CCM walitoa wapi pesa za kununua haya maeneo yote na majumba

wounded man

Senior Member
Feb 2, 2019
168
250
Sehemu yoyote ambayo ni potential basi kuna jengo moja au zaidi la CCM au kuna eneo kubwa la CCM, hapa namaanisha kila Tarafa au Kata basi kuna maeneo au kuna jengo la CCM, huwa najiuliza sana hiki chama tawala, chama kihenga Tanzania kilitoa wapi pesa ya kununua mali hizi zote

Kilifanya mradi gani mkubwa wa kupata pesa za kujiwekeza hivi, mbona hatujaambiwa kuwa wanachama washawahi kuchangia kwa ajili ya kufanya uwekezaji huu mkubwa waliofanya,

Mbona Serikali haijawahi kuweka document zozote hadharani za kuiuzia CCM mali hizi zote, kwa nini haijawahi kubinafsisha kwa yale maeneo ambayo hayaendelezwi ya ccm,

Kumbuka ccm inamagofu mengi sana katikati ya miji na inaharibu taswira ya miji na mijini,

Najua kuna wajuzi humu mtakuja kunipa majibu kuwa
1. CCM ilitoa wapi pesa ya kununua majengo haya yote?
2: ni lini serikali iliihuzia ccm mali hizi zote?
3: kwa nini zile ambazo haziendelezwi hazibinafsishwi miaka na miaka?

Nb
Sina chama ila nina mengi mapinduzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Shombe la Kisomali

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
4,310
2,000
Duuh, umewaza mbali sana kiongozi.. Yaan hawa CCM undefined, nipo tarafa hapa wana Block moja pesa kama zote, wanakodisha..
Yaan actually kila sehemu/kijiji wapo tena center
 

harder king

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
3,776
2,000
Ccm ni zaidi ya ukoloni!!!

kuna wilaya moja wamewanyang'nya halmashauri stand kuu ya mabasi na amna aliedhubutu kuliongelea hli swala popote na siku sio nyingi hii stend (haitumiki tena) itatambulika kama uwanja wa ccm japo hili eneo lilikuwepo mikononi mwa halmashauri tangia likiwa pori!

CCM NI ZAIDI YA WAKOLONI WALIONDOLEWA NA NYERERE!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,529
2,000
Ccm kama ccm haijawahi kununua chochote ccm imepora mali za umma kipindi chama kimoja kwa sasa ccm ni mufilisi kabisa bila kutoa misamaha yakodi katika sukari haipati kitu au kupora pesa BOT kagoda escrow haina kitu
 

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,123
2,000
Ccm haina jengo hata moja ambalo inalimiliki kwa halali. Majengo yote ya ccm zikiwemo shule,viwanja vya michezo kila mkoa,viwanja nk. Vyote vilikuwa Mali ya chama na serikali wakati wa mfumo wa chama kimoja. Mali zote hizo ni Kodi za watanzania wala si michango ya Kadi ya za ccm.

Tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992,ccm kwa vile walikuwa madarakani,waliamua kujimilikisha majengo,shule,viwanja nk. Ndo maana kuna vijiji unashangaa ccm wana ofisi lkn serikali haina ofisi...!! Jambo la kutia moyo ni kwamba, watanzania tunajua,siku ccm ikiondoka madarakani itakuwa ndo mwisho wa kumiliki hizo rasirimali. Na ccm haitakuja kurudi tena madarakani mpaka dunia inaondoka. Ni km ilivyotokea kwa KANU ya Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,640
2,000
Wakati wa utawala wa chama kimoja. Ilikuwa hamna tofauti ya chama na serikali.

Watumishi walihamishwa toka sehemu moja kwenda nyingine. Wakati wa kofia mbili, mkuu wa mkoa alikuwa Mwenyekiti wa chama mkoani.

Ilikuwa kama vile kila mtu alikuwa mwachama wa TANU/CCM by default.

Ujio wa vyama vingi, mali zote hizo hazina uhalali kuwa za CCM. Bora ziwe za Halmashauri za miji husika. Labda kuondoa ofisi tu, lakini viwanja vya mpira ni mfano mzuri.
 

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
2,913
2,000
Viwanja vya mpira/michezo 8+
Ghorofa zenye kuanzia 3 na kuendelea 14+
Ghorofa mbili kushuka 10+
Viwanja vilivyo wazi vyenye ukubwa zaidi ya hekali 2 vipo 16+
Viwanja saizi ya kati 8+
Viwanja vidogo 24+
Nyumba saizi ya kati 36+
Nyumba ndogo 21+
Nyumba zenye fremu 58+
Vituo vya runinga 2
Kampuni chini ya chama 5+
Mashirika 4+
Shule 6+
Magari kama yotee
Watumishi kama wotee
Maafisa kama wotee
Askari kama wotee
Wanasiasa kama wotee
Single mothers kama wotee
Wasagaji kama wotee
Wasanii kama wotee

Swali: Vitu vyote hivi vilipatika kwa njia zipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom