CCM: Waliofanya fujo Zanzibar ni wapinzani (CUF) na ndio waliochoma ofisi za CCM na kufanya vurugu

Problem kubwa hapa ni kutamani maisha ya kiarabu na kutukuza misingi na fikra za kizungu,ndicho kinatupa tabu sana binadamu wa karne 20 & 21 hakuna kingine chochote.Kwani wapiganapo mafahali wawili zihumiazo ni nyasi (wafrika weusi ambao ni wepesi kusahau enzi zile za kufungwa minyonyoro na kutembea kilometa nyingi sana).Sasa wanapiganishwa ili waweze kutawaliwa kirahisi kikubwa zaidi ni kwamba hawajitambui kwani dini zimepumbaza akili na fikra zao.:hatari:
 
Kwani CUF ni wapinzani? Au ni kwa tafsiri ile ya JK aliposema wapinzani wanachochea mgogoro wa Malawi huku akijua waliotoa tamko ni Edward Lowassa, Samwel Sitta na Bernard Membe? Nini maana ya upinzani huko Zenji? Lakini si ni kweli Uamsho ni CUF? Chezea Ismail Juha wewe?
 
KWA NINI KISONGE WAWEWESEKA NA
CUF? Maskani ya KISONGE ndio kinara wa
kucheza ngoma ya baadhi ya
viongozi wa serikali/CCM ya
kupinga maridhiano ya wazanzibari,
serikali ya Umoja wa kitaifa na na
kujenga farka, fitna, chuki, ukabila, ugozi, chokochoko na uvunjifu wa
umoja na mshikamano miongoni
mwa wazanzibari imechomwa moto
kufuatiwa vurugu za hivi juzi
baada ya kutekwa nyara kwa
Sheikh Farid. Katia kuifanikisha azma hyo KISONGE na
wanamtandao wenzao wameapa
kutofautisha baina ya CUF na
harakati za UAMSHO. Kwa kuwa
usalama wa taifa wako dhidi ya
jumuiya ya UAMSHO hazikwepeki tuhumakua wao ndio
wanaotuhumiwa kuandaa kiufundi
mpango wa kumteka Sheikh Farid.
Pia hawawezi kukwepa tuhuma kua
ndio walioandaa kuchomwa kwa
maskani hiyo na nyengine ghafla bila ya kuchelewamara tu
ziliporipuka ghasia hapo juzi. Lengo kuu la mtandao ambao
maskani ya KISONGE linaufanyia kazi
ni kuizima nuru njema ya umoja wa
wazanzibari ambayo ndio silaha
pekee ya kuirejesha Jamhuri ya
watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili. Lengo ni lile lile linaliondaliwa
na system chini ya Jamhuri ya
Muungano na vibaraka wao wa
Zazibar kuwa wazanzibari
wasambaratike, wagombane,
wasiwe wamoja, wasiaminiane na wasisikilizane. Wanajua wazanzibari wakiwa wamoja
wanapata jukwaa na sauti ya
pamoja ya kujadili na kudai nchi
yao huku wakisahau mawazo ya
tofauti zao za kisiasa na badala
yake kuuhisi machungu ya kudhalilika kwa nchi yao.
Ukiwaondoa wazanzibari katika
maelewano na umoja huu kwa
kujenga mazingira ya kila upande
uone bado sisi ni maadui kumbe
baina yetu bila shaka unafanikisha mpango wa kuwagawa wazanzibari
katika agenda tunayoipigania. Naendelea kuwafahamisha vijana
wenzangu vita vya KISONGE ni dhidi
ya CUF na si vinginevyo. Hawana
vita dhidi ya UAMSHO. Sasa tu ni
kwamba wanaumia vyema mtaji
mpya wa UAMSHO. Wanajua inayoudhibiti umoja wa kitaifa na
mwenye engine ya mabadiliko
wanayoyapinga ni CUF. Hivyo
wanafanya kila wawezalo ili CUF
ionekane ndio chanzo cha vurugu
zote hizi, ndio mpangaji, msimamiaji na mtekelezaji. Lengo alo kuu ni
kujenga picha ya uongo kwa CCM
wenzao kuwa CUF si wenzeao na
hawako pamoja na CCM na
wameunda UAMSHO ili waihujumu
CCM/ serikali nje ya maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa. Hili
ndilo linalojengwa na mtandao wa
KISONGE. Kufikia hapo ni
kuwarudisha nyuma wale wote
wenye imani na maridhiano na
umoja wa kiaifa kutoka CCM waone kumbe CUF hawako katika mstari
wa maridhiano. Ndio maana CCM wa
KISONGE wanapindisha ukweli na
kuweka hoja "kwa nini vurugu hizi
zichome maskani za CCM pekee
kama kweli hazikufanywa na CUF?" Mimi sina imani kama maskani za
CCM zimechomwa na wafuasi wa
UAMSHO kwani tumezoea mara
zote kila kunapoashiria kuwepo
kwa harakati za UAMSHO kama vile
mihadhara askari polisi hujipanga kuzilinda maskani mbili za CCM,
KACHORORA na KISONGE. Siku
ambayo KISONGE iliyochomwa moto
askari walikuwepo wapi? Huu bila
shaka ni mpango uliopikwa vyema
yaani polisi wasije na badala yake kundi la vijana lipelekwe kutia
moto ili ionekana wametia moto
UAMSHO. UAMSHO ni taasisi ya kidini
na ilijitangaza wazi haina
mahusiano na chama chochote na
wafuasi wao ni kutoka vyama vyote. Katika kuifuta picha hii ya
kwamba UAMSHO hawana chama,
KISONGE walianza na uchokozi wa
kuandika machapisho ya kila aina
katika mabango yao ambayo
yanatoa ujumbe kuwa UAMSHO ni CUF. Sisi CUF kwa kufahamu
wanachokifanya huwa
hatuchokozeki. Tunaielewa vyema
dawa yao ni kuwadharau na kweli
tumewadharau wamedharaulika.
Lakini wako vijana wa UAMSHO ambao wanachokozeka kila ambapo
kisonge wanapoongeza kejeli na
mausi dhidi ya UAMSHO. Tuanazidi kuambia vijana hao kuwa
huo ni mtego wa KISONGE
Unaodhaminiwa na mtandao
ulioshtushwa na umoja wetu
wanataka muingie kichwa kichwa
katika mtego huo (kama hamjaingia) ili azma yao itimie.
Vipuuzeni vitimbi hivi na badala
yake busara na akili itumike
kupambana navyo. Viongozi wa CUF
mara ngapi wamekamatwa? Mara
ngapi wamefunguliwa kesi? Na mara ngapi wamefungwa
magerezani? Mbona
hawakuhamasisha mapigano? Na mbona wafuasi hawakuingia
barabarani kupigana? Kwa sababu
viongozi wanawalea wana CUF kwa
misingi ya busara na taratibu
sahihi za kupambana na mfumo huu
kandamizi. Ukikurupuka mfumo ndio unakutaka ili ukusambaratishe
kabisa. Mara baada ya KISONGE kuungua,
walitoa taarifa kupitia facebook
kuwa "jiandaeni MTENDENI (Makao
makuu ya CUF) wakati wowote
kuanzia sasa itawaka". Hii
inaonyesha wazi kuwa wao wako dhidi ya CUF kwani wanajua ndiko
ziliko fungua za kasha la
maridhiano na umoja wa kitaifa
wanazozitafuta. Kama hiyo haitoshi wamechapisha katika
kipande cha ubao wao wa uchezi
kilichobakishwa na moto "CUF OYEE, MAPINDUZI DAIMA"
wakimaanisha "hongereni CUF kwa
kutuchomea maskani yetu lakini
tunawambia MAPINDUZI DAIMA" Vijana tutulie tutumie busara,
makundi kadhaa wa kadhaa
yameshaandaliwa na system kamavile ubaya ubaya, mbwa
mwitu na kadhalika ili wafanye
hujuma nyingi kupitia jina la
UAMSHO na huku mtandao
wanahusisha UAMSHO na CUF.
Wazanzibari tunaotaka jamhuri yetu tutulie tufuate kamaba ya
pamoja, akitokea mtu akaikata hii
kamba ya pamoja tutapambana
nae kwa nguvu ya pamoja wakati
ukifika.
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa CCM walikuwa na jeshi la janja wili(may be ganja weed)CUF walikuwa na Blue Guard ,sasa baada ya ndoa yao watu hawa ,vijana wao wakawaacha pembeni ,kiukweli hawafit in kwa muundo wa siasa na serikali ya umoja wa kitaifa.

Nahisi watoto hawa(ganja weed&Blue guard) ndio wanafanya balaa zaidi wakisaidiwa na mdogo wao (uamsho )kipenzi cha mama yao (CUF).

Baba yao CCM hana la kufanya maana CUF mkewe,janja weed mwanawe wa kuzaaa,Blue guard mtoto wa mkewena uamsho kitoto chao kipenzi,japokuwa kaka mtu bara wameshaanza kukishughulikia kitoto chao( Akina ponda).

Huku nadhani itachukua muda ,maana utafikiri hao uamsho ni sheikh faridi pekeyake kwanini viongozi wenzake wasihojiwe kwa kina kuhusiana na kadhia nzima?tunasikia vihuni vya miaka 10-17 ndivyo vinakamatwa!
 
Yaani ni waongo wakutupwa.........Maana ukweli hawasemi kua wakati wanachoma moto askari walikua wanafanya nini nyuma yao..Mbona wanafiki sana
unafiki nini ...mbona ofisi za cuf hazikuchomwa
 
Huyo kiongozi aliyesema maneno hayo busara imemtoka na alikuwa akiropoka tu kwa kiwewe cha kuchomwa kwa ofisi ya CCM,mbona yalipochomwa makanisa hakusema ni wapinzani?

Busara imemtoka?? itamtokaje wakati hanayo??
Huyo kiongozi yupo "blank" kichwani kwake.
 
Problem kubwa hapa ni kutamani maisha ya kiarabu na kutukuza misingi na fikra za kizungu,ndicho kinatupa tabu sana binadamu wa karne 20 & 21 hakuna kingine chochote.Kwani wapiganapo mafahali wawili zihumiazo ni nyasi (wafrika weusi ambao ni wepesi kusahau enzi zile za kufungwa minyonyoro na kutembea kilometa nyingi sana).Sasa wanapiganishwa ili waweze kutawaliwa kirahisi kikubwa zaidi ni kwamba hawajitambui kwani dini zimepumbaza akili na fikra zao.:hatari:
nakubaliana na wewe asilimia mia .....hizi midini ni upuuzi tu ambao unawafanya watu washindwe kufikiri sawasawa..midini hii ya wazungu na waarabu ovyo kabisa tupa kule
 
nakubaliana na wewe asilimia mia .....hizi midini ni upuuzi tu ambao unawafanya watu washindwe kufikiri sawasawa..midini hii ya wazungu na waarabu ovyo kabisa tupa kule

Kama kweli mnadhani kuwa dini zote za uzunguni na arabuni ni za hovyo, iweje basi kukumbatia ustaarabu mwingine utokao huko? Elimu ya uzunguni, mavazi, vyakula, siasa, muundo wa serikali, n.k. Kwani basi kujichagulia vile uvipendavyo wewe na kudharau mawazo ya wengine? Kama una japo chembe ya busara pigania mila na tamaduni za kina mwanamalundi et al.
 
looooo........Hi ndoa vipi tena, inanikumbusha the Law of diminishing marginal utility maana nayo ina apply kwenye ndoa ( the more you had too much of the same thing, the lesser the apetite).
 
Back
Top Bottom