Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,608
- 1,743
Yaani amini usiamini Qurani haikubakisa kitu ,nilipoisikia habari ya mafisadi ,nilijaribu kusoma soma na kutafuta kama kuna ukweli wowote wa haya yaliibuliwa ndani ya Tanzania kuhusu wabadhirifu wa mali na wenye kufisidi hazina ya Tanzania.
Katika Qurani kumetajwa watu wajulikanao Majuju natumai hata kwenye bibilia wamo ,mwenye ukumbusho anaweza kutuletea.
Hawa Majuju ni watu wanaoharibu na kufisidi kila kilicho mbele yao na inasemekana wataonekana na kuja karibu wa mwisho wa dunia na kwa vile dalili zakufikia mwisho wa dunia katika Uislamu zimeanza kuonekana naona hapa Tanzania tayari wameshafika ,maana hakuna wizara unayoigusa usione imemegwa na kuliwa ,ukienda kwenye ardhi na maliasili utaona wameanza kula na kubakiza mashimo inasemekana hawa Majuju wanakula hata mawe ,na ukitazama madini ni mawe na kula kwa lugha ya kileo ni kuiba hivyo imefiti hapo ,ukienda kwenye misitu halikadhalika utaona magogo na miti yote wanakula ,si ndio hapo kwenye biashara ya magogo Majuju wamepita ,na ukiangalia kule baharini ndio usiseme ,hawa jamaa wameifisidi nchi yote na kama wanavyosema yatabaki mashimo na jangwa tu ,Chama Cha Majuju.
Wiki endi njema.