CCM wamechoka, Kuchukua kodi kwenye pesa za matumizi kwa mwananchi ni kosa, kodi huchukuliwa kwenye faida

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,943
28,384
Formula ya kodi dunia nzima ni kwamba kodi huchukuliwa na serikali kutoka kwenye jumla ya faida kwenye kitu mwananchi anachofanya au faida unayopata ndio wanatakiwa wachukue kodi yao.

Sasa hawa jamaa washajichokea au sijui ni uchumi upi wanesoma wao pesa ya matumizi ya mwananchi serikali haina haki ya kuigusa tena wanatakiwa wakae mbali nayo.

Kwa mfano unaweza kushindwa kutuma pesa ya matibabu kwa sababu makato yako juu hivo mgonjwa akasumbuka, kwenye daily consumption CCM walitakiwa kukaa mbali kabisa na huo mfumo.

Ndio mbinu za kuongeza tax base ziko nyingi sana lakini hawana hata namna ya kufikiri kabisa wamebaki wanaongoza nchi kwa kubabiabia leo hili kesho lile hawana hoja kabisa na wameishiwa maarifa.
 
Back
Top Bottom