CCM Wameanza kupiga kura Jana Usiku Kwenye Kata ya Kigogo

Msamiati

R I P
Mar 6, 2011
1,072
0
Juzi jamaa yangu mmoja aliniambia kuwa Alikutana na kikundi cha wazee kama watatu hivi wakiwa na makaratasi ya kupigia kura wanapigisha watu na wengine wanawapa hela kati ya 3000 na 5000. Mimi sikumuamini kabisa maneno yake lakini kilichotokea jana mpaka sasa sielewi.

Nimewaona wazee wa CCM walikua 6, Wawili nawafahamu kabisha ni watu maarufu sana kwenye maeneo yetu, walikuwa pamoja na mgombea wa nafasi ya mwenye kiti, walichokuwa wanafanya walikuwa wanaingia kwenye nyumba za wajumbe wa nyumba kumi, kisha wajumbe wana waita baadhi ya wakazi halafu wanawapigisha kura.

Mimi nilikuwa nimekaa pembeni kidogo kwenye kiduka, karibu kabisa na nyumba ya mjumbe wa nyumba kumi, wakafika eneo hilo na kuendeleza hako kamchezo, Mmoja woa ambaye ni mtu maarufu sana anaitwa hamisi akawa anazuga kana kwamba anabandika vitangazo vya kampeni. Akanisalimia na kubandika hicho kitangazo.

Baada ya hapo, nikajaribu kufatilia movement zao nikaona wanaingia kwenye nyumba za wajumbe wa nyumba kumi, kisha kilichokuwa kinafanyika, wajumbe wanawaitia watu ambao wanajua hawana misimamo mikali.

Warning: Uchaguzi wa mwaka huu una Joto kubwa sana, utakuwa tofauti na chaguzi za miaka yote, uhuni wa aina hii si uungwana kabisa, unaweza kuleta machafuko yasiyokuwa ya lazima. Naomba Wanaharakati mlifatilie hili ili lisije likageuza nchi yetu kuwa kisiwa cha umwagaji Damu.

Kwa yoyote atakae hitaji msaada wa kufatilia mimi namjua moja ya wajumbe waliofanyishwa mchezo huu kwa malipo ya tsh 10,000. Lakini huwa hakubaliani kabisa na Ufedhuri huu, naweza kuwaunganisha nae akawapa siri zote.

CC: Lucci Dotto Mnzava figganigga
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,111
2,000
Ulipo ona hivyo umechukua hatua gani au ndio kustaki hapa JF?
Wataarifa washika dau wa eneo husika ili wachukue hatua mapema.
 

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,832
2,000
kwann hukwenda polisi au kuita waandishi wa habari.kweli kichwa cha kuku hakivishwi kilemba
 

naxon

JF-Expert Member
Dec 6, 2014
342
250
Chamsingi ni kuwapa taarifa watu wa eneo husika wanaoweza kulitatua hususani wapinzani nadhani watalishughulikia kama una evidence.
 

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,222
1,225
Hivi kwenye matukio hayo kupiga picha hata kwa siri huwa shida eeh? Mbona matukio mengine twapiga sana mipicha!!!
 

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,393
1,225
JK na ccm ni wezi sana
katika maraisi wote ukanda wa africa mashariki hakuna raisi alie haribu nchi yake kama jakaya kikwete nchi imekuwa kama haina kiongozi inaendeshwa kuhuni huni kuanzia ikulu hadi kwa mabalozi wa nyumba kumi
 

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,393
1,225
kwann hukwenda polisi au kuita waandishi wa habari.kweli kichwa cha kuku hakivishwi kilemba
polisi kufanya nini wakati hao polisi ni mawakala wenu?? Huku nliko kuna mzee mmoja na vijana watatu wanachama watiifu wa chama cha kitapeli cha ccm wamelazwa hospitali mmoja katobolewa jicho, na huyu mwingine nasikia hajaamka tangu alipookolewa na polisi jana usiku kwa mambo hayo hayo ya kihuni yanayo fanywa na chama chako cha kitapeli hichoo
 

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,393
1,225
kwann hukwenda polisi au kuita waandishi wa habari.kweli kichwa cha kuku hakivishwi kilemba
polisi kufanya nini wakati hao polisi ni mawakala wenu?? Huku nliko kuna mzee mmoja na vijana watatu wanachama watiifu wa chama cha kitapeli cha ccm wamelazwa hospitali mmoja katobolewa jicho, na huyu mwingine nasikia hajaamka tangu alipookolewa na polisi jana usiku kwa mambo hayo hayo ya kihuni yanayo fanywa na chama chako cha kitapeli hichoo.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
10,599
2,000
mwenye nazo namba/simu za waandishi wa habari ambao ni sharp shooter aziwe humu ZIWE MSAADA KWA WOTE WATAKAO~SHUHUDIA #NDIVYO_SIVYO POPOTE PALE HATA WA HUKO MIKOANI ZIANIKWE wasalaamu
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Hongera kwa kufichua mbinu hiyo mbovu, hakikisha unawashirikisha viongozi wa ukawa wa eneo hilo. Ccm kwa wizi wanatisha!
 

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,720
2,000
kwann hukwenda polisi au kuita waandishi wa habari.kweli kichwa cha kuku hakivishwi kilemba
Hivi polisi ndio wa kuwaamini,kesi ya ngedere unapeleka kwa tumbili,kwanza mimi nona huu uchaguzi ni batili kwanza unamaliza hela bure ,chaguzi zote zinatakiwa zisimammiwe na tume ya uchaguzi na si ofisi ya Pinda/Ghasia.Wangesubiri tu uchaguzi mkuu ili kupunguza gharama zakuwa na chaguzi mbili tofauti kwa pamoja .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom