Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Kwenye bunge lililopita yapo mashirika, na taasisi za umma nyingi yaliandikiwa ripoti nzuri na kamati za bunge(beautiful reports),yalitajwa kama mashirika ya kupigiwa mfano,yalipigiwa chepuo kuwa ni ya mfano,lakini leo kila kukicha tunaambiwa huko kuna madudu pia!.
Gazeti la Mwananchi la leo,limeandika "NSSF YALIWA MCHANA KWEUPE",hili ni shirika ambalo kamati ya kudumu ya bunge ya mashirika ya umma ililitaja mara kwa mara kama mfano wa kuigwa,jana ilitajwa mradi wa ujenzi wa mji wa Kigamboni una harufu ya rushwa ya Bilioni 179,leo tena tunaambiwa huko watu wanakula mchana kweupe.
Nao TCRA wametajwa kuwa walitumia bilioni 18 kwa ajili ya semina na warsha*(mwananchi :April 9.2016)!.Yaonekana hata kamati nyingi za bunge lililopita nazo zilikuwa dhaifu kama siyo walihusika na ulaji huu wa mchana mchana.