CCM wameshinda zaidi ya vijiji 250 kwa ulaghai na uzembe wetu

DCONSCIOUS

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,269
1,500
Jumla ya vijiji 150 ccm imepita bila kupingwa kwa hila zao lakini pia kwa uzembe wa baadhi ya viongozi wetu. tunaomba chama kitoe tamko katika hili kwani inakatisha tamaa sana.
 
Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,617
2,000
Mkuu

Inawezekana ushauri wako ni mzuri sana na unatekelezeka. Lakini kama uko katika maeneo ambako hila na uzembe umefanyika na kuipatia ushindi CCM na kukikosesha ushindi 'chama chako' utakuwa hauwatendei haki unaotaka watoe tamko endapo haufafanui hila na uzembe au hautoi taarifa iliyokamilika!

Hata haujasema ni wapi huko!

Kwa sababu ziko hila nyingi Sana hasa kupitia fomu zilizowekwa kimtegomtego (ambiguity) au hila za makusudi tu...

Kwa sababu nakuelewa hapa, basi tunaweza kuwasiliana;

0712 260 280
 
GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,039
2,000
Ni vizuri ukaleta taarifa iliyokamilika mkuu,, ni wapi huko? Imekuaje mpaka ccm wapite bila kupingwa vijiji/mitaa yote hiyo?
Weka taarifa iliyokamilika tafadhali
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Kuna uzi unasema katibu wa jimbo alikataa kutumia mhuri sahihi wa chama na kuamua kutumia mhuri wake binafsi.
Kwa kufanya hivyo amesababisha kuenguliwa kwa wagombea wote same mjini.
Tunaomba mfuatilie ili kama kuna ushenzi huo,awajibishwe mara moja.
Mkuu

Inawezekana ushauri wako ni mzuri sana na unatekelezeka. Lakini kama uko katika maeneo ambako hila na uzembe umefanyika na kuipatia ushindi CCM na kukikosesha ushindi 'chama chako' utakuwa hauwatendei haki unaotaka watoe tamko endapo haufafanui hila na uzembe au hautoi taarifa iliyokamilika!

Hata haujasema ni wapi huko!

Kwa sababu ziko hila nyingi Sana hasa kupitia fomu zilizowekwa kimtegomtego (ambiguity) au hila za makusudi tu...

Kwa sababu nakuelewa hapa, basi tunaweza kuwasiliana;

0712 260 280
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,044
2,000
Jumla ya vijiji 150 ccm imepita bila kupingwa kwa hila zao lakini pia kwa uzembe wa baadhi ya viongozi wetu. tunaomba chama kitoe tamko katika hili kwani inakatisha tamaa sana.
Watu muhimu kwa kazi wameenda kutalii bunge la ulaya..wengine wanapiga posho operation delete ccm..utapata stroke mkuu
 
GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,039
2,000
Kuna uzi unasema katibu wa jimbo alikataa kutumia mhuri sahihi wa chama na kuamua kutumia mhuri wake binafsi.
Kwa kufanya hivyo amesababisha kuenguliwa kwa wagombea wote same mjini.
Tunaomba mfuatilie ili kama kuna ushenzi huo,awajibishwe mara moja.

Tumaini Makene..... Tafadhali litoleeni ufafanuzi hili la Same maana limevuma sana huku JF,, bila shaka hapo makao makuu mmeshalifuatilia tunaomba ufafanuzi tujue kama kuna ukweli au ni uzushi tu
 
rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,900
2,000
Jumla ya vijiji 150 ccm imepita bila kupingwa kwa hila zao lakini pia kwa uzembe wa baadhi ya viongozi wetu. tunaomba chama kitoe tamko katika hili kwani inakatisha tamaa sana.

wandugu hii kazi wanayofanya Chadema na vyama vya upinzani siyo nyepesi kwa jinsi mnavyofikiri,ebu chukulia mfano Chadema katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu,ebu angalia responsibilities zake zilivyo kubwa,nafikiri kabla hatujalaumu tuangalia na ugumu wa kazi yenyewe kiundani,kujenga upinzania imara miongoni mwa hao majambazi siyo kazi nyepesi,naomba tuvumiliane kila mtu afanye kadri awezavyo kuleta mabadiliko
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
54,227
2,000
Kuna uzi unasema katibu wa jimbo alikataa kutumia mhuri sahihi wa chama na kuamua kutumia mhuri wake binafsi.
Kwa kufanya hivyo amesababisha kuenguliwa kwa wagombea wote same mjini.
Tunaomba mfuatilie ili kama kuna ushenzi huo,awajibishwe mara moja.

Aisee...duuh
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,044
2,000
Mkuu

Inawezekana ushauri wako ni mzuri sana na unatekelezeka. Lakini kama uko katika maeneo ambako hila na uzembe umefanyika na kuipatia ushindi CCM na kukikosesha ushindi 'chama chako' utakuwa hauwatendei haki unaotaka watoe tamko endapo haufafanui hila na uzembe au hautoi taarifa iliyokamilika!

Hata haujasema ni wapi huko!

Kwa sababu ziko hila nyingi Sana hasa kupitia fomu zilizowekwa kimtegomtego (ambiguity) au hila za makusudi tu...

Kwa sababu nakuelewa hapa, basi tunaweza kuwasiliana;

0712 260 280
Wacha porojo makene..hivi unajitokeza afisa mkubwa kama wewe unatoa madai mepesi kama haya? Fomu za kimtego mtego ndio zipi?,same vijiji 100 vimekwenda na maji shauri ya muhuri tu.mpo bize na matamko na posho za operation delete ccm mnasahai lama huu ndio uchaguzi mzito sana..yale ya chopa tatu kata tatu yanaanza mapema
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
1,225
Chadema kilianza na shetani kitamaliza na sheda ,

chama kilianzishwa kihuni na kinaendeshwa kihuni hata viongozi wake wahuni.
 
1701

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
861
500
Bado ndoto za 2015 zpo?acha presha kaka,hakuna kiongozi wa upinzan mwenye malengo ya kuitoa ccm
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
1,225
Mkuu

Inawezekana ushauri wako ni mzuri sana na unatekelezeka. Lakini kama uko katika maeneo ambako hila na uzembe umefanyika na kuipatia ushindi CCM na kukikosesha ushindi 'chama chako' utakuwa hauwatendei haki unaotaka watoe tamko endapo haufafanui hila na uzembe au hautoi taarifa iliyokamilika!

Hata haujasema ni wapi huko!

Kwa sababu ziko hila nyingi Sana hasa kupitia fomu zilizowekwa kimtegomtego (ambiguity) au hila za makusudi tu...

Kwa sababu nakuelewa hapa, basi tunaweza kuwasiliana;

0712 260 280
Hivi we makene unaakili kweli eti fomu za mitego kwahiyo nyie chadema mkitegwa lazima mnase tatizo lenu mnawaza namna ya kugawana posho za makao makuu tu mengine hamnashida nayo ngoja kiama kiwashukie.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,044
2,000
wandugu hii kazi wanayofanya Chadema na vyama vya upinzani siyo nyepesi kwa jinsi mnavyofikiri,ebu chukulia mfano Chadema katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu,ebu angalia responsibilities zake zilivyo kubwa,nafikiri kabla hatujalaumu utuangalia na ugumu wa kazi yenyewe kiundani,kujenga upinzania imara miongoni mwa hao majambazi siyo kazi nyepesi,naomba tuvumiliane kila mtu afanye kadri awezavyo kuleta mabadiliko

Unaanza utetezi mapema.katibu mkuu ana manaibu wawili.mmoja yupo ziarani ulaya katika kipindi hiki kigumu utamtuma vipi afisa mkubwa kama mwalimu.pia sekretariet yote imetawanyika kuambatana na operation delete ccm..chadema hawapo makini kama tudhaniavyo
 
NGANU

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
1,919
1,500
Suala la mhuli limeikumba pia halmashauri ya wilaya ya MEATU mkoani simiyu japo uamuzi wa pingamizi haujatolewa hadi leo,
huku viongozi watatu wakisota lupango huko maswa.
 
Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,529
2,000
Naanza kusikia halafu ya anguko la upinzani 2015.Kama wanakosa umakini ktk kujazo form, unategemea nini, kwa kweli inaudhi sana, njama za ccm zinajulikana lakini viongozi hawako vigilant ktk kushughulikia.Kujaza form pekee inachukua about 60% ya ushindi na 40% inapatikana kwenye kampeni na majukwaani. CDM rudini darasani mjifunze kupambana na ccm otherwise ni ugonjwa wa moyo.Ndiyo maana ccm wanajiandaa kuunda serikali 2015 kwani wanajua hawana mpinzani makini.
Wapinzani hasa viongozi lazima wabaini kwa umakini njama za ccm mapema

Nakumbuka Mh.Mbowe aliwahi kusema kuwa form zina matatizo ya kiufundi, je walifanyia kazi mapungufu hayo?? au waliishia kusema kwenye press??? sheeeda sana kushabikia upinzani.
Tulitegemea walichukua all the necessary precautions.
Haingii akilini eti kisa mhuri!!!!! kwani ofisi tulizoambiwa zimejengewa uwezo ni uwezo gani!!!

Be watchful CCM wako makini hawatishiwi mikutano mingi, they seem to be strategical than any. INAUMA SANA
 
reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,202
2,000
Mkuu

Inawezekana ushauri wako ni mzuri sana na unatekelezeka. Lakini kama uko katika maeneo ambako hila na uzembe umefanyika na kuipatia ushindi CCM na kukikosesha ushindi 'chama chako' utakuwa hauwatendei haki unaotaka watoe tamko endapo haufafanui hila na uzembe au hautoi taarifa iliyokamilika!

Hata haujasema ni wapi huko!

Kwa sababu ziko hila nyingi Sana hasa kupitia fomu zilizowekwa kimtegomtego (ambiguity) au hila za makusudi tu...

Kwa sababu nakuelewa hapa, basi tunaweza kuwasiliana;

0712 260 280
Ina maana hiyo mitego mitego mnanasa nyinyi tu, au? Hoja ya msingi hapo ni uzembe wa viongozi wenu; PERIOD!
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,902
2,000
mtoa mada amelenga chama gani kitoe tamko? Maana naona akina tumaini makene wanatokwa na mapovu tu as if wameambiwa wao
 
reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,202
2,000
wandugu hii kazi wanayofanya Chadema na vyama vya upinzani siyo nyepesi kwa jinsi mnavyofikiri,ebu chukulia mfano Chadema katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu,ebu angalia responsibilities zake zilivyo kubwa,nafikiri kabla hatujalaumu tuangalia na ugumu wa kazi yenyewe kiundani,kujenga upinzania imara miongoni mwa hao majambazi siyo kazi nyepesi,naomba tuvumiliane kila mtu afanye kadri awezavyo kuleta mabadiliko
Kwani kazi zote hadi chini anatakiwa kufanya Slaa? Hana wasaidizi? Si kuna makatibu wa mikoa ambao anaweza kuwasiliana nao? Hao makatibu wa mikoa si wanao makatibu wa wilaya? Hao wa wilaya si wana wasaidizi wao hadi kwenye ngazi za tarafa? Hao wa tarafa si wana wasaidizi wao hadi ngazi za kata? Hao wa kata si kuna walio chini yao hadi ngazi za vijiji? Hao wa vijiji si kuna walio chni yao hadi kwenye ngazi za vitongoji na mitaa? Flow of information inatakiwa ku-flow that way kinyume chake ni uzembe tu kwahiyo acheni CCM wafaidike na uzembe wenu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom