dkt. Bashiru kuelekea uchaguzi Mkuu amesema hakuna uchawi, wizi, kupendelea huku akiwataka waache visingizio wachape kazi.

"Bwana Sugu kaa mkao wa kula nakuja kwako hakuna uchawi kuna kazi, hakuna sijui wizi sijui kupendelewa acheni visingizio," alisema Dkt, Bashiri akiwa Dodoma.

"Chapa kazi ya siasa mpate dawa yenyewe iingie mpone hiyo ndio CCM mpya lakini ni vizuri tukahamasisha Watanzania wengi kushiriki katika uchaguzi ikiwezekana wote wenye umri wa kupiga kura."
 
mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,196
2,000
lLa ana muogopa sana S ugu, mpaka unampa taarifa nakuja kwako,? Kwa nini atoe taarifa? Anadhani Sugu ni mtu wa mchezo mchezo eee? Akitaka kuijua nguvu ya Sugu wamruhusu afanye mkutana siku moja na Bashiru tena wa hadhara ndio atajua uchawi au kazi...Anasema hakuna uchawi wakati Gamboshi wamejitokeza tayari? Hovyoo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom