Elections 2010 Ccm walisema elimu bure haiwezekani, leo wanasema bure??

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Jaman hii nchi inasikitisha, kama waziri wa Elimu anakuja na mpya bila kushirikisha wadau na taasisi za Elimu kuhusu mwanafunzi akimaliza std 7 avuke aingie moja kwa moja kidato cha nne. Hii ni kama ya Mungai kufuta michezo.

Wewe waziri shirikisha wadau jamani. Me naomba tushirikishe wadau haya masuala tusitumie siasa harafu baadae tuanze kulalamika. Hivi hii JK anasemaje??
 
Jaman hii nchi inasikitisha, kama waziri wa Elimu anakuja ......................... aingie moja kwa moja kidato cha nne. Hii ni kama ya Mungai kufuta michezo.

Wewe waziri shirikisha ...............??
Sijui mantiki ipi waziri Magembe katolea uamuzi huo, lakini mie nipo hapo kwenye rangi nyekundu - Mungai hakufuta michezo. Alifuta mashindano ya kitaifa ya UMISHUMTA na UMISETA tuu iliyokuwa inachukua mwezi 1 -2 kumalizika, kila mwaka, kwa wanafunzi kuchangishwa mchango wa UMISHUMTA/UMISETA iwe isiwe unacheza michezo! Michezo iliendelea kama kawaida na aliwaambia wahusika wizarani waje na program ya mashindano ya kitaifa ambayo haitamfanya mwanafunzi na mwalimu wa michezo (ambaye si ajabu anafundisha somo lingine), kuwa nje ya darasa kwa muda mrefu zaidi. Walishindwa na ndio waliokuwa wapayukaji wakubwa eti waziri kafuta michezo, lakini inawezekana pia kufuta mashindano ya kitaifa kuliingilia agenda na miradi ya watu fulani fulani wisarani humo! Think about it: michango ya TZs 1,000 kwa kila mwanafunzi uwe usiwe unacheza michezo, zidisha kwa idadi ya wanafunzi wa shule za msingi, for example, na kikubwa zaidi hiyo hela ilikuwa haina risiti, na wizara ilikuwa inatoa fungu kila mwaka kwenye budget yake kushughulikia mashindano hayo! Rudia hii tena kwa shule za sekondari na utaona ni bonge la mradi!

Kwa hiyo, the biggest misconception that Mungai alifuta michezo is false! Alichofuta ni mashindano ya kitaifa tuu. Fact!
 
Back
Top Bottom