Uchaguzi 2020 CCM wamemwachia Magufuli fupa la Doto James na Mayanga Construction alitafune mwenyewe!

Kwameh

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,759
2,057
Doto James.JPG

Doto James, Bwana Malipo Mkuu wa serikali

Ni kaa la moto!

Hakuna mtu anaetaka kuligusa.

Wazungu wanaita "third rail," kwa sababu reli ina mitarimba mitatu: miwili inatambaa sambamba ardhini, yenyewe unaweza kuigusa, kuichezea na hata kuing'oa wakati wowote ili mradi treni halipiti na serikali haikuangalii. Mtarimba wa tatu wa reli unatembea hewani sambamba na ile mihimili ya ardhini, lakini mhimili huu umebeba umeme! Treni liwe linapita, treni halipiti, serikali wanakuangalia au hawakuoni, huthubutu kugusa huu waya muda wowote!

Kwa mara ya kwanza raia Tundu Lissu aligusa huu mtarimba, masaa mawili baadae akamwagiwa risasi 16 kena kena (point blank range)!

Ni mtarimba wa Doto James, mtoto wa dada yake Rais Magufuli ambae ni katibu mkuu Hazina aliyeteuliwa na mjomba wake akitokea Tanroads mkoani. Ndie Mtanzania peke yake ameiona na kuidhinisha mikataba ya manunuzi wa ndege, bwawa na rufiji, na reli ya SGR zaidi ya Rais Magufuli.

Majuzi kwenye kampeni, mgombea Urais, raia Lissu akiwa Mbarali, ameibua timbwili pacha lingine ambalo tulikuwa hatujawahi kulisikia: Aliyepewa zabuni ya kujenga airport Chato ni mme mwenza wa Rais Magufuli, Mayanga Construction. Na aliyeidhinisha hela ni mtoto wa dada, Doto James.

Mpaka sasa wameibuka makada wa CCM kujibu hoja za upinzani, Spika Ndugai, Mstaafu Makamba, Mwenezi Polepole, Msemaji Abbasi na wengine, lakini hakuna aliyethubutu kugusa waya wa Doto James wala Mayanga construction. Msemaji Abbasi kajaribu kusogelea suala la gharama za miradi kujulikana lakini hakusema mikataba iko wapi na nani kawahi kuiona zaidi ya Rais na Doto James ambae anasaini hundi za malipo. Sheria ya mikataba iliyosainiwa na Magufuli mwenyewe inataka mikataba iwe wazi kwa umma kupitia bunge.

Raia Lissu anasema Baba wa Taifa amekaa Ikulu miaka 24 hajawahi hata kufikiria kufanya manuva za kuweka ndugu zake wa damu kwenye nafasi nyeti ili wapitishe mahela ya kujenga airport kijijini kwake kama Mobutu Sese Seko, wala kuidhinisha miradi ya usiri.

Sasa makada wamemwachia Rais Magufuli apambane na hilo fupa alilorushiwa na raia Lissu. Wanaogopa kulikoroga zaidi, maana hawajui Rais JPM mwenyewe anafikiria nini. Wamezoea kuongea kwa kupata cues ( ishara) kutoka kwa Rais. Wanamuiga mpaka kuongea vilugha vyao kwenye halaiki za umma wenye makabila mengi, kitu kipya katika nchi. Lakini kwa hili la Doto James na Mayanga Construction Rais JPM kimywa! Makada hawajui cha kusema. JPM anaweza kulitafuna hilo fupa mwenyewe au ataendelea kuliacha limtafune yeye ?
 
Kwa lugha ya Mhe. Lissu, JPM ni Rais wa kwanza wa ajabu kumpata Tanzania. Yupo sahihi. Ni Rais wa ajabu mno. Uajabu wake ni kutofuata katiba, kutokuwa na busara wala hekima za kiuongozi, kuwa mbabe asiyeshaurika, mdhalilishaji wa hadharani, muonevu, mbadhilifu, nk. Hayo ya kina Doto James na Mayanga Constructions Ltd ni baadhi kati ya mengi yanayoleta kichefuchefu kinachoudhi sana. Tulikosea 2015. Huyu SIYO.
 
Huku kudhalilishwa hadharani kunawakera wengi. Wengine wameamua kumpa kura Lissu kwa kukosa kuthaminiwa utu wao. Unafika kazini kisa kuna mtu ana mamlaka juu yako anaweza kuongea na wewe kwa dharau, kejeli, majivuno na kwa ukali mbele ya wanaokuheshimu.
 
Mtu na mjomba wake.

Mjomba ni rais.

Kajomba ni katunza hazina.

Baba wa kajomba ndiye kapewa tenda.

Aiseeeeeeeeeee!

Mwaisaa mtu mbad kwani we unalisemeaje hili?
 
Hii kitu hovyo kabisa.. ila ccm wanafiki sana
Kwa lugha ya Mhe. Lissu, JPM ni Rais wa kwanza wa ajabu kumpata Tanzania. Yupo sahihi. Ni Rais wa ajabu mno. Uajabu wake ni kutofuata katiba, kutokuwa na busara wala hekima za kiuongozi, kuwa mbabe asiyeshaurika, mdhalilishaji wa hadharani, muonevu, mbadhilifu, nk. Hayo ya kina Doto James na Mayanga Constructions Ltd ni baadhi kati ya mengi yanayoleta kichefuchefu kinachoudhi sana. Tulikosea 2015. Huyu SIYO.
 
Mtu na mjomba wake.

Mjomba ni rais...
baba yake kajomba hajapewa tenda, nilivyoelewa mimi

Mama Jesca ana mdogo wake, ambae kaolewa na Mayanga Construction

kwa hiyo Mayanga na Magufuli wameoa nyumba moja

kwa hiyo hili ni pande la Mama Jeska

Mama Jeska anakaaga kimya kimya nyuma ya jukwaa kumbe mmmmmh.... Mama Sitti!

Inaonekana the last clean first lady was Maria Nyerere
 
baba yake kajomba hajapewa tenda, nilivyoelewa mimi...

Hapa ninaona Baba Jessica aliona opportunity kwa Mayanga Constructions na aliamua kuitumia. Haya ni maongezi ya wanaume wakati wanawake wakiwa jikoni.
 
H

apa ninaona Baba Jessica aliona opportunity kwa Mayanga Constructions na aliamua kuitumia. Haya ni maongezi ya wanaume wakati wanawake wakiwa jikoni.
anhaaa, kwa hiyo inawezekana hapa Mama Jessica hakuamua chochote... Okay, tunaweza kumpa benefit of the doubt Mama Jessica kwa sababu anaonekana ni mama wa kumwagilia maua sebuleni na wa jikoni kama ulivyosema.
 
Magumashi ana ubaguzi wa hali ya juu.
° Undugunaizesheni anaongoza yeye.
° Ukabila anaongoza yeye
° Ukanda anaongoza yeye
° Udini anaongoza yeye
° Kuvunja katiba anaongoza yeye
° Ukiukaji wa haki za binadamu anaongoza yeye.
Hata ndani ya chama chake wanamshangaa kwa jinsi asivyoshaurika
 
1600995565631.jpeg
 
baba yake kajomba hajapewa tenda, nilivyoelewa mimi

Mama Jesca ana mdogo wake, ambae kaolewa na Mayanga Construction...
Behind every successful man there is a strong woman. Ninakumbuka Robert Mugabe alianza kuonyesha tabia za ajabu baada ya mke wake wa kwanza Sally Mugabe kufariki. Wazimbabwe walisema kama Sally angekua hai angemshauri mzee astaafu na wangebaki na heshima kubwa kwenye jamii.
 
Magumashi ana ubaguzi wa hali ya juu.
° Undugunaizesheni anaongoza yeye.
° Ukabila anaongoza yeye
° Ukanda anaongoza yeye
° Udini anaongoza yeye
° Kuvunja katiba anaongoza yeye
° Ukiukaji wa haki za binadamu anaongoza yeye.
Hata ndani ya chama chake wanamshangaa kwa jinsi asivyoshaurika
PAMOJA NA HAYO APEWE MUDA MWINGINE TENA AMALIZIE KAZI
 
Atamalizia The Hague usijali
TUTATANGAZA USHINDI WETU MNONO NA HATA MKIANDAMANA HATUWAPIGI NGOO MTATEMBEA WEE MWISHONI MTALALA KIMYA LENGO LENU TUNALIJUA TUWAPIGE ILI MPATE CHANZO SASA TUMESTAHARABIKA CHOMBO CHETU NI CHA KISASA VIJANA WAMESOMA JUST LIKE SWITSERLAND
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom