Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,704
- 9,060
Wana JF na Watz wote kwa ujumla,
Nina maswali machache lakini muhimu kwa Mwenyekiti wa CCM(T) na Rais wa JMT kwa tiketi ya CCM(Chama Cha Makinikia), Mhe. John Joseph Pombe Magufuli kuhusiana na huu mgogoro wa MAKINIKIA ambao kimsingi kabisa ulitengenezwa na CCM(Chama Chama Makinikia) kama ifuatavyo:

- Je, CCM walikuwa wapi miaka yote hii tangu mwaka 1998 ikizingatiwa kuwa mikataba yote hii ilikuwa ikisainiwa na Vigogo wa CCM?
- Rais Magufuli alikuwa ni sehemu ya Uongozi tokea mwaka 1995 kwa maana ya Mbunge na Waziri katika Baraza la Mawaziri ya Awamu ya 3 na 4. Je, hakuwa anayaona haya??
- Rais Magufuli anataka Watz tumweleweje anaposimama leo na kupingana na Marais wastahafu waliomtangulia ambao ni Wanamakinikia wenzake?
- Je, anaonaje sasa kama ataunda chama kingine cha Siasa mbali na CCM-Chama Cha Makinikia ili aiongoze Tanzania kwa sera za kupingana na CCM?
- Je, katika kuunda hizi kamati 2 za kukichunguza Chama Cha Makinikia-CCM amewasiliana na Marais Wastahafu Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee wa Msoga ambao kwa hakika kabisa ndiyo waliomwingiza Rais MAGUFULI hapo Ikulu ya Magaogoni?