CCM wamewasaliti Watanzania, wanastahili lawama zote

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
CCM waliwaahidi watanzania kwamba wamewaletea mgombea bora atakayeipeleka nchi katika mapinduzi ya uchumi wa viwanda, cha ajabu mpaka sasa hakuna dalili zozote za mapinduzi pamoja na kuelekea kumaplizika kwa nusu ya kwanza ya awamu ya tano.


Uthibitisho ni wasiwasi wa hata uhakika kupatikana kwa huduma za jamii kama umeme,maji,Madawa na miundo mbinu ya kutosha kutokana ukosefu wa fedha zilizotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo,kila moja ni shahidi kua iliidhinishwa bajeti ya shilingi za kitanzania trillion 11.3 ambapo mpaka sasa zimepatika trillion 3.9 sawa sawa na 34%. Hii inaleta tabu kidogo hasa kuelekea kwenye mwaka mpya wa bajeti ikiwa hata nusu tu ya bajeti iliyopita haijafikiwa.


CCM walikosea sana kuwapa Watanzania matumaini hewa ambayo hivi sasa yamefifia kwa kiasi kikubwa sana kutokana na wananchi kuanza kuitupia lawama serikali kwa hali mbaya ya uchumi ilivyo hivi sasa, kila kilicho kibovu hivi sasa lawama zinaelekezwa kwa serikali kushindwa kuwamudu kuwahudumia.Watu wanaishi kwa kutozifahamu kesho zao kukosa matumaini.


Niseme tu kwamba kuibuka kwa makundi mbalimbali ya watu wanaoikosoa serikali wakiwemo wasanii wa miziki kwa nyimbo zao, asasi za kiraia na vyama vya siasa ni dalili tosha kwamba tunakoelekea hakuna ayefahamu.Lawama zote ni lazima wabebe CCM kwa sababu walikua na uwezo wa kuweka viongozi watakaothubutu badili taifa kama walivyoahidi.


Hakuna asiyetambua kua tatizo kubwa ambalo ni kosa la kiufundi kwenye mambo haya ni Ukosefu wa vipaumbele vya taifa ambavyo vilipaswa kuidhinishiwa bajeti na bunge la jamhuri ya muungano, badala yake imekua ikiibuka miradi ambayo haiwepo kwenye bajeti mfano mdogo tu kuhamisha makao makuu ya nchi mkoani Dodoma mradi ambao unatumia sehemu kubwa ya bajeti ya nchi kukamilisha miundombinu yake pamoja na kutotengewa bajeti na bunge.


Ni bora tu CCM kuliko kuendelea kuwapotosha watanzania, waseme ukweli kua wameshindwa kabisa kulifikisha taifa kule ambapo wengi walitarajia,Wawachie watu wenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya na wananchi wakafurahia matunda ya taifa lao kuliko d"Drama" hizi ambazo hazieleweki kama alivyosema msanii Ney wa mitego kua kazi yao ni kugombea "Front pages" tu.
 
Familia zao zinakula na kutibiwa vizuri, ndio maana hawajui msalaba waliobeba wananchi. Takwimu zimejieleza vizuri tu, na pia maisha ya watanzania ni kielelezo tosha. Katika maadui watatu aliowataja Nyerere tuongeze wa nne, CCM.
 
Back
Top Bottom