CCM waliojiita wanamtandao bado wanataka kusifiwa nje ya utawala

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,542
2,000
Makamba alishika ukatibu mkuu baada ya Mangula. Likaundwa kundi lilioitwa wanamtandao. Wakawatenga wana CCM wengine. Mtu kama Mangula alisahaulika kabisa akawa mtu wa kijijini, Iringa. Nafasi ya katibu mkuu ikawa ni ubingwa wa vijembe, akajisahau na CCM ikakosa umaarufu akiwa hana habari.

Kinana kwa nafasi hiyo naye akadeka na kuwaita wengine mizigo. Akazunguka nchi nzima akiwalaani wenzake ndani ya chama. Wakaitwa magamba yanayostahili kuvuliwa. Skendo moja baada ya nyingine ikiwa ni pamoja na meno ya tembo, lakini hakuguswa hata siku moja.

Wakati huo huo mstaafu Mkapa aliwekwa kando. Akazomewa hata barabarani kwa kuamini aliharibu uongozi au kwa maana ya kuonesha kwamba wanamtandao walimshinda. Hata sherehe za kitaifa aliachana nazo kwa kuzomewa. Hakuwahi kurudi Ikulu eti kusalimiana na rais.

Imekuja awamu ya 5, wanamtandao hawaamini siyo zamu yao. Wanataka wafike Ikulu kila siku, umaarufu ubaki kwao, hawataki kutulia vijijini na niaonavyo, hawako tayari kuzomewa. Wanatukana kwa kukosa sifa za mwanzo. Wanajisahaulisha waliyowafanyia wenzao wa awamu ya 3. Wanataka waombwe ushauri wakati wao hawakuruhusu kushauriwa.

Kwa mtindo waliouanzisha, tuwaombe wakubali kwamba awamu yao imekwisha, wake pembeni. Wasilazimishe kutawala nchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom