CCM wameharibu CV ya Pinda, si yeye tena, anafuata anachoelekezwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wameharibu CV ya Pinda, si yeye tena, anafuata anachoelekezwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Jan 4, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Yaani kwa uadilifu aliokuwa nao Waziri Mkuu Pinda na imani ya Wananchi juu yake kwa sasa iko mashakani. Maana yeye kwa uadilifu wake akianzisha kitu anategemea watamuunga mkono kumbe loh! inakuja kauli tofauti na muelekeo wake na badala yake anarudi kuomba msamaha. Mfano alisema "Dowans ni genge la watu wachache" kitendo cha kuwaita genge maana yake alimaanisha si watu wazuri na wanastahili kuadhibiwa kwa kuwa ni wachache na hivyo serikali ingewamudu. Lakini sasa anasema " serikali inabidi iilipe Dowans" hakujua kuwa hilo genge wamo hata wakubwa zake. Hakujua kuwa hizo fedha huenda ndizo zitasaidia kuimarisha mkoa wake mpya wa Katavi, la sivyo itaendelea kuwa Wilaya ya Mpanda lo! Baba wa watu kaufyata. Hana maamuzi kuhusu masuala magumu na muhimu na nchi. Kakimbilia kwenye salary za walimu. Hapo ndo kaona atatokea. Lakini baadae watamuuliza "wewe unajua bifu la JK na watumishi" asije akaahidi ambacho hatatimiza. Ahhh, Pinda inabidi atoe kauli ambayo ikiwezekana ipingane na maovu yaliyopo serikalini ili aoneshe ushujaa wake vinginevyo, ataonekana ni YES MAN. Maadam alishasema yeye si Mroho wa mali bali maslahi ya nchi basi akemee maovu waziwazi. Vinginevyo baibai, ataishia kwenye rekodi isiyo na chochote kama walivyo kina Philip Mangula na wengineoooo. Ah CCM NI BALAA KWA KUHARIBU CV ZA WACHAPAKAZI. NGOJA TUONe KWA NEXT pRESIDENT MAGUFULI kama naye atachakachuliwa. Nawasilisha.

   

  Attached Files:

 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wadau mnasemaje au jamaa bado anaconfidence?
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa Mkulima, okoa CV yako mapema.

  Mzigo wa kuwatakasha MAFISADI walioiteka serikali ya CCM na taifa letu kwa ujumla ni zaidi ya mtu kujitwisha zima la misumari ya moto. Sote huku mitaani tunakuhurumia sana sana kwa hilo kama si kukushangaa mahangaiko yote hiyo.

  Ni kipindi cha kila mtu kuubeba msalaba hapo mtoto wa mkulima.
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Waswahili wanasema mtumike kafiri upate mkate wako!ndicho anachokifanya mheshimiwa pinda!!
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Kuna mama mmoja huko huko CCM alisema hakuna msafi katika wanaCCM, hakuna mtu msafi ndani ya CCM.
  Sasa kama hukumwamini ndio uyaone sasa.Ukiwa CCM kuchakachuliwa ni lazima.
  Na bado unataka Rais mwengine atoke CCM?
  Kweli CCM wameweza kutuzuga!! Karibu TZ.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  kesha chomekewa akili mpya mtoto wa mkulima sio yule aliyekuwa analia bungeni kwa uchungu na hutamwona akidondosha chozi kwa minajili ya kuwasaidia watanzania kachovya mkono wake kwenye asali na maziwa
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Ooh pinda why? "If you can't join them, fight them". Na pia "if you can't fight them, join them". Sasa ww hauko na mafisadi kwa nini usiwaadabishe wale unaoweza, maana madaraka unayo. Ukijitofautisha nao sisi wananchi ndio tutaokubeba inatakiwa utu please sisi siyo hao akina mkwere & co, kama alikuteua basi imekula kwake, onyesha nia yako dhabiti dhidi ya mafisadi maana ww uko kwenye mwanga lakini mafisadi wanafanya mambo yao gizani! Na toka lini penye mwanga, giza likawepo? Anza na kitu simple hebu tutajie hilo genge la watu wachache wanaomiliki dowans, mkwere hatokufanya kitu. Au unataka niamini msemo usemao "uoga ni umaskini"?
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Una maanisha kuwa mtoto wa mkulima ameshachakachuliwa akili? Kweli CCM noma.
   
 9. O

  Okinawa Senior Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mtoto wa Mkulima ulisema: "Dowans ni genge la watu wachache" kitendo cha kuwaita genge maana yake alimaanisha si watu wazuri na wanastahili kuadhibiwa kwa kuwa ni wachache na hivyo serikali ingewamudu. Lakini sasa anasema " serikali inabidi iilipe Dowans" hakujua kuwa hilo genge wamo hata wakubwa zake.

  Yani Genge la Wahuni halafu lilipwe bilioni 185 ya Wavuja Jasho wa Tanzania?

  Bora ungekataa kuwa Waziri Mkuu chini ya Utawala wa kifisadi wa Mkwere.

  Mbona ulikuwa umekataa lakini wakakushawishi ukakubali. Bora ungeendelea kukataa tu.

  Credibility yako kwa watanzania utaishusha sana.

  Lakini mjue kwamba hizi hela mkiwalipa Dowans (MAFISADI WA CCM) NCHI HAITAKALIKA. UTAZUKA MGOGORO AMBAO HAMTAWEZA KUUTULIZA. NA IKIANZA VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE MAFISADI HAWATAPONA !!!!!!!!!
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Alikuwa na akili tangu lini? mbona mnapaisha bure?
   
 11. N

  Nyota Njema Senior Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu si wa kuhangaika naye. Toka mwanzo wenye akili zetu zisizo za kushikiwa na mtu tulijua ni upatu uvumao tu. Pinda hana uwezo wa kufanya kazi ya uwaziri mkuu Tanzania hata kama kweli atakuwa ni mtu safi, hana uwezo full stop! Lowasa alikuwa na nguvu nguvu kidogo lakini tatizo lake lilikuwa ni wizi na tamaa.

  Wako wengi ndani ya hiyo CCM. Najiuliza kwa staili gani watatoka tena 2015! Watz tuamuke, hawa ni wachumia tumbo tu, hawana mapenzi ya kweli na wananchi.....Mwakyembe, Magufuli, Tibaijuka, Sita, sijui naninani vile hamna cha kutegemea pale.
   
 12. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  pinda hana jipya, ni very coward, anamuogopa mkwere na kamwe hawezi mpinga boss wake fisadi mkwere ambae kaweka pale na warabu akina rostam. Hawa jamaa tukiendelea kuwachekea watatukamua hadi tone la mwisho la damu zetu.
   
 13. joika

  joika Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh hii balaaa
   
 14. n

  ngoko JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maskini alisahau kuwa genge ndilo linaloamua nani awe Rais etc , hope alikumbushwa hilo .
   
 15. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,743
  Trophy Points: 280
  Una uhakika Pinda ni mwadilifu? Kuna ushahidi???
   
 16. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nilishasema No one swims in a muddy pond an get out of it clean!!!! Ukishakua ndani ya CCM wewe ni mchafu tu!!!!
   
 17. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Hivi alishajibu kuhusu hisa zake Sumry??
   
 18. N

  Nyota Njema Senior Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa comment hii, ni wachache wenye uelewa wanaolijua hilo. Hakuna msafi ndani ya chama hicho, wanashindana tu kuchumia matumbo yao.

  Siku ccm ikianguka kwenye uchaguzi wataikimbia wote. Siku hiyo inakuja, tusubiri kuliona hilo.
   
 19. T

  The Future. Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pinda tayari kesha kazi, sio yule ninae mjua.
   
 20. m

  mpingomkavu Member

  #20
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pinda hakuna anachokifanya bora angejipumzikia kwao mpanda akaendelea na kilimo kwani uwaziri mkuu hauwezi anabaki kulia na kulalama hovyo tu.
   
Loading...