CCM wametuma vijana kununua shahada za kupigia kura za wanachuo Tumaini Makumira Univ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wametuma vijana kununua shahada za kupigia kura za wanachuo Tumaini Makumira Univ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinganola, Mar 19, 2012.

 1. kinganola

  kinganola Senior Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huwezi amini lakini hili suala linaukweli asilimia 100%,wawakilishi wa ccm hapa chuoni na majina nitayatoa kesho mara baada ya mikakati ya kuwatia nguvuni kukamilika.haijulikani wamepewa tshs ngapi na watanunua kadi moja kwa tshs ngapi.Kazi kubwa waliokuwa wakiifanya leo ni kujaribu kupata idadi ya wanafunzi waliojiandikisha kupiga kura kituo cha makumira.
  Nawasilisha...
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nyie ni wasomi kama mtakubali kununuliwa kwa hela haramu shauri yenu ila kumbukeni ONE MISTAKE 2 GOALS
   
 3. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani wasomi ! Tz is onto the tips of your fingers! Ok. Yangu 'majicho'
   
 4. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siamini kama msomi wa chuo kikuu anaweza kuuza kadi yake ya kupigia kura!!! ikitokea hivyo basi taifa limekwisha!
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwanini na wewe unafichaficha kusema ukweli wote? Msomi anatakiwa kuwa role model ktk jamii. Labda hao wa Makumira ni madafu, vichwa vyao vimejaa maji tupu.
   
 6. v

  valid statement JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  One mistake SEVERAL GOALS.
   
 7. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ikitokea msomi wa chuo kikuu tena amkumira ameuza kkadi ya kura ujue ...tumekwisha hatuna taifa.mwenye kudhulumu aendelee kudhulumu na hata mwenye kutenda dhambi na aendelee hivyo hivyo...MAKUMUIRA ACHENI KUTUAIBISHA VIJANA WA TZ.....USE YOUR COMMON SENSE....
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Watakuwa form two hao wakiuza shahada,sitakuwa na imani na chuo hicho cha 2maini,naskilizia
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu mbona unatoa habari prematurely? Unasema utatoa majina yao baada ya mikakati ya kuwatia nguvuni kukamilika kwa hiyo unadhani kabisa kwamba wao ama waliowatuma hawatembelei mtandao huu? Ungesubiri hadi uwatie nguvuni basi ungekuja na thread iliyokamilika lakini hii inaonyesha kwamba huna mpango wa kuwatia nguvuni. Hii ni sawa na kusema nikamateni nisimpige adui yangu!
   
 10. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Sio kweli, hizi ni tetesi tu. Ingekuwa kweli ungeleta habari kamili pamoja na hao wanaonunua shahada. Kwa nini unatuambia tusubiri hadi kesho, we kwa ni nini usingesubiri hadi hiyo kesho ukapata full data kisha ukaleta hapa?
   
 11. kinganola

  kinganola Senior Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wametumwa kutafuta kadi,tunajua hakuna msomi atakaye uza kasi yake labda awe mnywa gongo,kitakachofanyika hapa ni kuwawekea mtego,kadi watapata ila punde kitawanukia na hawata amini...
  Unajua shida iliyopo hapa kuna vijana ni makada wa ccm na wamesha itwa kwenye vikao na kukabidhiwa fedha na majukumu...
  Njaa mbaya na usidhani kila mwana University ni mwanamapinduzi,kuna wanafiki huku kama kawaida...
   
 12. D

  Dawa ya Mjinga JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 382
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Someni hii elimu ya uchaguzi kutoka kwa mwalimu kwa mfumo wa shairi.

  Mafisadi hakuna kuwachagua

  Nikiwa Mtanzania, wajibu nauchukua,
  Elimu takupatia, ni wewe utaamua,
  Moyo ulojaa nia, hatua bora chukua,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Waja na nyingi ahadi, tena zisizo mashiko,
  Wale wote mafisadi, watapata mishtuko,
  Kama utajitahidi, kutumia kura yako,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Ustawi wa taifa, upo mikononi mwako,
  Watalihodhi taifa, kiuza shahada yako,
  Nawe tapoteza sifa, iliyo halali kwako,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Wanayo mingi misemo, kuonyesha wanaweza,
  Uongozi si mdomo, kama matendo vilaza,
  Mwaka huu ni kikomo, chali wote twawalaza,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Ni bora wakae kando, sheria iwatafune,
  Hodari kula magendo, na jela wakaione,
  Tusije legeza mwendo, lazima watafutane,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Uongozi sio pesa, kama wanavyo dhania,
  Nyerere mfano hasa, ni mengi katufanyia,
  Porojo za kisiasa, ndizo wamengÂ’angÂ’ania,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Twataka maendeleo, na sio porojo zao,
  Heshima na utu leo, si hoja vichwani mwao,
  Nchi pasi mwelekeo, walinda rafiki zao,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Si kwa dini wala rangi, tutapata viongozi,
  Ukabila si msingi, kupata wachapakazi,
  Rafiki wasiku nyingi, si hoja kumpa kazi,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Kisa eti ni Mkara, kura hutompatia,
  Dhambi ilo tia fora, ndugu yangu wajitia,
  Taifa takosa dira, vizazi vitajutia,
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Na viongozi wa dini, shime nanyi nawatia,
  Elimu safi makini, waumini kuwambia,
  Kwani hata wapagani, waweza onyesha njia.
  Mafisadi twawajua, hakuna kuwachagua.

  Mwalimu Theophil P. Mlungwa
   
 13. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wachukue pesa halafu wasitoe kadi, kwani hizo ni pesa walizodhurumiwa muda mrefu
   
 14. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viva cdm
   
 15. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sishangai kusikia WASOMAJI wa makumira kununuliwa,hivyo ni vyuo vya kata kama udom,vina wasomaji si wasomi,so si k2 cha ajabu.Hata siku moja intelectual hawezi kushabkia ccm
   
 16. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  kama chuo watauza shahada zao basi vijijini ni maangamizi.
   
 17. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,111
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180

  Wapokee pesa na kutoa ahadi ya maneno kuwa wataipigia ccm. Lakini wasitoe kadi zao kwani kadi ndio utaifa wako, Pokea pesa kwani ni kodi ya wazee,kaka,dada zako ni haki yako kuiula ila msitoe kadi ya kupigia kura. Hapo ndio tutajua kuwa wasomi wako juu sio wa kudanganywa kwa shibe ya siku moja. Kula ccm kura cdm
   
 18. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Machalii wa CHADEMA wao wanawaibia mababu zao na mabibi zao shahada za kupiga kura.
   
 19. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huo Ujambazi ulijaribiwa na Masha SAUT 2010, lakini akambulia aibu.

  I will BET MY NECK mwanafunzi wa CHUO KIKUU hata akiwa Magamba hawezi kuuza kadi yake ya KURA ASILANI. Unless huyo MWANAFUNZI NI WA CHOO KIKUU!
   
 20. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  hebu punguza uongo mjukuu wangu.nijuavyo wanafunzi sio permanent residents wa eneo hilo kwani kila mwaka hugraduate.sasa tukichukulia mara ya mwisho ku update daftari la wapiga kura utaona kuna wanafunzi wachache sana waliobaki kama wapiga kura halali eneo hilo.sanasana ni wale waliokuwa first year mwaka 2010 ambao sasa wako mwaka wa tatu(final year)

  wazembe wa chadema watahangaika sana kutafuta hivyo vikura vichache vya wanafunzi wa mwaka watatu wakati ccm wamejitosa vijijini kuhakikisha kura kumi kwa kila nyumba kumi zinapatikana.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
Loading...