TIQO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 13,787
- 2,078
Ni dhahiri shahili CCM kuelekea ukingoni mwa mwaka huu wamejipanga kwenye mitandao ya kijamii kupiga propaganda, ni kweli sasa hivi CCM inatumia vijana kwa vibibi kwenye mitandao ya kijamii kupiga propaganda na kupotosha umma, kwa hili naona wamefanikiwa kwa kiasi flani kufanya siasa kwenye mitandao ya kijamii kwani wametoa ajira kwa vijana na vibibi kushinda kwenye mitandao kufanya siasa na propaganda, lakini wanasahau kuwa Mtanzania wa kawaida anata maji safi, umeme wa uhakika, Elimu bora, Barabara vijijini zipitike muda wote, Bei za mazao zilidhishe, Huduma bora za afya n.k kwa hili CCM wamelala fofofo wao wamejikita kwenye propaganda wananchi wanataka maji safi wewe unakuja unawaambia CHADEMA chama cha ukanda, cha kidini, cha ukabira haya yanamsaidia nini mwananchi wa kawaida aliyevuna Kahawa yake Bukoba au aliye vuna Korosho yake Lindi na Mtwara je yatamsaidia bei kupanda?
Vijana wapenda mabadiliko ya kweli ni muda muafaka sasa wa kupambana na mkoloni mweusi ambae ni baba ako, mama ako, kaka ako, dada ako, bibi yako, babu yako, mjomba ako, shangazi yako ambaye analewa propaganda za CCM ili aendelee kumwachia mkoloni mweusi akifaidi keki ya taifa na familia yake na rafiki zake hili halikubaliki Taifa hili la Tanzania ni la waTanzania sote haijalishi wewe ni UDP, CCM, CHADEMA au CUF bila kujali kabila lako, dini yako, wala ukanda unao toka haki itendewe kwa wote.
CCM mmeajiri vijana kufanya siasa za maji taka kwenye mitandao ya kijamii lakini wananchi hawataki habari za Zitto awe mwenyekiti, Mbowe atolewe, Seif amenogewa na umakamu wa rais wananchi wanataka maendeleo mmewafanyia nini wananchi? Mpaka mjinasibu mwendelee kukaa madarakani?