CCM wameshaivuruga nchi - TAHADHARI

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,921
3,801
Kwa kweli namna katiba inavyovurugwa ni wazi kabisa Chama cha Mapinduzi kimeshaivuruga nchi na sasa, na sasa kila mmoja anaongoza kivyakevyake, msemo wa Kiswahili maarufu ule usemao mwenye nguvu mpishe, ndio tunaokwenda nao sio tena kufuata ule msemo wa Uongozi ni dhamana.

Mnavuruga Katiba ya nchi halafu mnaonekana hamjali kabisa, mnaonyesha kiburi waziwazi.

Mtiririko huu unaanthiri nyanja zote za utendaji kazi serikalini maana mahakama haki itapotea watafanya na kuamua wanavyotaka, polisi nao watafanya wanavyotaka kwani CCM hawezi kuwakemea tena polisi sababu polisi ndio walinzi wa masanduku ya kura za wizi na walazimishaji wa kuwaondoa mawakala, majeshi watafanya wanavyotaka maana na wao ndio wanaolinda misafara ya viongozi wa serikali ya CCM na unaweza kuona muendelezo huo kama hayo ya mabenki kuchotwa hela yote ni mataputapu yanayosababishwa na uvunjwaji wa katiba. Spika wa bunge naye anafanya anavyotaka kila kitu kinaonekana kimevugwa.

Huwa nikikaa nawaza na kujisemea pamoja na kujiuliza. Je, Tanzania tunaelekea kuwa kama zile nchi zenye mapigano yasiokwisha kwa kweli ninakuwa na masuali mengi ya kuona tunaondoka taratibu kwenye lile hekalu la amani na utulivu.

Kuna tabu gani ya kufuata Katiba na kila mmoja akafanya wajibu wake kutoka katika miongozo iliyomo ndani ya Katiba na yakitokea malalamiko wananchi wanalalamika Katiba imevunjwa ni wajibu wa serikali kujitokeza haraka kuivunja hoja hio kwa miongozo inayoeleweka na sio majibu ya papo kwa papo.

Kuna watu wanasema Rais Samia amevunja au anavunja katika kwani mawaziri waliopo hawakula kiapo kwake yeye ni Rais mpya kama atateua wapya au walewale basi awatayarishie siku awaapishe.

Kama Tanzania tuiweke kwenye umbo la meli basi naona kama kamba ya nanga inaelekea kukatika.
 
Hapo Babati penye jina lako kuna ujinga mwingi unaendelea kituo cha polisi. OC CID yupo bize kuwabandika kesi watuhumiwa mbalimbali kisha anadai pesa ndefu ili kuruhusu dhamana zao.
Pole mkuu, ulipata lini hiyo changamoto? japo kwa sasa sipo Babati ni Landanai Simanjiro kitambo sn
 
Ndiyo nipo hapa mkuu tangu 2018 baada ya serikali dhalimu ya CCM kutunyima ajira but ukiona nachati hivi ujue nipo karibu na mnara wa CM siyo sehemu zote zina network.
Sawa ndugu, huko utatoboa vizuri tu maana mazao yanakubali huko. Biashara na ajira katika zama hizi hazilipi, labda uamue kula haramu kama huyo OC CID
 
Sawa ndugu, huko utatoboa vizuri tu maana mazao yanakubali huko. Biashara na ajira katika zama hizi hazilipi, labda uamue kula haramu kama huyo OC CID
Umekutana naye lini mkuu? Babati huwa nakuja kuja japo siyo kivile ni mara chache chache nina washikaji kibao hapo, pia kitu kinaitwa ajira sitaki tena labda nipate UN.
 
Ni kweli watu wengi wanahitaji katiba mpya au ni wewe na wenzako wachache?
Nina amini mngekuwa wengi katiba mpya ingepatikana
JK alianzisha hakuwa na akili? mpuuzi wewe mchakato ukianza hapa sasahivi utaanza kushabikia kijinga kuwa serikali sikivu siju ukoko gani
 
Mimi sitaki kupanua domo langu kwanza kwa huyu mama.Nina matumaini nae yule hayati ndie alietimua nchi ikawa serikali yake ni kinala wa kufanya uhuni,umafia,ukatili kwa raia na wageni kwa kutaka sifa.Mama Samia tunakuomba ule uhuni wa hayati kwenye kuiendesha nchi usiuendeleze WATANZANIA WAPO HOI WAMECHOKA SANA.
 
Umekutana naye lini mkuu? Babati huwa nakuja kuja japo siyo kivile ni mara chache chache nina washikaji kibao hapo, pia kitu kinaitwa ajira sitaki tena labda nipate UN.
Nimeachana naye juzi aise, nitakuja kwenye agriculture, natumaini utakuwa mwenyeji wangu
 
Kwa maana hio watu waache viherehere, wataapishwa ? Na kama hawakuapishwa mtafanya nini ?
Kila mwenye kijinafasi kidogo tu anatutambua wananchi wa Tz ni piga tajame
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom