Uchaguzi 2020 CCM walijikita kununua wapinzani wakaacha kuwekeza kwa wapiga kura

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Natabiri kuondolewa kwa katibu Mkuu CCM na katibu Mwenezi wa CCM Mara tu uchaguzi utakapomalizika.

Chama dola hakiwezi kuishi kwa kutegemea dola pekee bali kinapaswa kuyaishi wanayowaza na kuyataka wananchi.

Chama dola kilichojikita kutegemea dola hudhalilika ifikapo kipindi Cha kampeni, leo Geita imemtia aibu Mwenyekiti wetu, haiwezekani ukaongoza chama ukashindwa kujenga imani kwa watu wa nyumbani kwako.

Geita na Mwanza ilipaswa kuwa ngome ya CCM lakini tunashangaa Lissu anapata mapokeo makubwa zaidi hadi kufikia watu kutaka kulala alipolala yeye, hii Ni fedhea na ishara tosha kwamba lipo tatizo labda la sera za chama au uongozi uliopo kuanzia ngazi ya wilaya haukutokana na wanachama na wananchi.

Kufa kwa chama hakupimwi kwa ushindi wa kura, kura zaweza kuchakachuliwa na tume wakishirikiana na dola. Kufa kwa chama cha siasa nikuondoka mioyoni mwa watu.

Mugabe awamu yake ya mwisho alishinda kwa zaidi ya asilimia 80 ila alipoondolewa hakuna mtu aliyejitokeza kuandamana au kudai hakutendewa haki. Walimwacha, hii inamaana asilimia zaidi 80 zilitokana na dola na si uchaguzi.

Viongozi wangu wa chama, kubalini mmekiua chama kwa dharau na fedhea kwa wanachama. Mmekiua chama kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mlipokubali kuyokufanyika kwa uchaguzi, mmekiua chama pale mlipotuhusu watu kutoka upinzani kuingia CCM na kisha kuruhusiwa kugombea bila kupingwa mkisaidiwa na dola. Mmekiua chama kwa kujiona ninyi Ni viongozi na watu wenye upeo mkubwa kuliko wengine wote. Mmekiua chama pale mlipojipa madaraka yakuteu mnayejisikia ndiye awe mgombea.

Mmekiua chama pale mlipokubali kukataza wanasiasa wengine kufanya siasa mkabaki ninyi tu. Mmekiua chama pale mlipowabambikia wapiga kura kesi kisa hawaungi mkono chama. Mmekiua chama pale mliposhuhudia watu wasiojulikana wakiteka na kuua bila ninyi kukemea,waliotekwa na kuumizwa hata kuuwawa walikuwa shangazi, mama, baba, dada na kaka za wapiga kura. Mlipaswa kukemea mkakaa kimya Jambo lililowafanya watu kuamini damu yenu na uhai wenu ni muhimu kuliko wa wanyonge.

Leo mmegawanyika, Kagasheki tulimpotezea miaka 5 leo tunamnyanyua atuombee kura bila kujua yeye pia ana moyo.

Tuliowakata katika majimbo tunawalazimisha watuombee kura bila kujua nao Wana moyo na wangependa kuongoza. Tunawalazimisha tume wawapitishe wagombea bila kupingwa bila kujua mwangwi huu wa dhuluma unaenda kukita kwenye masikio ya wapiga kura.

Please please please, kuongoza siyo PHd Bali ni maarifa. Tulikosa maarifa tumebaki na dola ambayo dola mara nyingi hutumia nguvu kuliko maarifa.
 
Wanategemea kura za maruhani ziwatoe kimasomaso!
Maruhani yenyewe yamekufa
Screenshot_20200924-102138.jpg
 
Tulieni... porojo porojo tu
Awamu ijayo.. mengi yaja kuendeleza Hapa kazi tu!!!

Ushindi utawashangaza
 
Na bado wanafanya makosa yale yale...naona kwa sasa wanawekeza kwenye matamasha ya muziki na kuvalisha wasanii kofia badala ya kunadi sera..
 
Kununua wapinzani.. ulifanya wewe hewani.. siku nyingine weka proof sio kuturushia porojo za kijiweni
 
Mwamuzi mzuri ni tarehe 28/10 lakini kwa dalili inayoonekana kwenye mikutano ya kampeni baadhi uliyoyanena yawezekana kuchochea watu kutaka mabadiliko.
 
These words ain't just paid to go
In the one ear, out the other ear, No
 
Ni mpumbavu pekee anefikiri ile hama hama haijathiri chochote!

Hebu fikiria jimbo kama la Lijuakali chadema mnategemea kushinda?
 
Kama wanachama wa CCM 100 tu Tanzania wangu Kuwa na msimamo in public kama Huu mngekinusuru hichi chama! Ila kwa kweli wana CCM mmeamua kuacha kutumia akili kabisa!
 
Nimeongea na sister wangu anasema Lissu akienda Mwanza itafurika kwa nyomiiiii.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Kabisa mtu mwenye akili timamu anaamini magufuli atashindwa kwenye uchaguzi huu? Kabisa anaamini lissu atashinda na kuwa rais wa awamu ijayo? Haya ni maajabu kwakweli..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom