Katibu Mkuu wa CCM atoa onyo kwa Membe akimtaka kutokuwa juu ya katiba ya chama

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
77a00ec04d6edcc2823d3dadba9dd61f

Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 27 Novemba 2019 na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM, wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV, kupitia chaneli yake ya Youtube.
Dk. Bashiru ameeleza kuwa, kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu.
“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika. Kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.

Desemba mwaka jana, Dk Bashiru Ally alimtuhumu hadharani Bernard Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha John Magufuli katika uchaguzi wa urais. Akijibu tuhuma hizo, Membe alieleza kushangazwa na mfumo uliotumika kumuita huku akieleza kuwa labda ni kutokana na ugeni wa Dk. Bashiru.

Membe alisema: “Nilituhumiwa na Katibu Mkuu Dk. Bashiru Ally kuwa ninaihujumu Serikali ya Awamu ya Tano na kunitaka nifike ofisini kwake kujibu tuhuma baada ya kudai hana namba yangu ya simu. Na mimi kwa kumheshimu Katibu wangu wa chama tarehe 7, Desemba mwaka jana nilimpelekea barua kwa dispatch (ushahidi) na kusainiwa nikimuomba kunipangia siku, muda na tarehe ya kufika kwake lakini cha kushangaza ameendelea kukaa kimya.”
 
77a00ec04d6edcc2823d3dadba9dd61f

Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 27 Novemba 2019 na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM, wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV, kupitia chaneli yake ya Youtube.

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika. Kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.
Hiyo kauli "Utamaduni wa chama" ilizaliwa wakati wa mzee Makamba akiwa katibu mkuu wa CCM, unataka kujua ilikuwaje hadi akasema hivyo? Je Bashiru anatoa kauli hii akionya jambo lile lile? Endelea kukaa nami online upate udambwi udambwi kamili hapa hapa jukwaa la siasa!
 
77a00ec04d6edcc2823d3dadba9dd61f

Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 27 Novemba 2019 na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM, wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV, kupitia chaneli yake ya Youtube.

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika. Kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.
Kwa Bashiru Ally.
Membe ni mtu mdogo sana kwa CCM na wala sio tishio ila wenyewe ndio mnampaisha.
Jambo la pili CCM imekufa na dalili zipo wazi.Ukiwa Muislamu unajua wazi kuwa wakati wa kuswaliwa maiti huwa tunasema "Mleteni maiti" na hatusemi mleteni Rashid wala Juma.
Kinachoendelea nchini kote si kazi nzuri ya CCM ila ni kazi nzuri ya JPM(Sijui atanielewa???)
 
Back
Top Bottom